Tangazo

Pages

Saturday, December 26, 2015

NGUMI ZA KUFUNGULIA MWAKA KUFANYIKA FREDS CORNER MANZESE JANUARY 2

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Selemani Galile 'Selemani Toll' na Zumba Kukwe wanatarajia kuzidunda mwanzoni mwa mwezi ujao katika mpambano wa kufungulia mwaka 2016 kg 75 mpambano utakaofanyika january 2 katika ukumbi wa frends corner manzese

mpambano uho ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wao wa kwanza miaka mitatu  nyuma kutoka droo ambapo kila bondia amejigamba kumsambaratisha mwenzie

akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano uho ni maalumu kwa ajili ya kumaliza ubishi wa miaka mitatu ya nyuma mpambono walioutoa droo
hata hivyo siku hiyo kutakuwa na mapambano
 ya nguvu ambayo yatawakutanisha mabondia

 mbalimbali ambapo bondia Shomari Milundi atapambana na Hussein Mbonde uku Shedrack Ignas akikumbana na Abdalla Luwanje wakati Mwinyi Mzengela atakumbana na Mohamedi Kashinde na Ramadhani Maonya atakumbana na Said Faraji wakati Kelvin Majiba atakumbana na Ibrahimu Hamis 

Super D alisema kuwa wameandaa mapambano hayo kwa ajili ya kukuza viwango vya mabondia chipkizi na kuimalisha zaidi wale wenye uwezo kwa ajili ya kuwapatia mipambano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
Super D aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani za nguvu pamoja na ulinzi wa kutosha na ngumi zitaanza mapema ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi warudi majumbani mapema wakiwa na furaha ya mchezo utakaochezwa


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile



Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Friday, December 25, 2015

BONDIA THOMASI MASHALI ALIVYO USAMBALATISHA UFALME WA FRANSIC CHEKA MOROGORO

Mabondia wa kike Lulu Kayage kushoto na Mwanne Haji wakioneshana umwamba kastika mpambano wao wa ubingwa wa raundi kumi ambapo lulu kayage alibuka bingwa wa TPBC kwa kumpiga Mwanne kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Lulu Kayage kushoto akimtwanga ngumi Mwanne Haji wakati wa mpambano wao wa ubingwa Lulu alishinda kwa point katika mpambano uho wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Mwanne Haji kushoto akipambana na Lulu Kayage wakati wa mpambano wao Lulu alishinda kwa point

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa raundi sita Mbilinyi aslishinda kwa point mpambano uho Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa raundi sita Mbilinyi aslishinda kwa point mpambano uho Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA VICENT MBILINYI KUSHOTO SHABANI KAONEKA NA IMAN DAUDI MAPAMBANO WAKIMSHANGILIA USHINDI WA MBILINYI

Bondia Fransic Cheka akikwepa konde zito la Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika morogoro Mashali alishinda kwa point mpambano uho  SUPER D BOXING NEWS

Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Morogoro Mashali alishinda kwa point mpambambano uho wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Morogoro Mashali alishinda kwa point mpambambano uho wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Thursday, December 24, 2015

MABONDIA WAPIMA UZITO KUZIPIGA KESHO UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO

Bondia Vicent Mbilinyi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Deo Njiku utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro siku ya Desemba 25 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Deo Njiku kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa jamuhuri Morogoro kwa ajili ya sherehe za xmas Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Lulu Kayage akipima uzito

Mwanne Haji akipima uzito


Promota Kaike Siraju katikati akiwainia mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao siku ya desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Thomas Mashali na Fransic Cheka wakitambiana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE AKIPIMA UZITO

Wednesday, December 23, 2015

BONDIA VICENT MBILINYI HAPANIA KUMCHAKAZA DEO NJIKU DESEMBA 25 MOROGORO


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Vicent Mbilinyi wakati wa maandalizi yake ya mwisho kucheza na Deo Njiku Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya kupambana na Deo Njiku desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea na mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya mpambano wake wa Desemba 25

kwa ajili ya kupambana na Deo Njiku mpambano utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

mpambano uho wa raundi sita umekuwa na kivutio kikubwa
Mvuto wa pambano hilo unatokana na ukweli kuwa, linakutanisha mabondia wa vizazi tofauti, Mbilinyi akiwa ni bondia wa kizazi cha sasa, wakati Njiku akiwa mmoja wa mabondia wakongwe.
 uku Mbilinyi akiwa chipkizi  ambapo alisema maandalizi yake ni ya hali ya juu, nia ikiwa ni kuhitimisha utawala wa mabondia wakongwe.
"Niko kwenye mazoezi makali, chini ya kocha wangu Rajabu Mhamila 'Super D'. Nia ni kushinda pambano hilo na kuimalisha rekodi yangu ya mapambano niliyoshinda.
"Lakini pia, nataka kuhakikisha namchapa Njiku, ili sio tu kujenga heshima yangu, bali pia kumaliza utawala wa mabondia wakonge nchini. Hii itaongeza molari miongoni mwa mabondia vijana nchini," anasisitiza Mbilinyi


ambaye anatokea katika kambi ya Super D Boxing Promotion inayozalisha na kukuza vipaji vya vijana mbalimbali nchini na kuviendeleza katika mchezo wa masumbwi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Wednesday, December 16, 2015

SUPER D COACH AENDELEA KUWANOWA VIJANA

KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KULIA AKIFANYA MAZOEZI YA KUKAZA MISULI YA TUMBO NA MABONDIA VICENT MBILINYI KUSHOTO HASSANI KIWALE 'MORO BEST'




KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KULIA AKIFANYA MAZOEZI YA KUKAZA MISULI YA TUMBO NA MABONDIA VICENT MBILINYI KUSHOTO HASSANI KIWALE 'MORO BEST'



HASSAN KIWALE 'MORO BEST' AIBUKIA KWA SUPER D COACH

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hassan Kiwale 'Moro Best' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao desemba 25  katikati ni kocha Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwaongoza mabondia kufanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo kushoto ni Vicent Mbilinyi, Hassani Kiwale 'Moro Best' na Ibrahimu abass Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D' kulia akimwelekeza jinse ya kutupa makonde bondia Hassani Kiwale 'Moro Best' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wa ubingwa utakaofanyika desemba 25 na Selemani Bangaiza Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Hassan Kiwale 'Moro Best' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao ya desemba 25 mwingine ni kocha Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA HASSANI KIWALE 'MORO BEST' AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA RAJABU MHAMILA 'SUPER D

BONDIA HASSANI KIWALE 'MORO BEST' AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA RAJABU MHAMILA 'SUPER D

BONDIA HASSANI KIWALE 'MORO BEST' AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA RAJABU MHAMILA 'SUPER D

KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKIWA NA MABONDIA HASSANI KIWALE'MORO BEST' OMARI BAI NA VICENT MBILINYI






VICENT MBILINYI Bondia anayejipanga 'kumpopoa' Deo Njiku Desemba 25

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa desemba 25 na deo Njiku utakaofanyika jamuhuri mkoa wa Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
VICENT MBILINYI
Bondia anayejipanga 'kumpopoa' Deo Njiku Desemba 25
NA MWANDISHI WETU

UWANJA wa Jamhuri mjini Morogoro, utakuwa mwenyeji wa mapambano kadhaa ya masumbwi, yatakayofanyika Desemba 25 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu ya Krimas.
Moja ya mapambano yatakayorindima siku hiyo ni pamoja na lile linalomuhusisha Vicent Mbilinyi, atakayetoana jasho na Deo Njiku, pambano lisilo la ubingwa la uzito wa kilo 53, linalovuta hisia za wengi miongoni mwa mashabiki wa masumbwi.
Mvuto wa pambano hilo unatokana na ukweli kuwa, linakutanisha mabondia wa vizazi tofauti, Mbilinyi akiwa ni bondia wa kizazi cha sasa, wakati Njiku akiwa mmoja wa mabondia wakongwe.
Tanzania Daima limefanya mahojiano mafupi na Mbilinyi kuataka kujua alivyojipanga kuelekea pambano hilo, ambapo alisema maandalizi yake ni ya hali ya juu, nia ikiwa ni kuhitimisha utawala wa mabondia wakongwe.
"Niko kwenye mazoezi makali, chini ya kocha wangu Rajabu Mhamila 'Super D'. Nia ni kushinda pambano hilo na kutanua rekodi yangu ya mapambano niliyoshinda.
"Lakini pia, nataka kuhakikisha namchapa Njiku, ili sio tu kujenga heshima yangu, bali pia kumaliza utawala wa mabondia wakonge nchini. Hii itaongeza molari miongoni mwa mabondia vijana nchini," anasisitiza Mbilinyi

MSUKUMO KATIKA MASUMBWI

Katika miaka ya hivi karibuni takwimu zinaonesha kuwa masumbwi ndio mchezo wenye kuingiza pesa nyingi kuliko mchezo wowote duniani, ambapo kwa hivi sasa kinara wa utajiri kupitia mchezo huo ni bondia Floyd Mayweather.
Mkali huyo anafuatiwa na Manny Paquaio ambao wote ni mabondia wanaoshikilia nafasi mbili za juu za utajiri michezoni, huku  michezo mingine ikifuata.
Hiyo ndio sababu ya vijana wengi kuhamasika kujitosa katika mchezo huo, mmoja wapo akiwa kijana wa Kitanzania Vicent Mbilinyi, aliyezaliwa Septemba 5, 1992 mjini Musoma mkoani Mara akiwa ni mtoto wa nne katika ya sita wa mzee Alphonce Mbilinyi.
Alipata elimu yake ya msingi kuanzia mwaka 1999 katika Shule ya Mzimuni iliyopo Magomeni Dar es Salaam na kumaliza mwaka 2015.
Bondia huyu mahiri kwa ssa, hakupata bahati ya kuendelea na masomo kutokana na ukata wa familia, ambao ulimlazimu kuishia hapo, akiwa tayari ana damu za ubondia kutokana na kuupenda mchezo tangu akiwa anasoma darasa la kwanza.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mbilinyi alisema alianza kupenda mchezo huo akivutiwa sana na kocha Sako Mwaisege 'Dungu' ambaye alikuwa akifanya mazoezi ya ngumi na kujiunga naye kama kocha wake wa mtaani pale maeneo ya Magomeni.
Baada ya kujifua sana kwa mazoezi na mbinu mbalimbali, kocha huyo alimpeleka katika timu ya Ngome pale Mwenge alipokutana na kocha Thimos Kingu na baada ya kupigana sana katika mashindano ya ridhaa na kukomaa katika mchezo wa masumbwi
"Baadae mazoezi ya Ngome yakanishinda, ambapo nilikuwa naishi Kibaha, Pwani kwa hiyo nilikuwa natumia shilingi 5,000 nikawa nimeshindwa kutokana kukosa mtu wa kuniwezesha katika swala la nauli," anasema.
Mbilinyi anaeleza kuwa baada ya kutoka Ngome, kocha Sako Mwaisege akampeleka moja kwa moja kwa kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Super D ambaye mpaka sasa anampa makali ya mchezo huo.
Jukumu kuu la Super D likiwa sio tu kumfundisha, bali pia kumtafutia mapambano mbalimbali ndani na nje ya nchi, ingawa hajaanza kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, ila anategemea ipo siku atakuja kuvuka kwa ajili ya mchezo wa masumbwi.
Pambano la kwanza la Mbilinyi, katika ngumi za kulipwa lilipigwa Januari 30 katika Ukumbi wa Manyara Park, ambako alipambana na Kulwa Bushiri.
Mpaka na sasa Mbilinyi amecheza mapambano nane, akishinda matano kati ya hayo, ametoka sare mapambano mawili na kupigwa pambano moja, rekodi inayompa matumaini ya kuzidi kufanya makubwa.
Baadhi ya mabondia aliocheza nao ni Kelvin Majiba, Khalid Hongo, Saidi Mundi, Yusufu Mkali, Epison John, Haridi Manjee.

WITO KWA WADAU WA MASUMBWI

Bondia huyo anayaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kufadhili mchezo wa ngumi kama wanavyofanya katika michezo mingine, ambayo mpaka sasa ina wafadhili wengi hivyo kuwataka wengine wageukie masumbwi.
Anabainisha kuwa, iwapo wafadhili watajitokeza kwa wingi, kutasaidia vijana wengi kufikia malengo sio tu ya kuliletea sifa taifa, bali pia kujikwamua kiuchumi, hasa ukizingatia kwa sasa michezo, hususani ubondia ni ajira wanayoitegemea.
Bondia huyo pia ametoa wito kwa vijana mbalimbali kujiunga na mchezo wa ngumi, kwani kwa sasa unalipa, kama inavyothibitishwa sio tu na kina Mayweather na Pacquiao, bali pia vijana kibao wa Kitanzania ambao wameanza kufanikiwa kupitia ngumi.
Mbilinyi anaenda mbali zaidi kwa kuwashauri vijana kuacha uasherati na matumizi ya dawa za kulevya na uvutaji wa bangi, kwani unapunguza nguvu na kurudisha nyuma harakati za kimaendeleo za vijana, hasa wanamichezo.

WASIFU:
JINA KAMLI: Vicenti Mbilinyi
KUZALIWA: Septemba 5, 1992
ALIKOZALIWA: Musoma, Mara
MCHEZO: Ngumi za Kulipwa
MAPAMBANO: Nane


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnoa bondia Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Deo Njiku mpambano utakaofanyika siku ya desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS



Kocha wa kimataifa wa mchezio wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akifanya mazoezi ya nguvu na bondia Vicent Mbilinyi anaejiandaa kutwangana na Deo Njiku siku ya Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Saturday, December 12, 2015

BONDIA VICENT MBILINYI ANA UCHU WA KUWA BINGWA WA DUNIA

BONDIA VICENT MBILINYI


KATIKA miaka ya hivi karibuni takwimu zinaonesha mchezo wa masumbwi 'Boxing'  ndio mchezo wenye kuingiza pesa nyingi kuliko mchezo wowote Duniani ambapo kwa hivi sasa utajili huo unashikiliwa na bondia Floyd Mayweather akifuatiwa na Manny Paquaio ambao wote ni mabondia na namba zote mbili za juu wamechukuwa wao  michezo mingine ikifuata

hii yote ni dondoo tu zaidi hapa nataka kumzungumzia bondia chipkizi Vicent Mbilinyi 

bondia huyu alizaliwa tarehe 05/09/1992 Musoma Mara ni mtoto wa nne  katika  watoto sita wa familia ya Alphonce Mbilinyi

alipata elimu yake ya msingi kuanzia mwaka 1999 katika shule ya mzimuni iliyopo magomeni Dar es salaam na kumaliza mwaka 2015

ajapata bahati ya kuendelea na masomo kutokana na ukata wa familia kuwa na maisha magumu

Mbilinyi alianza kupenda mchezo wa masumbwi tangu anasoma darasa la kwanza ambapo alivutiwa sana na kocha Sako Mwaisege 'Dungu' ambaye alikuwa akifanya mazoezi ya ngumi na kujiunga nae kama kocha wake wa mtaani pale maeneo ya magomeni ambapo walikuwa wakijifunza mchezo uho kupitia Sako

baada ya kujifua sana kwa mazoezi na mbinu mbalimbali kutoka kwa kocha  aliamua kumpeleka katika timu ya ngome pale mwenge alipokutana na kocha Thimos Kingu na baada ya kupigana sana katika mashindano ya ridhaa na kukomaa katika mchezo wa masumbwi

baadae mazoezi ya ngome yakanishinda ambapo nilikuwa naishi Kibaha mkoa wa Pwani kwa hiyo nilikuwa natumia shilingi 5000 nikawa nimeshindwa kutokana sijakuwa na mtu yoyote wa kuniwezesha katika swala la nauli ambalo lilikuwa likinigalimu kila siku hata hivyo akuishia hapo

Mbilinyi anaeleza kuwa baada ya kutoka Ngome kocha Sako Mwaisege akampeleka moja kwa moja kwa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye mpaka sasa anafanya nae kazi ya ngumi kwa kumfundisha na kumtafutia mapambano mbalimbali nchini na nje ya nchi japo ajanza kutoka nje ya mipaka ya tanzania ila anategemea ipo siku atakuja kuvuka mipaka hiyo kwa ajili ya mchezo wa masumbwi

Mbilinyi alicheza mpambano wake wa kwanza katika ngumi za kulipwa january 30 katika ukumbi wa Manyara Park alipambana na Kulwa Bushiri mpaka sasa Mbilinyi amecheza mapambano 8 akishinda 5 droo 2 na sale 1

baadhi ya mabondia aliocheza nao ni Kelvin Majiba,Khalid Hongo,Saidi Mundi,yusufu Mkali,Epison John, Haridi Manjee,,

bondia huyo ambaye anapenda kuyaona makampuni mbalimbali yakijitokeza kufadhili mchezo wa ngumi kama wanavyofanya katika michezo mingine ambayo mpaka sasa ina wafadhili wengi ivyo kuwataka wengine wageukie katika mchezo wa masumbwi kwani kwa vijana kwa sasa ni ajira yao ambayo wanaitegemea kujikwamua kimaisha

bondia huyo pia ametoa wito kwa vijana mbalimbali kujiunga na mchezo wa ngumi kwani kwa sasa unalipa kwani wengi wa mabondia wameanza kufanikiwa kupitia ngumi

alitoa wito kwa vijana wenzie kuacha huasherati matumizi ya dawa za kulevya na uvutaji wa bangi kwani unapunguza nguvu kwa mwanamichezo yoyote yule awezi kujihusishwa na maswala hayo


KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA SUPER D AKIMNOWA BONDIA VICENT MBILINYI







VICENT MBILINYI BONDIA MWENYE UCHU WA KUWA BINGWA WA DUNIA

BONDIA VICENT MBILINYI AJIANDAA KUMKABILI DEO NJIKU DESEMBA 25

Bondia Ramadhani Maonya kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao ambapo Mbilinyi anajiandaa kucheza na Deo Njiku desemba 25 na Maonya anajiandaa kucheza na Said Faraji January 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ramadhani Maonya kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao ambapo Mbilinyi anajiandaa kucheza na Deo Njiku desemba 25 na Maonya anajiandaa kucheza na Said Faraji January 2SUPER D BOXING NEWS

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Maokola wakati wa mazoezi ya Mbilinyi kujiandaa na mpambano wake na Deo Njiku utakaofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Mohamed Muhunzi akipambana na Vicent Mbilinyi


Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Omar Bai wakati wa mazoezi ya Mbilinyi kujiandaa na mpambano wake na Deo Njiku utakaofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D ' kushoto akimfundisha bondia Vicent Mbilinyi jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'upcut' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake na Deo Njiku utakaofanyika Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKIWA NA BONDIA VICENT MBILINYI

Vicent Mbilinyi akifanya mazoezi na Rajabu Mhamila 'Super D'