Tangazo

Pages

Sunday, May 6, 2012

MAYWEATHER AMDUNDA COTTO NA KUWA BINGWA WA ASIEPIGIKA


 
 
BONDIA Floyd Mayweather Jr. ameendeleza ubabe baada ya alfajir hii kumtandika kwa pointi Miguel Cotto katika pambano lililokuwa kali na la kusisimua.
Mayweather alitumia kasi yake na ufundi kumshinda Cotto, ingawa haikuwa kazi nyepesi kwani mpinzani wake huyo alikuwa akitupa makonde ya maana na kushambulia mwanzo mwisho.
''Wewe ni bingwa hatari,'' Mayweather alimuambia Cotto ulingoni baada ya pambano. 'Wewe ni kinana wa nguvu ambaye sijawhai kukutana naye.''
Mayweather alitawala raundi ya mwisho, ya 12 akimnyanyasa Cotto na kujihakikishia kucheza mapambano 43 bila kupigwa. Tofauti na mapmabano yake mengi, Mayweather alitokwa damu puani mbele ya Cotto.
Majaji wawili walitoa pointi 117-111 na wa tatu akatoa 118-110, hivyo Mayweather ameshinda kwa pointi 116-112.
Mayweather aliyepigana wiki chache tu kabla ya kuingia jela ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu, alikutana na pambano gumu dhidi ya mplnzani ambaye anakwenda mbele wakati wote
Lakini alikuwa mwenye kasi na mjanja zaidi ya Cotto na alionekana kumvaa katika raundi za mwisho.
Katika raundi ya mwisho, Mayweather alipiga ngumi yake bora zaidi kwenye pambano hilo, uppercut ya mkono wa kushoto ambayo ilimuonekana kumuumiza Cotto. 
Mayweather, aliyeahidiwa kupewa dola za Kimarekani Milioni 32, alilazimika kupigana kila dakika katika raundi 12 za pambano dhidi ya mbabe huyo wa Puerto Rico. 
Mayweather atakuwa jela wakati Manny Pacquiao anapanda ulingo huo huo wa MGM Grand Juni 9, dhidi ya Timothy Bradley. Pambano tamu zaidi la ngumi wanalolisubir9ia wapenzi wengi wa mchezo huo duniani ni kati ya Mayweather dhidi ya Pacquiao, ambalo halijapangwa kufanyika.
Hii inatokana na msistizo wa Mayweather kutaka Pacquiao afanyiwe vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu, ingawa tayari Pacquiao amesema yuko tayari kufanya hivyo.
''Nataka kupigana na Pacquiao, lakini anahitaji kufanyiwa kwanza vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu kabla ya kupambana naye,'' alisema Mayweather.
Takwimu za makonde, zinaonyesha Mayweather alipiga ngumi 179 zilizofika kati ya 687 alizotupa na Cotto alipiga ngumi 105 zilizofika kati ya 506.
Cotto, ambaye sasa anakuwa amepigwa mapambano matatu 37, aliahidiwa kupewa dau kubwa zaidi katika historia yake ya kupigana, dola Milioni 8.

No comments:

Post a Comment