Wednesday, October 31, 2012
Tuesday, October 30, 2012
KOCHA WA NGUMI C. MZAZI KUWAPOZA MACHUNGU MABONDIA WALIODHURUMIWA NA PROMOTA KAIKE

Mabondia
hao wanatarajia kupanda Ulingoni Novemba 18/2012 huko maeneo ya Mabibo
katika ukumbi wa D.I.D, ambapo pambano hilo litakuwa ni la upinzani
kubwa kutoka na mabondia hao kutambia na kufikia kutaka kuzichapa kavu
kavu mtaani.
Akilizungumzia
pambano hilo kocha mzazi alisema kuwa mabondia hao wote ni wazuri ambao
wanaofundishwa na kocha mzuri mwenye uwezo mkubwa pia ni mabondia
wazuri
na ni tegemeo zuri la baadae.

Hivyo
basi Mwaite Juma, kutoka BigRight boxing gym atacheza na Baina Mazola wa
No talking gym katika pambano la raundi nane.
Na Pambano hilo kali litasindikizwa na Karim
Ramadhan (mdogo wa Nasibu Ramadhan-bondia bora wa mwaka) atakaecheza
na Martin Richard.
Siku
hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi ya kiushindani ya kuwekana sawa
nani zaidi ya mwingine kati ya mabondia wa mabibo na mwananyamala.
Tamasha Kuhamasisha Ngumi Mtwara
Bakari dunda akivishwa mkanda na mbunge wa mtwara baada ya kuchukuwa ubingwa huo katika ukumbi wa makonde
Tamasha la kuhamasisha masumbwi mkoani mtwara lilimalizika kwa
mafanikio mazuri kwa watu kuitikia na kukubali mapambano mengine mengi
ya ngumi kufanyika mkoani humo.
katika tamasha hilo lililosindikizwa na pambano la ubingwa wa taifa
la uzito wa unyoya kati ya Bakari mohamed'dunda wa blackmamba ya mtwara
alimshinda abdala seleman wa dar es salaam,
Nae mkongwe Rashid 'snake man" matumla alimshinda kiaina yake
bondia Patrick amote wa kenya katika pambano ambalo liliwasimua sana
mashabiki na kuwafanya kushindwa kukaa vitini muda wote wa pambano na
hasa pale mkenya alipokwenda chini kwa konde zito lililotupwa na matumla
baada ya kukwepa ngumi na kutupa hilo konde kwa kushtukiza,mwanzo
alianza taratibu na kuonekana kama mchovu kutokana na kitambi
alichonacho na kujikwaakwaa ulingoni lakini kadiri muda ulivyosogea
ndivyo alivyobadirika na kuonekana mzuri zaidi.
pambano jingine lililowaacha hoi wapenzi wa mtwara na kukaa kimyaaa
na kuduwaa kwa mshangao ni la haruna mnyalukolo wa dar na ashraf wa
blacmamba kwani ngumi zilipoanza tu walianza kwa nguvu sana na kutupiana
makonde mfululizo yaliyomuingia kila mmoja na kupelekana chini kwa zamu
na wote walivimba nyuso na kutokwa na damu baada ya kupasukapasuka
mpaka mwishowe ashraf spidi na uvumilivu ulipomshinda na kukubali
kuliachia pambano kwa kukataa kurudi ulingoni raundi ya nne pambano
lilikuwa la raundi sita.
Monday, October 29, 2012
BONDIA MTANZANIA SAID MBELWA KUGOMBANIA MKANDA WA WBO (World Boxing Organization) Intercontinental middleweight championship

Bondia Said Mbelwa waTanzania akipima uzito jana kwa ajili ya mpambano wake wa kugombania ubingwa wa WBO (World Boxing
Organization) Intercontinental middleweight championship na bondia kutoka against
Afghan-German boxer Hamid Rahimi
Bondia Said Mbelwa waTanzania akibusu bendera ya taifa mara alipowasili nchini against
Afghan kwa ajili ya mpambano wake wa kugombania ubingwa wa WBO (World Boxing
Organization) Intercontinental middleweight championship na bondia kutoka against
Afghan-German boxer Hamid Rahimi

Mabondia wa nchi ya Afghan-German Hamid Rahimi, kushoto , wakiwa
wanangaliana kwa usongo na Said Mbelwa wa
Tanzania wakati wa upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao wa leo
kugombania ubingwa wa WBO (World Boxing Organization) Intercontinental
middleweight championship fight in Kabul, Afghanistan,
Subscribe to:
Posts (Atom)