Tangazo

Pages

Friday, June 29, 2012

BIG RIGHT KUWAZAWADIA MABONDIA WAKE ENDAPO WATASHINDA



 Kocha wa ngumi wa Kambi ya mazoezi ya Big Right, Ibrahim (katikati) akiwa na mabondia wake wakati akiwasimamia katika Kambi yao ya mazozi ya pamoja kama timu kujiandaa na mapambano yao yanayotarajia kufanyika Julai 15 katika Ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es Salaam, mwaka huu.
********************************************

KATIBU wa Vijana wa CCM Kata ya Kinondoni, Rehema Mbegu, ameahidi kutoa zawadi ya Baiskeli kwa Mabondo wa Klabu ya Mazoezi ya Big Right ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, iwapo watashinda katika mapambano yao yanayotarajia kufanyika hivi karibuni, ili kuwa moyo zaidi vijana kuupenda mchezo wa Masumbwi.

Rehema mbegu, mara kadhaa amekuwa akishirikiana na vijana wa Kata yake katika masuala mbalimbali ya Kijamii na ya kuendeleza michezo, ambapo amekuwa karibu zaidi na vijana wa rika zote na kuwapa sapoti kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri kujishughulisha na michezo zaidi ili kuepuka kutojiingiza katika mkumbo wa matumizi ya madawa ya kulevya.

Mabondia hao baada ya kuhakikishiwa zawadi nono ya kila atakayeshinda kuibuka na Baiskeli, wamezidi kuwa na morali zaidi na kutoa ahadi zao kwa Katibu huyo kuwa watafia ulingoni hadi kieleweke kwa kutupa mawe ya ukweli kwa wapinzani wao watakaokutana nao siku hiyo ya pambano.

Vijana hi wamekwishaanza kambi yao ya pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja kama timu chini ya Kocha wao, Ibrahim Bigright na kuongeza muda wa mazoezi ambapo kwa sasa wanafanya mara tatu hadi kwa siku.

Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele, kutoka Kambi ya Matumla, katika uzani wa fly weight, Mwaite Juma kutoka Bigright Boxing,ambaye atapigana mkongwe Anthony Mathias,  katika uzani wa Bantam.

Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa ni kati ya JUMA
FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo kutoka kambi ya mzazi
 
Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa

Thursday, June 28, 2012

PAMBANO JINGINE LA UBINGWA WA TAIFA




kaike promotion imeandaa pambano lingine la ubingwa wa taifa kati BAINA MAZOLA na

Rajabu Mhamila

'Super D'

JUMA FUNDI(ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia nchini philipines) litakalopigwa jumapili ya tarehe 15 mwezi wa saba,pambano hili ni mtiririko wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi na wale tunaowategemea kwenda kuchukua mikanda mikubwa ya dunia.



 Inafahamika wazi kwa taifa letu,mchezo wa ngumi ni miongoni mwa mchezo unaopeperusha vema bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio na wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kishidashida bila ya utaalam mzuri wa uongozi utaalam upo katika uchezaji na mchezo unaohitaji msaada wa hali ya juu sana kuinuliwa.wadhamini wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa letu.



mchezo wa tarehe 15july utasimamiwa na Tpbo na mapambano yamepangwa na ibrahim kamwe chini ya uratibu wa kaike siraju yataongozwa na mapambano ya utangulizi kati bondia anaechipukia kwa kasi issa omar(toka bigright boxing mwananyamala) na Ramadhan kumbele bingwa wa taifa toka kambi ya matumla-keko.

Anthony Mathias(aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi mwaite juma(toka bigright boxing) mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini  na katika picha ni issa omar akinolewa na mwalimu wake Ibrahim bigright

DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim kamwe
TICKETS; +255 715 707777

Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round super feather weight - doi miyeyusho v/s shaban mtengela 6 round light weight - Bakari mohamed v/s sadiki momba - 6 round

Wednesday, June 27, 2012

BONDIA OMARI KIMWERI NABII ASIEKUBALIKA KWAO KUTETEA MKSANDA WAKE WA WBO JULY 13 ULAYA

BONDIA OMARI KIMWERI AKIWA AMEPOZI BAADA YA KUMALIZA MAZOEZI

BONDIA OMARI KIMWELI AKIWA AMEPOZI NA MMOJA YA WATU WAKE WA KARIBU
 B
Add caption
BONDIA OMARI KIMWERI WA PILI KUSHOTO AKIWA KATIKA MOJA YA POSTERS YANAYOTANGAZA MPAMBANO WAKE WA JULY 13

MTANZANIA BINGWA WBO WA NGUMI OMARI KIMWERI KUTETEA MKANDA WAKE JULY 13 ULAYA


MANNY PACQUAIO AIBUKA MBABE KWA USHINDI WA MEZANI

MANNY PACQUIAO WINS WBO AFTER 5 INTERNATIONAL JUDGES EVALUATION OF VIDEO.


Manny Pacquiao has won a WBO review into his split-decision defeat by Timothy Bradley earlier this month.
On the night two judges scored the bout 115-113 in the American’s favour, prompting boos around the MGM Grand.
The WBO has now met with five international judges to evaluate a video of the fight and they unanimously scored it in favour of Pacquiao.
The original result still stands as the WBO does not have to power to overturn it, but a rematch could be ordered.
It was a first defeat in seven years for Philippines fighter Pacquiao, who landed 94 more punches than Bradley.
Pacquiao is already guaranteed a rematch because of a clause in his contract.

Tuesday, June 26, 2012

SUPER D AITWA KUTOA UJUZI WA MASUMBWI IFAKALA,KILOMBERO



KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila

'Super D' amepata mwaliko wa kwenda kufundisha  pamoja na kuwapati ujuzi aliokuwa nao katika mchezo wa masumbwi mwaliko huo alioupata kutoka mkoa wa Ifakala mjini Kilombero kutoka kwa klabu ya Kilombero Boxing Klabu  ambaye mwenyekiti wake ni Hiyari Bohari na katibu wa Klabu Hiyo ni Ramadhani Mindu wamempatia mwaliko wa siku mbili

Kocha huyo kwa ajili ya kuwanoa Makocha na kuwapatia ujuzi wa ziada mabondia chipukizi mwaliko huo unaomtaka kwenda kutoa ujuzi wa mchezo wa masumbwi kwa kushirikiana na kocha kutoka mkoa wa Morogoro Boma Kirangi mafunzo hayo yanayotakiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agost yanaonekana kuwa na umuhimu kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kuwa na mwamko wa mchezo wa masumbwi nchini
Hata hivyo Super D 'alisema kuwa amepokea mwaliko kwa furaha na yupo tayali kutoa ujuzi wake alioupata wakati wa mafunzo ya kimataifa kwa vijana watakaojitokeza' Super D aliongeza kwa kusema mchezo wa maumbwi nchini unapendwa na wengi ila unakosa wafadhili kwa ajili ya kutoa sapoti mbali mbali Super D ametoa wito kwa makampuni mbalimbali  pamoja na wadau wa michezo kujitokeza kusaidia kwa namna moja au nyingine hususani mafunzo anayotaka kuyatoa akiwa mkoa wa Kilombero
Ambapo vijana wengi wanapenda kufahamu zaidi mchezo huo kwani kuna vijana zaidi walioamasika kucheza mchezo huo kwa kuwa na nia moja ya kuhakikisha mchezo wa masumbwi  unawafikisha mbali ya kuwa ni mchezo pia utawapatia ajira

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali

RAJABU MHAMILA 'SUPER D' NA VISIBITISHO VYA KUWA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI


CHETI CHA UTAMBULISHO WA KUFUZU MAFUNZO YA NGAZI YA KWANZA YA UKOCHA WA MASUMBWI KIRICHOTOLEWA NA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA RIDHAA NCHINI TANZANIA BFT  KWA RAJABU MHAMILA 'SUPER D' 
CHETI CHA UTAMBULISHO WA KUFUZU MAFUNZO YA NGAZI YA KWANZA YA UKOCHA WA MASUMBWI KIRICHOTOLEWA NA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA RIDHAA NCHINI TANZANIA BFT  KWA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'

CHETI CHA UTAMBULISHO WA KUFUZU MAFUNZO YA NGAZI YA JUU YA UKOCHA WA MASUMBWI  KIMATAIFA KIRICHOTOLEWA NA KAMATI YA OLIMPIC DUNIANI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA OLIMPIC TANZANIA YA KUMTAMBUA SUPER D NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

MOJA YA NEMBO INAYOTUMIWA NA SUPER D KUMTANGAZA KWA NJIA MBALIMBALI IKIWEMO FLANA ALIZOWAI KUTOA KWA MAKOCHA WENZIE WAKATI YUPO KATIKA MAFUNZO YA MCHEZO HUO KIMATAIFA



Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

MASHALI SASA AWATAKA CHEKA, KASEBA




Mashali akivalishwa mkanda wake wa ubingwa baada ya kuutetea jana kwa kumtwanga TKO raundi ya tano Maisha


Na Prince Akbar
BAADA ya kumtwanga kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya tano Samson Maisha wa Mbeya, bingwa wa Taifa wa TPBO, Thomas Mashali 'Simba wa Teranga' amesema anamtaka mshindi wa pambano kati ya Japhet Kaseba na Francis Cheka apande naye ulingoni, ili adhihirishe yeye ndiye ‘king’ wa ndondi Tanzania.
Mashali akiwa amemdondosha Maisha jana
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwenye ukumbi wa Friends Corner, Manzese jana baada ya ushindi wake huo, Mashali alisema kwamba anaamini kwa sasa katika nchi hii hana mpinzani na ameomba yeyote atakayeshinda kati ya Kaseba na Cheka asikwepe kupanda naye ulingoni.
“Huyu mtoto (Maisha), si saizi yangu, wamempakazia tu, baada ya kuona mabondia wote wa Dar es Salaam sasa hivi wananiogopa, nilikuwa nampiga huku namhurumia, na bado amefia katikati ya safari (raundi ya tano). Namtaka mshindi kati ya Kaseba na Cheka,”alisema Mashali.  
Katika pambano hilo la jana la uzito wa Middle, Mashali alimzidi uwezo mpinzani wake kuanzia raundi ya kwanza na katika raundi ya tano alimkalisha chini kwa ngumi kali ya mkono wa kulia.
Maisha alijitutumua kuinuka ili aendelee na pambano, lakini alionekana dhahiri hajiwezi na ndipo Kocha wake, Bagaza Mambane akarusha taulo ulingoni. Hata hivyo, Maisha anaonekana ni bondia mzuri akipata mazoezi zaidi na ujanja wa katika masumbwi.

TPBC INATAMBUA MKATABA WA CHEKA NA KASEBA JULAY 7

 

 



Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inatambua mkataba (mikataba) kati ya Francis Cheka na Kaike Siraju aliyosaini kupigana na Japhet Kaseba siku ya July 7, mwaka huu.


 Aidha Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamshauri bondia Francsi Cheka awe na mawasiliano mazuri na promota wa pambano hilo ili hali ya kutoelewana iliyokwisha kujitokeza imalizwe kwa manufaa ya tasnia ya ngumi nchini.

TPBC inawashauri wadau wote wanaotaka kufikia makubaliano na mabondia kutofanya hivyo nje ya utaratibu wa mchezo wa ngumi ambao ni kusaini mikataba mbele ya Kamisheni na wakili ili maslahi ya wote yalindwe.

Tunapenda pia kuwashauri mabondia wote kuacha tabia ya kusaini mikataba zaidi ya mmoja hususan wakati bado wakiwa na pambano mkononi.

Monday, June 25, 2012

BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA THOMAS MASHALI AMBWAGA MAISHA SAMSONI

BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA THOMAS MASHALI [aka-simba asiyefugika] jumapili usiku ktk ukumbi wa friends corner ulioko manzese jijini dsm alifanikiwa kuutetea vyema ubingwa wake wa taifa unaotambuliwa na TPBO- ktk uzito wa kati [MIDDLE]Pale alipomlazimisha bondia maisha samson kutoka mkoani mbeya kujiuzulu ktk raundi ya 5 ya pambano baada ya kumpa kipigo cha kikatili mpinzani wake huyo,PAMBANO LILIPANGWA KUWA LA RAUNDI 10 .
katika raundi za manzo za pambambo maisha alionyesha kummudu mpinzani wake vilivyo lkn mashali alicharuka mara tu raundi ya tatu ilipoanza na kufanikiwa kumuangusha mpinzani wake ktk raund ya 4 na ya 5 jambo lililopelekea maisha samson kuacha kuendelea na pambano ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kumpata zaidi iwapo angeendelea na pambano hilo
 refarii wa pambano hilo alikuwa sakwe mtlya

MAPAMBANO YA UTANGULIZI;-

UZITO-FLY KGS 50.8 [6 ROUND ]
JUMA FUNDI ALIMPSHINDA KWA POINTS SHABANI MADILU
[2] UZITO FEATHER KGS 57 [6 ROUNDS]
JONAS SEGU ALIMSHINDA BONDIA MKONGWE VENANCE MPONJI KWA POINTS

[3] UZITO SUPER LIGHT KGS 63.3  [6 ROUNDS]
ABDALLAH MOHAMEDI [aka prince Naseem] walikwenda sare na bondia yohana mathayo

[4] uzito wa light kgs 60.2 6 rounds
shaban mohamedi ndonga alimpiga bondia mussa hasani kwa knock-out ktk round ya kwanza tu ya pambano

Saturday, June 23, 2012

DVD MPYA HIZI HAPA KUPATIKANA KESHO Friends corner hotel-manzese siku ya jumapili 24/6/2012

 DVD YA MANNY PAQUAIO ALIYOPIGWA KIUTATA IPO INAPATIKANA
  1. DVD YA FLOYD MAYWEATHE MPAMBANO WAKE WA MWISHO KABLA YA KWENDA JELA NAYO INAPATIKANA KWA MAELEZO ZAIDI PIGA NAMBA 0713 406938,0787 406938,0754 406938 NA 0774 406938 AU FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI ULIZA SUPER D AU FIKA KLABU YA ASHANTI ILALA AU AMANA

MIYAYUSHO ALIVYO MSAMBALATISHA MMALAWI

Date: 2012-06-22
Venue: Kinondoni Vijana Hall, Dar es Salaam, Tanzania

John Masamba!!

Commission: Pugilistic Syndicate of Tanzania
Promoter: Twalib Assenga
 
[1] Bantamweight
Francis Miyeyusho WTKO round 5 of an 8 rounder VS John Masamba
-         Referee: Emmanuel Mlundwa; Judges : Pembe Ndava , Anthony Ruta, Ramadhan Basta.
 
[2] Super Fetherweight
Doy Miyeyusho WTKO round 2 of a 4 rounder VS Nasibu Joseph
-         Referee: Pembe Ndava
 
[3] Light Flyweight
Alphonce Rashid WPTS 4 rounds of a 4 rounder VS Nassoro Mbwiga
-         Referee: Pembe Ndava; Judges: Emmanuel Mlundwa 40 -36, Anthony Ruta 40-36, Ramadhan Basta 40 – 36
 
[4] Light weight
Amos Mwamakula WPTS 4 rounds of a 4rounder VS Rashid Ally
-         Referee: Omari Yazidu; Judges: Anthony Ruta 39 -37, Pembe Ndava 40 -36,Ramdhan Basta 39 -37  
 
[5] Super Featherweight
Cosmas Cheka WPTS 6 rounds of 6 rounder VS Obote Ameme
-         Referee: Pembe Ndava; Judges: Omari Yazidu 58 – 56, Anthony Ruta 58 – 55, Ramadhan Basta 59 – 54
 
[6] Light Flyweight
Yonas Thobias Lauka WTKO round 1 of a 4 rounder VS Said Madanda
- Referee: Omari Yazidu; Judges: Anthony Ruta , Pembe Ndava ,Ramdhan Basta
 
[7] Super Flyweight
Ramadhan Kumbele WKO round 1 of a 4 rounder VS Ramadhan Rashid
-         Referee: Ramadhan Basta, Judges: Omari Yazidu, Pembe Ndava, Anthony Ruta.
-         Regards,
 
FOOTNOTE: John Masamba FOUGHT BONIFACE STENA AT Bullets Grounds IN BLANTYRE, MALAWI ON MIKE CHITENJE PROMOTION 27 MAY 2012

HE FOUGHT GIBONS KAMOTA IN LUSAKA ON A ORIENTAL QUARRIES PROMOTION 23 MARCH 2012 BUT THOSE FIGHTS ARE NOT SHOWN IN boxrec.com

MASHALI V/S SAMSON ULINGONI-Friends corner hotel jumapili

 Mabondia Thomas Mashali kushoto na Maisha Samson wakitunishiana misuli


Mabondia Thomas Mashali na Maisha Samson wamemaliza zoezi zima la upimaji na tayari kwa ajili ya mpambano wao utakao fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese siku ya jumapili 24/6/2012. mpambano huo wa ubingwa wa taifa wa TPBO uzito wa midle na unaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yasin Abdallah na katibu mkuu Ibrahim Kamwe umemalizika vizuri na mabondia wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa fight.
 
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Ibrahim kamwe na kueleza kuwa mabondia hao wote wawili kwa pamoja wamepata @kilo 71 na watacheza raundi kumi.

pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama ifuatavyo;

juma fundi(52kg) v/s shaban madilu (49.5kg) - watacheza raundi nane mohamed shaban'ndonga' (61kg) vs Musa hassan (61kgs) - watacheza raundi sita Jonas godfrey (61.5kgs) vs Venance mponji(59kg) - watacheza raundi sita Abdalah mohamed'prince naseem'(64kgs) vs Yohana Mathayo(65.5kgs)- raundi sita Nasoro Hatibu 55kg vs Abdul Athuman 55kgs -watacheza raundi nne
Martin Richard 50kgs vs Hassan Kadenge 49kgs -watacheza raundi nne

ngumi zitaanza kama kawaida kuanzia saa kumi jioni, na tunarudia tena kusema katika ngumi hakuna kupendelea na TPBO itasimamia kwa haki zote bila kuangalia mtu. tutakachoangalia ni mchezo kuchezwa kwa kanuni za ngumi na utoaji points kulingana na bondia anavyoscore kwa ngumi  halali sio kulingana na makelele ya washabiki



Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa

Bondia Francis Miyeyusho amtwanga Malawi John Masamba

Bondia Francis Miyeyusho akimshambulia bondia kutoka Malawi John Masamba wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Miyayusho alishinda kwa K.O Raundi ya 5.picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia John Masamba kutoka Malawi akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana. Picha na www.superdboxingcoach,blogspot.com

Bondia John Masamba kutoka Malawi akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana. Picha na www.superdboxingcoach,blogspot.com
Bondia Obote ameme akioneshana kazi na Cosimasi Cheka
Bondia Miyayusho akisikiliza wimbo wa taifa wakati wa kuimba nyimbo za matasifa mawili
Bondia Rashidi Ali akioneshana kazi na Amnos Mwamakula wakati wa mpambano wao jana

MABABA WA CHEKA NA KASEBA WATAMBIANA


Baba Mzazi wa bondia Fransic Cheka , Bonifasi Cheka kulia akiwa amemkunja baba mzazi wa Japhert Kaseba, Josepher Kaseba wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuzungumzia mpambanbo wa watoto wao utakaofanyika siku ya sabasaba katika uwanja mpya wa Taifa. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baba Mzazi wa bondia Fransic Cheka , Bonifasi Cheka kushoto akizungumzxa na waandishi wa habari Dar es salaam lkeo kuusu mpambano wa mwanae utakaofanyika siku ya sabasaba kulia ni
Baba wa bondia Japhert Kaseba, Josepher Kaseba wa pili kushoto ni meneja matukio wa Dar Live na Promota wa Mpambano huo Kaike Silaju.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baba wa bondia Japhert Kaseba, Josepher Kaseba kushoto akipeana mkono na Baba Mzazi wa bondia Fransic Cheka , Bonifasi Cheka wakati walipokuwa wakizungumza na waandishi wa Habari Dar es salaam leo kwa ajili ya kutangaza mpambano wa watoto waoi utakaofanyika siku ya Saba saba.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Taifa. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, June 21, 2012

MABONDIA JUMA FUNDI NA BAINA MAZOLA KUONESHANA KAZI JULAI 15

Bondia Juma Fundi kushoto na Baina Mazola wakitunishiana misuri wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBO leo mpambano wao utafanyika julai 15 katikati ni Promota wa mpambano huo Kaike Siraju

RAMADHANI SHAULI AONESHWA MKANDA WA UBINGWA WA IBF AFRICA ATAKAOGOMBANIA IDDI PILI

 Bondia  Ramadhani Shauli akiwa ameushika Mkanda wa I.B.F Africa wakati ulipokuwa ukioneshwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwasili Dar es salaam jana ukitokea USA mkanda huo utakaogombaniwa na Shauli na bondia Sande Kizito kutoka Uganda utafanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Diamond Jubilee kushoto ni Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Madaraka Nyerere na Promota wa mpambano huoMkurugenzi wa Kitwe General Traders, Lucas Rutainirwa 
 
Ramadhani Shauli akiwa na mkanda wa ubingwa wa IBF Africa
Bondia  Ramadhani Shauli akiwa ameushika Mkanda wa I.B.F Africa wakati ulipokuwa ukioneshwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwasili Dar es salaam jana ukitokea USA mkanda huo utakaogombaniwa na Shauli na bondia Sande Kizito kutoka Uganda utafanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Diamond Jubilee kushoto ni Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Madaraka Nyerere na Promota wa mpambano huoMkurugenzi wa Kitwe General Traders, Lucas Rutainirwa 

BONDIA FRANCIS MIYAYUSHO KUPAMBANA NA NASSIBU RAMADHANI SIKU YA IDDY PILI


Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa

CHEKA KASEBA KUTWANGANA KATIKA TAMASHA


Wednesday, June 20, 2012

MIYAYUSHO KUPIMA UZITO NA MMALAWI ALIHAMIS KWA AJILI YA MPAMBANO WAO IJUMAA

Pambano la masumbwi kati ya bondia Francis Miyeyusho na 
mmalawi John Massamba lilitakalofanyika ijumaa.  Katika ukumbi wa Vijana Kinondoni upo pale pale si kama baadhi ya watu wanavyolipoti akizungumza na mwandishi wa habari hizi Rais wa ngumi za kulipwa Nchini PST Emanueli Mlundwa amesema Mmalawi huyo kafika na watapima uzito siku ya Alhamis katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni Saa Nne asubui kabla ya mpambano wao utakaofanyika siku ya pili
Nae bondia kutoka malawi akizungumza kwa njia ya simu kutoka maeneo ya keko alipofikia amesema yupo tayali kwa mpambano na atahakikisha anamkalisha chini Miyayusho katika raundi ya sita tu bila kupoteza muda anajiamini kwa kuwa na rekodi nzuri ya mapambano 40 kapoteza 5 katika hayo kashinda kwa K.O, 6

Mpambano huo unausubiliwa sana kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini kufuatia kuwa miyayusho ajacheza mda mrefu sana tangia mwaka jana alivyopambana na bondia Mbwana Matumla


Nae Miyayusho amesema atapambana kufa na kupona ili aweze kuweka rekodi yake vizuri na aweza kuwafuraisha watanzania waliomkosa kumuona mda mrefu akipambana ulingoni


Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa





Tuesday, June 19, 2012

THOMAS MASHALI KUTETEA UBINGWA WAKE NA BONDIA MAISHA SAMSON


bondia wa ngumi za kulipwa kutoka kyela mkoani mbeyaMAISHA SAMSON ameahidi kumtwanga mpinzani wake THOMAS
MASHALI kwa knock-out ya raundi ya 9 ktk pambano lao litakalo fanyika tarehe 24-06-2012 katika ukumbi wa FRIENDs- CORNER ulioko jijini dar-es-salaam.
ktk pambano hilo la raundi 10 thomas mashali atakuwa anatetea ubingwa wake wa taifa unaotambuliwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini tanzania chini ya rais wake YASSIN ABDALLAH -USTAADH.
Mabondia hao watapigana ktk uzito wa kati [middle kilo 72.5 .maisha amesema anasikia sana sifa za mashali anayejiita SIMBA ASIYEFUGIKA,lkn ajuwe siku ya pambano atamuonesha kazi ngumu na akamtaka mashali awe mvumilivu ulingoni kwani yeye ni tofauti na ambao mashawahi kuwapiga.
nina mapambano 8 ambayo sijapigwa hata pambano moja na nimepigana na mabondia wajeuji zaidi ya THOMAS MASSHALI ,na wanatoka nchi za malawi ,zambia na namibia ,hivyo siona sababu kwa nini nishindwe kumpiga THOMAS MASHALI na kumpora mkanda wake na kurudi nao kyela [mbeya] alijigamba bondia huyo kutoka mkoani mbeya.
kwa kumalizia nawataka wazawa wa mkoa wa mbeya waishio dar-es-salaam wafike kwa wingi siku hiyo ya pambano kushuhudia kiyama nitakachomshushia THOAS MASHALI. Alimliza kusema maisha samsom.
                                             
 mabondia wa ngumi za kulipwa tarehe 30-06-2012 ktk ukumbi wa community center watapambana na mabondia kutoka dar-es-salaam katika pambano lenye lengo la kumuenzi bondia magoma shabaani aliyfariki dunia hivi karibuni.promota wa pambano hilo  ndg ally mwazoa amesema sehemu ya mapato hayo yataisaidia familia ya magoma shabani.
na hii ni ratiba ya kuendelea na siyo ya muda ,tutajitahidi kufanya hivyo kila baada ya miezi 6 kwani magoma ameacha familia ambayo ilikuwa inamtegemea hivyo ni wajibu wetu sisi familia ya ngumi za kulipwa tendelee kuwa pamoja na familia yake.
hivyo ninawataka wapenzi wa masumbwi na wapenzi wa magoma shabani kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwa ajili ya kufanikisha lengo la mapambano haya
mapambano haya yatasimamiwa na TPBO
 Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Sunday, June 17, 2012

PAMBANO LA MATUMLA NA MRUSI LAOTA MBAWA



DAR ES SALAAM, Tanzania
BONDIA wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana Kwa jina la ‘Siberian Tiger’ ameingia mitini yeye na kocha wake baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot na kuonyesha kumuofia mpinzani wake Rashid Matumla wa Tanzania.

Kwa mujibu Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa  Afrika(IBF)hii ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia huyo kuingia mitini kwa woga.
Ngowi alisema Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.

“Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani (WBU)alisema Ngowi na kuongeza akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali ya juu.


Alisema Matumla  amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni  ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi huyo.

“Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali, wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la ‘The Rumble on the Mountain’ na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini  Marekani Deidre Lorenz ambaye atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi Juni 24 mwaka huu”alisema Ngowi.

Scott Quigg-Rendall Munroe: clash of heads means fight ends in draw



Scott Quigg

The WBA interim super-bantamweight title fight between Scott Quigg and Rendall Munroe ended in a disappointing technical draw on Saturday.
A clash of heads in the third round of the much-anticipated clash left Munroe with a deep cut above his right eye.
That gave referee Howard Foster little option but to end the contest early, as the scorecards can only be consulted after four completed rounds.
A rematch is expected to be arranged at a later date.
With an unbeaten 24-fight record, British champion Quigg entered the ring as favourite.
However, Munroe was aggressive from the outset and landed a uppercut on Quigg in the opening round.
Quigg immediately improved and battled back to have the better of the second, suggesting an enticing contest was set to unfold at Manchester Velodrome.
However, in the third round, as both boxers threw right hands a clash of heads resulted, and with blood pouring from Munroe's head the fight was stopped.
In the evening's main support fight, Ryan Rhodes failed to reclaim his European light-middleweight title after losing to Sergey Rabchenko.
The 35-year-old from Sheffield was knocked out in the seventh round by Belarusian Rabchenko, who is coached by Ricky Hatton.
Rabchenko's perfect record increases to 21 professional victories, while Rhodes drops to 46-6.

Saturday, June 16, 2012

MABONDIA WA TAIFA WAWAGALAGAZA WAKENYA

MABONDIA wa timu ya Taifa ya masumbwi nchini imewagalagaza mabondia wa Kenya wakati wa
Mashindano ya Kimataifa ya Ngumi ya kirafiki yaliyofanyika leo katika  uwanja wa ndani wa taifa ambapo mashindano hayo mbali na kutokuwa na mzamini yalikuwa na msisimko wa ali ya juu kutokana na mwamko wa mashabiki wa mchezo uho uliokuwa ukifanyika katika uwanja huo

Katika mpambano uho bondia wa Kenya Matayo Keya alimtwanga kwa point bondia kutoka Tanzania Said Hofu na bondia Frank Mnene alimtwanga John Christian wa TZ nae Bondia wa Tz  George Constantno alimtwanga Isack Meja

Na bondia wa kike kutoka Tanzania Sara Andrew alipigwa na bondia wa kike kutoka kenya Gronna Kusa katika atua nyingine bondia Denis Martin wa Tanzania alimtwanga  Kamau Ng'ang'a wa kenya na bondia Mohamed Chibumbuli alimtwanga Edwin Okongo wa Kenya

Katika hatua nyingine Viongozi wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Masumbwi Nchini Kenya wamefurai kuwepo hapa kwa ajili ya kujipima nguvu kwa kuwa ni jumuiya moja ya Afrika Mashariki ambapo mashindano haya yalikuwa yakitokea mara kwa mara kipindi cha nyuma ambapo mabondia wengi walikuwa wanakwenda kenya na wengine kuja nchini kwa ajili ya kupima viwango vyao

Nawo viongozi wa Chama cha mchezo wa Ngumi za Ridhaa BFT Mwenyekiti Michael Changalawe amesema mabondia wa Kenya wamejigalamia wenyewe kutokana na kutokuwepo na wazamini ambapo wengi wao wameupa kisogo kuzamini mchezo wa Masumbwi nchini unaopendwa na mashabiki wengi  hivyo amewataka wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia mchezo huu wa masumbwi