Tangazo

Pages

Saturday, June 23, 2012

MASHALI V/S SAMSON ULINGONI-Friends corner hotel jumapili

 Mabondia Thomas Mashali kushoto na Maisha Samson wakitunishiana misuli


Mabondia Thomas Mashali na Maisha Samson wamemaliza zoezi zima la upimaji na tayari kwa ajili ya mpambano wao utakao fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese siku ya jumapili 24/6/2012. mpambano huo wa ubingwa wa taifa wa TPBO uzito wa midle na unaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yasin Abdallah na katibu mkuu Ibrahim Kamwe umemalizika vizuri na mabondia wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa fight.
 
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Ibrahim kamwe na kueleza kuwa mabondia hao wote wawili kwa pamoja wamepata @kilo 71 na watacheza raundi kumi.

pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama ifuatavyo;

juma fundi(52kg) v/s shaban madilu (49.5kg) - watacheza raundi nane mohamed shaban'ndonga' (61kg) vs Musa hassan (61kgs) - watacheza raundi sita Jonas godfrey (61.5kgs) vs Venance mponji(59kg) - watacheza raundi sita Abdalah mohamed'prince naseem'(64kgs) vs Yohana Mathayo(65.5kgs)- raundi sita Nasoro Hatibu 55kg vs Abdul Athuman 55kgs -watacheza raundi nne
Martin Richard 50kgs vs Hassan Kadenge 49kgs -watacheza raundi nne

ngumi zitaanza kama kawaida kuanzia saa kumi jioni, na tunarudia tena kusema katika ngumi hakuna kupendelea na TPBO itasimamia kwa haki zote bila kuangalia mtu. tutakachoangalia ni mchezo kuchezwa kwa kanuni za ngumi na utoaji points kulingana na bondia anavyoscore kwa ngumi  halali sio kulingana na makelele ya washabiki



Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa

No comments:

Post a Comment