Tangazo

Pages

Sunday, June 3, 2012

ONESMO NGOWI ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI MKUTANO WA BERLIN UJERUMANI JUNI 2013





Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limeteua Rais wa Shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi,  Mtanzania Onesmo Ngowi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaa mkutano wa 30 wa Shirikisho hilo mwakani. Mkutano wa 30 wa IBF/USBA unatarajia kufanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni mwaka 2013.
 Ngowi alichaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la IBF/USBA uliomalizika Hilton Hawaiian Village Resort, jinini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 2 Juni. Uteuzi wa Ngowi unafuatia juhudi zake alizozifanya kuendeleza shirikisho hilo katika bara la Afrika tangu ateuliwe na Rais wa zamani wa IBF/USBA Robert Lee Sr. mwaka 1999 jijini New Jersey, Marekani. Onesmo Ngowi anakuwa mtu wa kwanza kutoka katika bara la Afrika kushika nyadhifa kubwa katika taasisi ya ngumi duniani na hii inaisaidia sana Tanzania na bara zima la Afrika kijitangaza vyema katika nyanja mbalimbali kama vile Utalii na bishara.
  Katika Kamati hiyo ya maandalizi kuna wajumbe sita nao ni ; Louis Priluker  wa Marekani, Roberto Rea wa Italia, Lahcen Oumghar wa Uholanzina Roberto Ramirez wa  Mexico. Kamati hiyo itafanya shughuli zake katika kipindi cha mwaka mmoja na itakutana mara 4 kwa mwaka. Sekretarieti ya Kamati ya Ngowi itakuwa katika jiji la New Jersey nchini Marekani kuliko na makao makuu ya shirikisho hilo duniani.
  Jiji la Berlin linasifika kwa uzuri wanndari zake pamoja na kuwa jiji la biashara la kimataifa katika bara la Ulaya. Mkutano huo ulianzimia kufanya mkutano wa IBF kwaka 2014 katika bara la Asia na mwaka 2015 IBF itafanya mkutano wake ktika bara la Afrika mahali ambapo patateuliwa.
  Ngowi  anawahimiza Watanzania ambao wako katika uandaaji wa mikutano kuchangamkia nafasi hii ambayo itawaleta watalii zaidi ya 1000 nchini toka nchi zaidi ya 200 duniani. Hii ni nafasi ya nadra sana katika biashara na watanzania ni muhimu wakachangamka kama wenzao wengine katika nchi zinazokuwa wenyeji wa mikutano kama hii.

No comments:

Post a Comment