Tangazo

Pages

Saturday, May 12, 2012

JELA ITAMFANYAJE FLOYD MAYWEATHER ABADIRIKE



LAS VEGAS, NV - MAY 05:  Floyd Mayweather Jr. addresses the media after his unanimous decision victory against Miguel Cotto after their WBA super welterweight title fight at the MGM Grand Garden Arena on May 5, 2012 in Las Vegas, Nevada.  (Photo by Ethan Miller/Getty Images)
Ethan Miller/Getty Images
Jela inaweza kumfanya vipi mtu?
Kwa marehemu 2Pac ilimuwezesha kupasua zaidi, na matokeo yake ilikuwa ni albamu kali daima ya disc mbili, All Eyez on Me.
Kwa Wesley Snipes, imemuangusha ile mbaya na kumhsusha umaarufu wake kwa haraka kuliko ilivyokuwa kwa Mike Tyson.
Kumzungumzia Iron Mike, kukaa kwake jela kulimfanya awe mwenye hasira na aliyechanganyikiwa na dunia.
Jela inaweza kusababisha athari kubwa kwa mtu anayekwenda kulala kwenye sero zake.
Kwa Floyd Mayweather anayetarajiwa kuishi jela kwa siku 87 kuanzia Juni 1, mwaka huu kwa kosa alilofanya mwaka 2010 la unyanyasaji, swali kubwa ni jinsi gani May Fedha atayakabili maisha ya jela.
Huku Money May akikadiriwa kuingiza kiasi cha dola za KImarekani Milioni 40 kwa ushindi wake dhidi ya Miguel Cotto, hajawahi kuwa maarufu duniani kwenye michezo kama ilivyo sasa.  Anafahamu hili, anapenda, na amekuwa akijitokeza kwenye vyombo vya habari na atahakikisha anadumu kwenye chati.

Floyd_mayweathers_jail_cell_will_look_like_this_originalHiki ni aina ya chumba cha jela ambacho Mayweather atakwenda kuishi.
Jinsi gani atakabiliana na maisha hayo?
Atakuwa jela wakati mpinzani wake mkubwa, Manny Pacquiao atakuwa akipigana na Tim Bradley. Pacman atakuwa ameishika dunia ya ngumi, wakati huo Mayweather anapanga foleni kwa ajili ya huduma za jela.

143836943_crop_340x234Ethan Miller/Getty Images
Atakuwa anatumiaje muda wake?
Atakuwa anazurura zurura tu muda wote, lakini hilo ni wazo zuri? Bila uwezo wa kufanya mambo yake aliyozoea katika maisha yake ya uraiani, atakuwa akifanya mazoezi.
Hiyo itakuwa ngumu? May Fedha aliongezeka uzito kabla ya pambano lake na Cotto, na kama hatakuwa makini ataongezeka zaidi. Wakati tukiwa hatujui mpinzani wake wa kwanza mara tu atakapotoka jela, kama atakuwaPacquiao, spidi ulingoni litakuwa jambo muhimu kuliko nguvu.
Kisha tena katika rekodi ya mapambano 43 bila kupoteza hata moja, Mayweather ni mtu safi na anayechukuliwa vizuri; hatakwenda kugombana ovyo kwa sababu hatakuwa na kitu cha kufanya.
Swali haswa kwa Mayweather, anaingia jela akiwa katika chati ya juu. Alikuwa akizungumzia kustaafu baada ya kumpiga Cotto, lakini tunajua bado hajaisha. Atapigana tena; swali pekee ni " nani atakuwa mpinzani wake?
Mayweather 'atapigika' jela? Atakuwa na hasira kuliko alivyo sasa? Kulingana na jinsi anavyoishi maisha yake sambamba na Ms. Jackson na 50 Cent, anaonekana aliyeridhika  na ana amani ya maisha. Je, hayo yatabadilika akiwa jela?

143943038_crop_650x440Al Bello/Getty Images
Kuna maswali mengi kuhusu May Fedha na maisha anayokwenda kuyakabili jela, lakini hakuna swali atakuwa mtu tofauti akitoka. Je, atakuwa mtu mzuri, au mbaya? zaidi tembeleahttp://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment