Tangazo

Pages

Wednesday, May 23, 2012

KESI YA MINTANGA JUNI 11



Mintanga
MAHAKAMA Kuu yaTanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Juni 11 mwaka huu kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri wa kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), Shaabani Mintanga ya kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8. 
Kwa mujibu wa shajala ya Mahakama, kesi hiyo itaendelea kusikilizwa siku hiyo mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib, ambaye alikuwa akiisikiliza tangu mwanzo. 
Kesi hiyo iko katika hatua ya kusikilizwa mashahidi wa upande wa Jamhuri, ambapo mashahidi ambao wameshatoa ushahidi ni pamoja na Godfrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) , Charles Ulaya na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya ngumi, Nassoro Michael. 
Mintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2008, akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8.

No comments:

Post a Comment