Tangazo

Pages

Tuesday, May 8, 2012

PAMBANO UBINGWA LA NGUMI LA UBINGWA WA TAIFA KATI YA RAMA KUMBELE NA JAMES MOKIWA


Wajasiliamali wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua nafasi ya kutangaza bidhaa zao katika pambano la ngumi la Ubingwa wa Taifa kati ya Rama Kumbele na James Mokiwa, litakalofanyika Mei 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, mwandaaji wa pambano hilo, T Asenga, alisema kuwa ameamua kutoa nafasi ya Meza 10 katika ukumbi wa Vijana siku ya pambano hilo ili waweze kutangaza bidhaa zao kupitia mashabiki na wadau watakaofika kushuhudia pambano hilo.
Aidha Asenga alisema kuwa ameandaa meza 10 ambazo Wajasiliamali watatakiwa kulipia kiasi cha Sh. 100,000/= kila meza ili kuweza kuonyesha biashara zao ambapo pia watakuwa wakionyesha kupitia Projecta zilizoandaliwa kwa ajili ya kuonyesha matukio yote ya ukumbini hapo.
Asenga amewataka wafanyabisharakujitokeza ili kujiandikisha na kuthibitisha ushiriki wao ili waweze kuingizwa mapema katika orodha ya matangazo.
''Iwapo wafanyabiashara watahitaji kutangaza ama kuweka matangazo ya biashara zao katika DVD na kurushwa siku hiyo ya pambano na DVD za mapambano ya ngumi watatakiwa kulipia kiasi cha Sh. 200, 000/='' Alisema Asenga, na kiingilio katika pambano hilo ni Sh. 4000 kawaid na 6000 kwa VIP.
KWA MAELEZO ZAIDI WAWEZA KUWASILIANA NA NAMBA ZIFUATAZO:- 0719 546 436/ AU 0684 232 617
Aidha Asenga alisema kuwa siku ya Mei 12 mwaka huu itakuwa ni siku maalumu kwa waandishi wa habari kufanya mahojiano na mabondia washiriki katika kambi zao za mazoezi na kuchukua picha za mazoezi, ambapo amewaasa mabondia kuwahi na kujiandaa kwa mavazi rasmi ya michezo siku hiyo.

No comments:

Post a Comment