Tangazo

Pages

Wednesday, June 20, 2012

MIYAYUSHO KUPIMA UZITO NA MMALAWI ALIHAMIS KWA AJILI YA MPAMBANO WAO IJUMAA

Pambano la masumbwi kati ya bondia Francis Miyeyusho na 
mmalawi John Massamba lilitakalofanyika ijumaa.  Katika ukumbi wa Vijana Kinondoni upo pale pale si kama baadhi ya watu wanavyolipoti akizungumza na mwandishi wa habari hizi Rais wa ngumi za kulipwa Nchini PST Emanueli Mlundwa amesema Mmalawi huyo kafika na watapima uzito siku ya Alhamis katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni Saa Nne asubui kabla ya mpambano wao utakaofanyika siku ya pili
Nae bondia kutoka malawi akizungumza kwa njia ya simu kutoka maeneo ya keko alipofikia amesema yupo tayali kwa mpambano na atahakikisha anamkalisha chini Miyayusho katika raundi ya sita tu bila kupoteza muda anajiamini kwa kuwa na rekodi nzuri ya mapambano 40 kapoteza 5 katika hayo kashinda kwa K.O, 6

Mpambano huo unausubiliwa sana kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini kufuatia kuwa miyayusho ajacheza mda mrefu sana tangia mwaka jana alivyopambana na bondia Mbwana Matumla


Nae Miyayusho amesema atapambana kufa na kupona ili aweze kuweka rekodi yake vizuri na aweza kuwafuraisha watanzania waliomkosa kumuona mda mrefu akipambana ulingoni


Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa





No comments:

Post a Comment