Tangazo

Pages

Saturday, March 31, 2012

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA



MABONDIA Selemani Galile na
Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa
wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika
ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa
kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es
Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha
anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika
atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue
kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo
najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali
alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa
kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka
bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote
raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa
TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia
mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo
hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri
mpinzani


Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na
huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis,
Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roj Jones na wengine wengi

Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa
mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani
ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu
Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

Tuesday, March 27, 2012

TOMASI MASHARI AJIFUA KUMKABILI SELEMANI GALILE APRIL 9


Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kulia akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Tomasi Mashari akifanya Mazoezi leo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Selemani Galile litakalofanyika April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Saturday, March 24, 2012

MMCHEZO WA MASUMBWI WANOGESHA BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI LEO

 Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi, Rajabu Mhamila Super D kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa masumbwi mwandishi wa Chanal Ten Meshaki Nzowa

 Warembo warioshiriki katika michezo mbalimbali leo kutoka kushoto Mwali Ibrahimu, Ceciria Jeremia na Aneti Kagenda
 Super D Boxing Coach akiwa katika Bonanza hilo leo

 Super D boxing Coach akiselebuka na mwana dada Hadija Khalili






Thursday, March 22, 2012

CHEKA VS MAUGO WAONESHWA MKANDA WA UBINGWA LEO


Na Mwandishi Wetu

WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo Wametyambulisha  rasmi mkanda huo ambao utashindaniwa Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuanikwa kwa mkanda huo kutaashiria kupamba moto kwa ambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

"Tunauanika mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda," alisema Kaike.

Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.

Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.

Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha  Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.

Saturday, March 17, 2012

RAMADANI SHAULI GABRIEL OCHIANG WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO


Mabondia Ramadhani Shauli wa Tanzania (kushoto) na Gabliel Ochiang wa Kenya wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika KESHO katika ukumbi wa friens Coner Manzese.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ramadhani Shauli akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Gabriel Ochiang wa Kenya kulia picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Ramadhani Shauli wa Tanzania (kushoto) na Gabliel Ochiang wa Kenya wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika KESHO katika ukumbi wa friens Coner Manzese. picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya mabondia pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupima uzito leoBondia Gabriel Ochiang wa Kenya akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauli kushoto.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, March 16, 2012

BOXING REFEREE'S

Referee’s wetu wa Boxing 90% wengi wao sio competent to be a boxing referee, ufahamu wao ni mdogo mno ktk maswala ya boxing, wengi wanafanyia uzoefu kwa kuwa waliwai kucheza ngumi hapo nyuma, ila hawajawai kupata proper training yeyote ya boxing referee.
APPEARANCE:
Wengi wanavaa uniform hazipo smart, shart alijapigwa pasi, viatu hata kiwi awapigi, suruali ndio usiseme.
PST – uniform zao ni trouser black na shati white na necktie red
TPBO – trouser black, shati dark blue, tai black
TPBC – wanavaa kama PST isipokuwa tai zao ni black
KBF – Chama cha Habibu Kinyogoli, wao wanakodi marefa
Referee’s hawa kama nilivyoeleza appearance zao zinatia aibu, hata mgeni wa kheshima akija ni aibu tupu kwa kweli, Ally Bakari a.k.a Champion kama anavyojiita, yeye huwa anavaa suruari njiwa, chini kapiga rubber, shati chafu hataa pasi alijapigwa, umeona wapi suruari ikavaliwa na raba, waangalie marefa wa Intanationa fight wanavyo vaa na kupendeza.
DDC Kariakoo, Francis Miyeyusho na boxer mmoja kutoka Kenya, sanction by  TPBO, Yasin Abdallah Ustaz alimfukuza kwenye ring Antony Luta hasi officiate fight kwa kuwa hakuwa smart na akuvaa uniform za referee za TPBO, hapo nilimpongeza na inatakiwa hivyo awe na msimamo, uwo ni mfano mmoja tu hipo mingi.
REFEREE IN THE RING:
Referee anatakiwa kabla boxer awajapanda kwenye ring yeye refa aende dressing room akawakague na kuwapa maelekezo na sheria zitakazotumika, na kabla awajavaa gloves akague ndipo wazivae. alafu azi sign kwa sheria sasa, Maana glove zinavaliwa dressing room, zamani wanavaa kwenye ring, hili kwetu alipo na alifanyiki na hawajui na hawafahamu.
Boxers wanapopanda kwenye ring, baada ya taratibu zote kufanyika, kama national anthem kupigwa, na Ring announcer ‘ MC ‘ kutangaza kila kitu ndipo Refa anawaita boxers ktkt kuwapa maelekezo ya mwisho kabla fight aijaanza, na kuwakagua kama gumsheed wamevaa, protectors, groves kama zimefungwa vizuri na huwa anawaambia mengi tumezungumza kwenye dressing room, I want clean fight at all time, protect yourself at all time, watch you head at all time, Ukipiga punch chini ya belt hiyo ni low blow ukiludia nakata point, ktkt ya mkanda its ok, above belt it’s ok, when I say stop, unatakiwa kustop na usipige ngumi, break una break faster, touch gloves, boxers wana touch gloves wanaenda neutral corner ready for fight.
Referee wetu awajui haya wanaojua ni wachache sana ntawataja wanaojua wakati nafanya majumuisho yangu, wanaita boxer ktkt wanayowaambia madudu matupu,
Mfano mmoja, Antony Luta, Dimond Jubelee main card Mbwana Matumla vs Francis Miyeyusho, refa Luta alianza kuwaambia boxers sheria za 10 points system wakati wa score cards, kuwa mtu anaweza kuongoza ktk round 7 za awali ila akaja kupigwa round zilizpbaki pake mshindi atakuwa aliongoza mwanzo, alichemka vibaya sana mpaka watu wakaanza kumzomea, akupaswa awaambie hayo japokuwa alikuwa sawa, yaliyopaswa kuzungumziwa pale niliyoyaeleza hapo juu.
DURING THE FIGHT.
Kosa lingine wanalolifanya hawa marefa wetu wa sasa wakati fight inaendelea ikatokea boxer mmoja kapigwa punch kakaa chini, sheria unatakiwa umuhesabia one to eight awe amesimama, na kabla ujamuhesabia unatakiwa uwakikishe the other boxer yupo ktk Neutral corner ndipo uanze kuhesabu, na ikifika nane u make sure boxer keshasimama unatakiwa huu walk back hatua 3 then unamuita boxer akufuate, coming!!!, coming!!! Atakapokuja unamwambia are you ok! Alafu afute glove unamluhusu aendelee na fight,
Refa wetu haya awayafuati tumeshuudia mala nyingi boxer anahesabiwa wakati Yule mwingine ajaenda Neutral corner ilo ni kosa, huwezi kuhesabu wakati the other boxer ajasimama neutral corner, alafu wanahesabu mpaka 10 boxer ajasimama,
Mfano hai mmoja ni refa Emanuel Mlundwa, Dimond Jubelee, Juma Fund vs Fadhili Magia, Juma Fund kapigwa punch kali kaka chini, kahesabiwa mpaka 10, apart from 8, na Mlundwa aku walk back hatua 3 na wala akumuita Juma fundi afute, badala yake akawa anaongea nae mpaka kengere ikagongwa, kama mimi ningekuwa refa wa ile fight ile ilikuwa ni clean KO!
DROP OF GUMSHEED.
Kizuia meno kikianguka marefa wetu huwa wanaokota wenyewe kwa mikono yao ambayo hata gloves hawajavaa, wanamuwekea boxer mdomoni, hii ni hatari kwa afya ya refa na boxer mwenyewe, kizuia meno kile kinakuwa kimelowa damu, mate, na kimeanguka chini kwenye sakafu chafu watu wamekanyagakanyaga,
Unatakiwa kikidondoka usimamishe fight, huu make sure umevaa surgical glove’s mikononi, hiokote, ipeleke ktk corner ya boxer muhusika, trainer na 2nd wake wataisafisha na wao ndio wanaposwa kumvalisha boxer wao, kosa hili linafanyika karibu kila fight. Surgical gloves box moja la 100pcs wanuza elfu 6 tu rakini marefa wetu wanapanda ulingoni wakiwa awajavaa glove’s. alafu wanashika kwa mikono wanamuwekea boxer mdomoni ni hatari kwa afya yake,

CURRENT REFEREE’S
Omary Yazidu, Said Chaku, Abdallah Mpemba, Ally Bakari “Champion”, Antony Luta, Issa Makaranga, Ramson Basta, Kondo Nassoro, Pembe Ndava, Emanuel Mlundwa, Names Kavishe, Mark Hatia, Yasin Abdallah Ustaz, John Chagu na Lucas Msomba.
Hawo ambao nime wa bold ndio competent referee’s wa ukweli, International referee’s, wengi wao awaonekani sana siku hizi mpaka big fight or special event or special case peke yake.
Swala hao waliobaki nani kawapa urefa??????????????????????
Wamekuwa trained na nani????? Mkufunzi gani kutoka vyama vya ngumi vikubwa duniani aliekuja kuwa train hawa marefa wetu??
Serekali na BMT mnajua haya?? Kuwa hawa marefa sio competent, hawana hata certificate zinazowatambulisha kuwa ni profesionaer boxing referee’s
Ustaz Yasin Abdallah – President wa TPBO huko Tanga ktk fight zake alikuwa refa na Judge nani kampa kibali cha yeye kuwa refa??
Tunacheza na maisha ya watu, akifa mtu sasa hivi kwenye ring tunawafungulia kesi ya mauwaji. Ally Bakari “ champion “, Said Chaku wamekuwa trained na nani????
Huko nyuma tumeshuhudia boxers wakifa ulingoni kama Mandera Rajabu, Antony Ndaki na wengineo, sheria na watu walikuwa wamelala ila safari hii mtu akifa kwenye ring tunawashtaki, marefa, Judge’s, chama kilichotoa kibali na tuna appoint the best Lawyer in town. Refa yeyote atakae panda ulingoni kama hana certificate inayo mcertify kuwa ni boxing referee ajiandae.
Naomba kuwakilisha
Mdau.

MABONDIA WA KENYA TANZANIA KUPIMA UZITO KESHO KWA AJILI YA MPAMBANO

BONDIA Gabriel Ochiang kutoka Kenya amewasili Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika jumapili hii na bondia Ramadhani Shauli wa Tanzania utakaofanyika katika ukumbi wa Frensi kona Manzese jijini.Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini leo majira ya saa mbili na nusu asubui kwa basi la Akamba bondia huyo kutoka kenya amesema kuwa kama kawaida yake ajamuona Mtanzania wa kumbabaisha zaidi ya aliyekuwa bingwa wa Mabara bondia Mbwana Matumla kwa sasa sijaona bondia mzuri zaidi yakeMabondia hawo wanatalaji kupima uzito kesho kwa ajili wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa wa raundi nane Naye bondia Ramadhani Shauli akizungumza kwa njia ya simu amesema kwa sasa angalii anapigana na nani yeye amejidhatiti kuendeleza ubabe kwa bondia yoyote anayepigana nae na kwa kuwa nimepata mpinzani kutoka nje ya nchi hapa ndipo watanzania watakapo kiona kiwango changu cha mchezo wa ngumi kwa sasa hapa nchini akuna bondia wa kuni babaisha kwani karibia wote viwango vyao vidogo ndio mana nimemuomba promota aniletee mtu toka nje ya nchi na nimefurai sana kupangiwa mkenya na nipo fiti kwa ajili ya mpambano huo.

COW BELL WADHAMINI MICHUANO YA NGUMI TEMEKE

Katibu wa Chama cha mchezo wa ngumi Temeke Ali Mchumila akimkabidhi flana ya wadhamini wa michuano ya Wilaya ya Temeke CAW BEll Makamu menyekiti wa Mpira wa Kikapu Nchini , Phares Magesa

Bondia Haridi Kibavu (kushoto) akimrushia konde Mahafudhi Swai wakati wa mpambano wao ulioandaliwa na Chama cha mchezo wa Ngumi Temeke, Dar es salaam jana, Kibavu aliashinda Kwa Pointi.
Kocha wa Mchezo wa Kimataifa wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akimsindikoza Bondia Ibrahimu Class wa Amana kwa ajili ya kucheza Jana

Mabondia Hamadi Omari na Thomas Son wakioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi wakati wa mashindano yaliyoandaliwa na chama cha mchezo wa Ngumi TEMEKE

Wednesday, March 14, 2012

Bondia wa UKRAINE VITALI Klitschko kujikita kwenye siasa

KIEV, Ukraine
BINGWA wa uzani wa juu unaotambuliwa na Chama cha Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC), Vitali Klitschko amesema hana mpango wa kuwa bondia mwenye umri mkubwa kushikilia ubingwa huo na badala yake, amepanga kujikita kwenye ulingo wa siasa nchini Ukraine.
Shirika la Habri la Marekani (AP), lilimnukuu bondia huyo juzi alipohojiwa kwamba ataendelea kuzichapa kwa muda gani.
Akijibu swali hilo, bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 alisema haitakuwa muda mrefu na badala yake, atajikita kwenye siasa kutokana na kwamba nchini Ukraine kuna nafasi nyingi.
Mwaka 1994 bondia George Foreman, ndiye aliyeweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kutwaa ubingwa huo, akiwa na umri mkubwa wa miaka 45 na Klitschko, alisema kwa ujumla hataki kuvunja rekodi hiyo ya Foreman.
Kwa sasa Klitschko ndiye kiongozi wa chama cha upinzani kiitwacho 'Udar' (mgomo) na anataka kuwa meya wa mji wa Kiev nafasi ambayo aliikosa mwaka 2006, wakati alipowania kwa kauli mbiu ya kupiga vita rushwa ambapo amepania kuwa tena katika uchaguzi ambao utafanyika baadaye mwaka huu.

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA


MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani


Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi

Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D

Tuesday, March 13, 2012

MDAU WA MCHEZO WA MASUMBWI AZUNGUMZIA UPATIKANAJI WA BINGWA WA TAIFA

 






Tumeshuhudia vyama vyetu vya ngumi vikitoa mabingwa wao wa Taifa wa weight tofauti kimakosa, Bingwa wa Taifa hawezi kupatikana kwa points ktk round ya kwanza mpaka ya nne, unless by KO, rakini baadhi ya Mabingwa wanapatikana kwa points chini ya round nne za awali, huyo si bingwa halali wa Taifa.Tale of the tape:Inabidi watu watangaziwe tale of the tape ili watu wajue. Contents za Tale of the tape ni Age, Height, Arm length, Weight. Tunaambiwa kuwa ni ubingwa wa Taifa bila kuambiwa ni weight gani wanayopigania.Ring Record:Hakuna ring record za fight zote zinzopigwa ktk miaka hii, vyama vyetu havina record za maboxer wanaowapiganisha au wanafanya makusudi tu, na record za maboxer wanaweza kuzipata ktk www.boxrec.com ila wanapiganisha watu bila kutuambia sisi wadau record za boxers wote wanaogombania mikanda, Ring record contain – Won, Loss, Draw, KO and NC of each boxer to be announce before fight.Unified Rules:Hapa ndio kuna hilo tatizo ambalo nimeliona kuwa Bingwa wa taifa anapatikana chini ya round ya nne kwa points, kwa KO sawa hakuna ubishi anakuwa champion wetu kialali ila kwa points chini ya round hizo huyo si bingwa wa Taifa, hiyo fight inaamuliwa kama Technical draw. Sheria zinasema hivi:No 3 Knockdown RulesOnly Referee Can Stop the FightScore Cards At The End Of Round No. 4Can Not Be Saved By Bell In Any Round Tukianza na hiyo ya kwanza – No 3 knockdown rules, zamani boxer ukipigwa na kuanguka ukaesabiwa ktk round moja mara tatu basi automatical fight imekwisha na bigwa kutangazwa ila kwa sasa sheria hiyo is no longer applicable, mtu unaweza kuhesabiwa hata mara kumi ktk round moja na fight ikaendelea.Only referee can stop the fight- hii inajieleza ni referee pekee mwenye right ya kusimamisha fight na kumpa ushindi anaestaili. Ili linafuatwa hakuna shaka, boxer akizidiwa na kunaweza kuatalisha afya yake tumeona referee’s wetu wakisimamisha fight na wakitoa ushindi.Score card at the end of round no. 4 – Hapa ndio kuna madudu tupu, round no, 1 mpaka round no. 4 hapa uwezi kutoa mshindi kwa points ikitokea boxers wamegongana vichwa au any Incidental hiyo fight itaamuliwa Technical draw kuanzia round no. 5 hapo likitokea la kutokea ndio score cards zinapotumika. PST ntawatolea mfano mmoja, mwaka 2010 DDC Magomeni Kondoa ulikuwa ubingwa wao wa Taifa Bantam weight kama sikosei au superflyweight, boxers waligongana vichwa round ya 3, PST wakatumia score card za round 2 kumtangaza bingwa wao wa Taifa, baada ya kutoa Technical draw, huyo hakuwa bingwa wetu halali wa Taifa. Pili, mwaka 2007 Dimond Jubelee hall Hussein Pazi vs Deo Njiku, superfetherweight, waligongana vichwa round ya 2,Hussein Pazi alipasuka vibaya sana juu ya jicho, Referee Mlundwa akafuata sheria ya Only referee can stop the fight akasimamisha fight, wakatumia score card kutangaza mshindi akawa Deo Njiku badala ya kuwatoa Technical Draw, Ingawa baadae Deo Njuku alinyang’anywa mkanda kwa kuwa alizidi weight. Can not be saved by bell in any round – hapo zamani sheria mtu akizidiwa kengere ( bell 0 inaweza kugongwa kumuokoa asiendelee kupata kipigo waende for a break, ila kwa sheria za sasa kituhicho hakuna, PST tena wanafanya madudu, ntatoa mifano 2 ktk fight zake tena za ubingwa wa dunia Venue ; Dimond Jubelee, 2011Promoter : BawazirSuction board : WCTLocal suction by : PSTTitle : Intercontinental flyweight championshipBoxers : Juma Fundi vs Fadhili MagiaJuma Fundi alipigwa punch kali akaenda chini, Referee Mlundwa akaanza kuhesabu ilipofika 8, Juma fundi akawa bado fahamu azijarudi, Mlundwa akaendelea kuhesabu mpaka 10 still Juma Fundi Fahamu zilikuwa bado azijarudi, kukawa na delay karibu ya 1 minutes akiongea nae, ilikuwa ni clean KO Juma Fundi kapigwa, ila delay za Mlundwa na Yule Juma Fundi ni boxer wake Mlundwa Kengere ikagongwa Juma Fundi akanusulika, na hiyo punch ilimchanganya akashidwa kucontrol game, hata hivyo alipigwa kwa points.Same date, Main Card, Mbwana Matumla vs Francis Miyeyusho, World Title Bantam weight, Referee Antony Luta, Mbwana alipigwa punch kali akakaa akalewa delay ya counting na kengere ikamuokoa Mbwana na kuanzia hapo Mbwana akashidwa kulimiliki pambana japo kuwa alianza vizuri sana, na alimkalisha Francis ila ile punch ndio ilimchanganya hakashidwa kucontrol fight.NB: Mabingwa wetu wa Taifa wanapatikana ktk njia ambazo ni kinyume na sheria, vyama vyetu vya ngumi vinatakiwa kujipanga na kuwa train Referee’s wake, ikiwezekana waiombe serekali iwaitie mkufunzi wa kimataifa aje kuwapa proper training na wawe issued na certificate otherwise itakuwa tunapata mabingwa ambao awana vigezo. Na vyama vyetu vya ngumi vi accept hizi challenge na wazifanyie kazi, Otherwise ipo siku tutawashtaki mahakamani. MdauNawakilisha

Sunday, March 11, 2012

MDAU WA NGUMI ATOA ANGALIZO LA SHERIA KWA NGUMI ZA KULIPWA




Kupambanisha boxers zaidi ya mara tatu ni makosa kisheria, hapa kwetu tunafanya kwa kutojua sheria au kwa mapromoter kutengeneza pesa. Wadau tumeliona ilo na tukiendelea kukaa kimya tutalitia aibu Taifa.
International fight zote zinaruhusu re-match na grand final after re-match, mfano Manny Pacquiao vs Erick Morales game ya kwanza alipigwa Many paquiao kwa points, akaomba re-match akashinda Manny Pac kwa KO round ya kumi. Elick Morales akaomba grand final re-match akapigwa KO round ya 3, akataka tena re-match sheria zikambana mpaka leo anataka kurudiana na Manny Pac ila walishamaliza three times fighting.
Mfano mwingine Manny Pacquiao vs Juan Manuel Marquez game ya kwanza draw, ikaja re-match akashinda Manny pac kwa points, Marquez akaomba grand final re-match ikapigwa akashinda Manny pac kwa pints ilikua very close fight, mpaka leo wanataka re-match ila sheria za boxing zinawabana haiwezekani tena.
Riddic Bowe vs Evender Holifield zimepigwa three times, moja draw mbili alipigwa Evander, na Evander alitaka re-match ikashindikana kwa kuwa walishamaliza zile three times fighting na awawezi kupigana tena. Na mifano mingi tu ila hiyo michache inatosha.
Hapa kwetu tumeshuudia boxers wakipigana zaidi ya mara saba na watu kwa kutojua sheria wanaona ni jambo la kawaida ila ni makosa kisheria, vyama vyetu vya ngumi PST, TPBO, TPBC ect, baadhi vinajua hilo na baadhi havijui hilo kabisa. Ni makosa kupiganisha watu zaidi ya mara tatu.
Rashid Matumla vs Maneno Osward wamepigana zaidi ya mara 5 au 6 na bado wanataka kupigana tena je hapo sheria zinafutwa au wanatubuluza???????
Francis Cheka vs Rashid Matumla wameshapigana zaidi ya mara 4 na bado kuna plan ktk mwaka huu kuwapiganisha tena.
Mada Maugo vs Francis cheka, walipigana PTA akapigwa Maugo, akaomba re-match zikapigwa Morogoro Jamuhuri akapigwa tena Maugo, sasa wameingia ktk grand final zitapigwa tena April tunaomba game hii iwe ya mwisho kwao la sivyo tutawashtaki mapromoter na chama chochote kitakachotoa kibali kwa ajiri ya fight nyingine baada ya hii ya April.
Mbwana Matumla vs Francis Miyeyusho wameshapigana mara tatu wameshamaliza ila wanataka kuandaliwa pambano la nne, je ni sheria zipi zinazofuatwa hapo.
Vyama vya ngumi za kulipwa walitazame hili kwa makini mkubwa sana tena sana, kama sheria awazijui basi waulize au waingie ktk mitandao waangalie na kufuatilia International fight na sheria zake, sio kubuluza watu na huku wanafanya madudu.
Naomba kuwakilisha!
Mdau wa boxing

Friday, March 9, 2012

CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI CHATAMBULIKA KIMATAIFA

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Dunia la ngumi za kulipwa  (WPBF) limempa hati ya kuwa mwakilishi wa Shirikisho hilo nchini Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa nchini (TPBO).
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kwa mtandao na Rais wa TPBO  Yassin Abdala 'Ustadhi' ilisema kuwa Shirikisho hilo lenye makazi yake nchini Marekani limempa hati hiyo ambayo itamruhusu kutoa taarifa muhimu za jinsi mabondia wa ngumi za kulipwa wa Tanzania wanavyoingizwa katika viwango vya Shirikisho hilo.
Alisema, sambamba na hilo pia litawasaidia mabondia watanzania kuweza kupata nafasi ya kugombea mikanda ya Shirikisho hilo.
"Ni jambo zuri kwa mabondia watanzania kwani watakuwa wanajua kila kitu kuhusu viwango vyao kuingizwa katika Shirikisho hilo lakini pia kupata nafasi ya kuwania mikanda hiyo ambayo itamsaidi kutambulika Ulimwenguni," alisema.
Sambamba na hilo pia Ustadhi amempongeza Mpiga picha wa Kampuni ya Business Times Limited inayochapisha magazeti ya Majira, Spoti Starehe na Business time,pamoja na Jarida la Maisha, ambaye pia ni Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi, Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mchango wake katika kuhakikisha anaukuza mchezo wa ngumi bila kubagua.
Alisema, Super D  amekuwa ni  msaada mkubwa sana katika kila maandalizi ya mchezo kwa kuwasaidia waandaaji ambao hupungukwa vifaa vinavyohusu mchezo hususan glovus na vifaa vingine.
Sambamba na hilo amekuwa akifuatilia mapambano ya ngumi popote pale hata mkoani ,na huku akiyaripoti yote yanayofanyika huko nje ya Dar es salaam kwa galama zake mwenyewe.
"TPBO tunayo macho yenye kuona na kuthamini michango ya watu wa aina yako hivyo tunakuahidi kukupatia cheti cha kuthamini mchango wako katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi  katika wakati muafaka," alisema.
Aliongeza kuwa yapo mengi ya kumshukuru kwani pia ameakuwa akiwasaidia mabondia wa mikoani kwa kuwauzia vifaa vya mchezo kwa bei ndogo kuliko hata ile ya madukani , hivyo kuwawezesha mabondia hao kuwa na uwezo wa kumiliki vifaa vya ngumi kiurahisi.

WANAFUNZI WA SHULE ZA MOSHI WAMWANDIKIA BARUA RASHID MATUMLA!!

Wanafunzi wanne wanaosoma katika shule za msingi na sekondari za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wamemwandikia barua bondia Rashid “Snake Man” Matumla wakimtakia kila la kheri katika mpambano wake na Vitaly “Siberia Tiger” Shemetov wa Urusi. Wanafunzi hao Levina Joachim(Shule ya Msingi Mwereni), John Makupa (Mawenzi Secondary), Ashura Omari (J.K Nyerere Secondary) na Oliva Philip (Shule ya Msingi ya Majengo) wamemwelezea Rashid “Snake Man” Matumla kama tegemeo kubwa la Taifa. Ifuatayo ni baadhi ya sehemu za barua zao:

“Mpendwa Golden Man, kama katika riwaya ya Sinderela natamani ungekuwa Prince wangu ninayekungojea unichukue katika mikono yako” alisema Ashura Omari katika barua yake. “Nakutakia ushindi mnono ili utimize ndoto zangu za wewe kuwa shujaa wangu kwa kumwonyesha Tiger huyo wa Siberia kuwa Tanzania tuna mabingwa wa kweli” Ashura Omari alimalizia katika barua yeke.
Oliva Philip alisema “Ni muda mrefu mji wa Moshi haujaweza kushughudia burudani kama utakayoileta wewe hivi karibuni. Naamini kuwa utaendelea kuungarisha mji wa Moshi ili kweli ujulikane kuwa ni kilele cha Afrika”
Naye Levina Joachim alisema “Golden man wewe ni nuru ambayo Tanzania iliipoteza kwa muda mrefu na tunakutegemea kuwa utairudisha na kuifanya ingare kila siku, nakutakia ushindi mzuri”
John Makupa alisema “Ningekuwa na uwezo ningekuja ulingoni siku hiyo nikakusaidia kushika mguu mmoja wa Tiger huyo wa Siberia ili umchakaze vizuri, lakini naamini kuwa utamuonyesha kuwa kweli wewe ni moto wa kuotea mbali”alisema Makupa.
Mpambano wa ngumi kati ya Rashid “Snake Man” Matumla na Vitaly “Siberian Tiger” Shemetov wa Urusi umeanza kuwa ni gumzo kubwa katika Manispaa ya Moshi huku wenyeji wengi wakifurahia na kungojea kwa matumaini makubwa ushindi wa Matumla siku ya tarehe 22 Juni mwezi wa sita.
Mpambano huo ambao utakuwa ni wa TPBC International Title katika uzito wa Super Middleweight utawakutanisha miamba miwili ya ngumi duniani. Mgeni mashuhuri katika mpambano huo atakuwa mcheza sinema mashuhuri wa Marekani Deidre Lorenz toka katika jiji la New York.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mpambano wa ngumi hapa Tanzania na Afrika nzima kuhudhuriwa na mcheza sinema mashuhuri kutoka Hollywood, nchini Marekani hivyo kulipa pambano hili sura mpya kabisa.
Bibi Deidre Lorenz atakuwa njini Moshi kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 17 Juni na pia kushiriki katika mbio za 22 za Marie Frances Mount Kilimanjaro Marathon ambazo zimepewa hadhi ya kuwa “Mbio za Marathon za kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB).
Mpambano huu una promotiwa na kampuni ya ASMM Peak Gemstone Traders LTD ya mjini Moshi na utajumuisha pia mabondia kadhaa kwenye mapambano ya utangulizi:
Pascal “Prince Kilimanjaro” Bruno atapambana na James “Sura Mbaya” Kitasi wa Kenya katika uzito wa Light Middle raundi 10 ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Bruno atakuwa anatetea mkanda wake wa ubingwa wa Afrika ya Mashariki.
Naye Alibaba “Dragon” Ramadhani atatetea mkanda wake wa Afrika ya Mashariki akichuana na Sebyala Med toka nchini Uganda katika uzito wa Middle

BONDIA WA ZAMANI,OSCAR DE LA HOYA AWA , AWAPAMBANISHA MOSLEY NA ALVAREZ

Bondia wa Mexico, Saul Alvarez (kulia) aka "Canelo" na
Mmarekani, Sugar Shane Mosley wakitazamana wakati promota na bondia wa zamani
Oscar de la Hoya (katikati) akiwatambulisha kwenye mkutano na Waandishi wa
habari mjini Mexico City kwa