Tangazo

Pages

Tuesday, May 8, 2012

RAIS WA IBF KUSIMAMIA PAMBANO LA UBINGWA WA MABARA ACCRA,GHANA MEI 26



SHIRIKISHO la ngumi la  Kimataifa (IBF) limemteua Rais wa Shirikisho hilo katika bara la Africa, Onesmo Alfred Ngowi kusimamia pambano la ubingwa wa mabara linalotambuliwa na IBF.
Mpambano huo utafanyika katika jiji la Accra nchini Ghana tarehe 26 Mei kati ya bingwa wa mabara wa IBF Emmanuel Tagoe wa Ghana na mpinzani wake Antonio De Vitis wa Italy katika uzito wa Junior Lightweight.
Katika mpambano huo wa kutetea mkanda wa ubingwa wa IBF ambao unashikiliwa na Emmanuel Tagoe wa Ghana Ngowi atasaidiwa na waamuzi wengine kama ifuatavyo: Refarii: Roger Barnor (Ghana). Majaji: Francisco de Ruvo, (Italy), Andre Pasquier (France) na Shadrack Acquaye (Ghana).
Mpambano huo uliopewa jina la “NI Sasa au Hakuna Tena” bondia Joseph Agbeko wa Ghana atagombea mkanda wa dunia wa Organizesheni ya Ngumi ya Kimataifa (IBO) akichuana na bondia Michael Domingo wa Ufilipino katika uzito wa Bantam.
Bondia Josepgh Agbeko anayeishi katika mji wa Bronx katika jiji la New York nchini Marekani atakumbukwa kwenye mpambano wake mkali wa kugombea ubingwa wa IBF kati katika uzito wa Bantam kati yake na bondia Abner Mares wa Mexico tarehe 3 mwezi Augusti 2011 katika jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani ambako ilibidi warudiane mara ya pili baada yakutokea malalamiko ya kuonewa kwa Agbeko.
Hata hivyo bondia Abner Mares alimshinda tena Joseph Agbeko waliporudiana tarehe 18 November 2011 katika jiji la California, nchini Marekani.
Naye bondia Joshua Okine wa Ghana ambaye alikuwa bingwa wa mabara wa IBF katika uzito wa Middle kabla ya kupoteza ubingwa wake kwa kupandisha uzito atapambana na bondia Theofiilus Teteh pia wa Ghana kugombea mkanda wa WBO Africa.
Bondia Sammuel Amaoko a.k.a Bruno wa Ghana atapambana na bondia Sidney Siqueira wa Beazil kugombea mkanda wa WBO Africa katika uzito wa Heavyweight.
Mapambano haya yaliyoandaliwa na GoldenMike Boxing Promotions ya Ghana yatafanyika katika uwanja wa kimataifa wa El-Wak,jijini Accra nchini Ghana chini ya usimamiziwa Mamlaka ya Ngumi zaKulipwa ya Ghana (Ghana Boxing Authority, GBA)
Usimamizi wa Ngowi katika mpambano huu unakuja kipindi kifupi baada ya Francis Cheka wa Tanzania kuunyakua mkanda wa IBF Continental Africa Title katika uzito wa Super Middle tarehe 28 April mwaka huu!
Imetolewa na,
Onesmo A.M.Ngowi

No comments:

Post a Comment