Tangazo

Pages

Friday, July 29, 2011

MABONDIA WA ZANZIBAR NA BARA KUONESHANA KAZI DDC KEKO KESHO



  1. Alphonce Mchumiatumbo akipima uzito Dar es Salaam jana kwa ajili ya mpambano wake KESHO na Amour Zungu utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Keko leo kulia ni msimamizi wa mabondia hawo. Kanda Kabongo

TENDE HIZOOOO MSIMU WAKE UHO EHEEE

Wafanyabiashara ya tende wakipima kwa kilo kwa ajili ya kuweka kwenye mifuko kuuza kushoto ni Sadam Mubaraq na Said Makingo kama walivyokutwa makutano ya mtaa wa Mafia na Swahili DAr es Salaam jana zao la tende upendwa kununuliwa sana katika kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani itakayoanza mwanzoni mwa mwezi ujao

Tuesday, July 26, 2011

Mbwana Matumla Kuzichapa na Francis Miyeyusho Jijini Dar es Salaam


KUSHOTO NI BINGWA WA UBO ANAYETETEA MKANDA WAKE MBWANA MATUMLA NA KULIA NI MPINZANI WAKE FRANCIS MIYEYUSHO HAPA NI BAADA YA KUSAINI KUPAMBANA TAREHE 30 OCT DIAMOND JUBILEE.KATIKATI NI DIRECTOR WA DARWORLD LINKS LTD AMBAO NI WAANDAAJI WA PAMBANO HILO MODDY BAWAZIR

Timu ya wabunge ya POOL yakikabidhiwa zawadi Dodoma


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akimkadbidhi Mshindi wa jumla wa mashindano ya mchezo wa POOL George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe (Kulia) zawadi ya ngao aliyopewa na Chama Cha mchezo huo (TAPA) mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano ya timu ya bunge na combine ya TBL na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi ilifanyika leo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Viongozi wa Serikali, wachezaji wa timu ya Pool ya Bunge na viongozi wa Chama Cha POOL Tanzania (TAPA) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kukabidhiwa kwa zawadi za washindi wa mashinndano hayo yaliyoandaliwa na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akimkadbidhi Mshindi wa pili wa mashindano ya mchezo wa POOL Dkt. Charles Tibeza Mbunge waBuchosa (Kulia) zawadi ya fimbo ya kuchezea aliyopewa na Chama Cha mchezo huo (TAPA) mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano ya timu ya bunge na combine ya TBL na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi ilifanyika leo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Thursday, July 21, 2011

DVD MPYA ZA NGUMI ZATOKA

  1.  DVD MPYA ZA MANNY PAQUAO NA FLOYD MAYWETHER ZIPO MTAANI ZINAPOATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI PIGA SIMU  0652755838 AU WASILIANA NA KOCHA SUPER D KWA 0787,0774-406938 AU FIKA KAMBI YA ILALA AU TIMU YA ASHANTI
d

Saturday, July 16, 2011

ILALA WAPATA SAPOTI YA MAJI KWA AJILI YA MAPAMBANO YA JUMAPILI JULAI 17




MCHAKATO wa Kuendeleza mchezo wa ngumi za Ridhaa Katika Mkoa wa
Kimichezo wa ILALA, unatarajiwa kuingia katika hatua nyingine Julai 17 kati ya klabu za ngumi ya Amana, Matimbwa,Ashanti,Bigrayt na klabu nyingine

Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa
Panandi Panandi uliopo bungoni Wilaya ya ILala ambapo mabondia wanne
kutoka katika kila klabu, watachapana makonde.

Mabondia wa Amana watakaopanda siku hiyo ni IBrahimu Class Kg.64,
Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48.
Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na MOhamedi Matimbwa Kg 64, MOhamedi
Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na MOhamedi Kumbilambali Kg 48 na Klabu ya Ashanti ni Uwesu Manyota,Ramadhani Kimangale,Mark Edson

Akizungumza Dar es Salaam leo Mratibu wa mapambano hayo ambae pia ni
kocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, Rajabu
Mhamila Super D, Alisema mpango huo utaendelea mpaka wahakikishe
wamefanikiwa kuibua vibaji na kuviendeleza

Alisema tangu waanze mpango wa kuandaa mapambano mkohani humo
wamefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo mkoani humo na kuwataka
wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili upate kuendelea
ambapo Super D alitoa mfano wa vitu wanavyoviitaji ikiwemo posho za
nauli kwa wachezaji vifaa vya kuwatia moyo na zawadi mbalimbali kwa
mabondia

Super D aliwashukulu wadau waliojitolea katoni 15 za maji kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo yatakayofanyika jumapili ya Julai 17 aliwataja waliosaidia kuwa Mohamed Sadiq 'Muddy Kala' na Mwanamama Halima Kaubanika aliyejitolea maji kwa wachezaji wote watakaocheza kwa siku hiyo

KAMBI YA ILALA YAKABIZIWA MAJI KWA AJILI YA MPAMBANO WA JUMAPILI JULAI 17

Rajabu Mhamila Super D Boxing Coach akiwa pamoja na Amir Mohamedi ' Msauzi' baada ya kukabidhi maji katoni 15 alizokabidhi kwa niaba ya Muddy Kalla Mtoto wa Ilala
Super D Boxing Coach akipokea maji toka kwa Amir Mohamedi ' Msauzi' baada ya kukabidhi maji katoni 15 alizokabidhi kwa niaba ya Muddy Kalla Mtoto wa Ilala


Baadhi ya vijana wanaonolewa na kambi ya Ilala wakiwa mazoezini

WAHARIRI WAPOKEA VYETI VYAO BAADA YA KUMALIZIKA KWA MKUTANO WA JUKWAA LA WAHARIRI ARUSHA


Mzee Salim Said Salim mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar wa tatu kutoka kulia katika picha akiwachekesha meza kuu ya JUKWAA LA WAHARIRI, mara baada ya kumaliza shughuli ya kugawa vyeti katika mkutano wa jukwaa la wahariri unaomalizika leo jijini Arusha, kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Serengeti Breweriers Tedd Mapunda, Nevile Meena Katibu wa jukwaa la wahariri, kushoto ni Theophil Makunga mjumbe wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri mtendaji wa Mwananchi Communication na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na Mhariri wa Tanzania Daima. Leo baada ya kumaliza mkutano huo wahariri hao watakwenda mjini moshi ambapo watatembelea kiwanda kipya cha bia cha Serengeti Breweriers, baadae watakuwa na mchezo wa mpira wa miguu kati yao na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti ,na baadae watakwenda kushuhudia tamasha la Serengeti Fiesta litakalofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi leo jioni.
Theophil Makunga mjumbe wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri mtendaji wa Mwananchi Communication, akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti (SBL)mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa jukwaa la wahariri.
Mhariri wa gazeti la Spotstarehe Masoud Sanane akipokea cheti chake.
Mhariri wa gazeti la michezo la Bingwa Grace Hoka akipokea cheti chake.
Mhariri wa gazeti la mtanzania Dani Mwakiteleko akipokea.
Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi Jabir Idrissa akipokea cheti chake
Deodatus Balile kutoka New Habari akipokea cheti
Mbaku Mnaku kutoka Busness Time akipokea cheti chake.
Ima Mbuguni kutoka Busnes Time akipokea cheti.
Reginand Simon kutoka mwananchi akipokea cheti.
Scolastica Mazula kutoka Times Radio akipokea cheti.
Abdallah Majura kutoka Sports FM akipokea cheti.
George Njogopa mwakilishi wa Dautch velle Sauti ya Ujerumani akipokea cheti.
John Solombi kutoka BBC akipokea cheti.
Flora Wingia kutoka Gauardian akipokea cheti.

JUKWAA LA WAHARIRI WATEMBELEA KIWANDA CHA SERENGETI MOSHI NA KUCHEZA MPIRA WA MIGUU NA WAFANYAKAZI



Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari, mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuwatembeza wahariri wa vyombo vya habari, ili kujionea mitambo mipya ya kiwanda cha kampuni ya bia ya Serengeti SBL, kilichojengwa maeneo ya Bomambuzi mjini Moshi. Wahariri hao wametembelea kiwanda hicho ikiwa ni kukalimisha ratiba ya mambo mbalimbali ambayo walijipangia, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa jukwaa la wahariri uliomalizika leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha. Katika jukumu lingine walilokuwa nalo ilikuwa ni kucheza mchezo mmoja wa mpira wa miguu kati yao na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti, ambapo mchezo huo umechezwa katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi CCP na timu hizo kutoka suluhu ya magoli 0-0, baadae usiku huu wataingia katika tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi.
Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication na mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga kulia na Mkurugezi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda wakitoka nje. mara baada ya kuzitumikia timu zao katika mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu, uliofanyika uwanja wa Ushirika Moshi na timu hizo kutoka sare ya 0-0.
Mmoja wa wachezaji wa timu ya Serengeti akiwatoka mabeki wa timu ya Jukwaa la Wahariri katika mchezo wao, uliofanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi leo jioni.
Mchezaji mwa timu ya Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akiukokota mpira kuelekea goli la wapinzani wao timu ya Jukwaa la Wahariri.
Kikosi cha Serengeti Breweriers kikijifua kabla ya mpambano huo.
Kikosi cha JUkwaa la wahariri kikijifua kushoto anayekiongoza ni Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Theophil Makunga.
Kikosi cha Serengeti Breweriers kikiwa katika picha ya pamoja kikongozwa na mshabuliaji wake Teddy Mapunda wa pili kutoka kulia mstari wa mbele.
Mgeni rasmi katika mpambano huo ambaye pia ni Mhariri mkuu wa Gazeti la Habari Leo Joseph Kulangwa, akisalimiana na mshabuliaji wa timu ya Serengeti Breweriers ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda kabla mchezo huo haujaanza, kulia ni kocha wa timu ya Jukwaa la Wahariri na mhariri wa Spoti Starehe Masoud Sanane.
Hii ni mitambo ya kiwanda kipyacha Serengeti Breweriers.
Hapa wahariri wakitembelea ghala la kuhifadhia masanduku ya bia.
Huu ni mtambo wa kusafisha chupa kama unavyoona wahariri wakitembelea mtambo huo.
Wahariri wakitembelea katika eneo la kiwanda hicho na kujionea mitambo hiyo.

Monday, July 4, 2011

Mafunzo ya ngumi yaendelea kambi ya Ilala

Kocha wa Mchezo wa ngumi Habibu KInyogoli (kushoto) akimwonesha jinsi
ya kupiga tumbo bondia Yohana Robart wakati wa mazoezi ya kambi ya
Ilala yanayoendelea katika ukumbi wa Amana CCM DAr es Salaam Robart
anajiandaa na mpambano na Rashidi Ally utakaofanyika jumamosi ya Julay
9

 

Kocha wa Mchezo wa ngumi Habibu KInyogoli (kushoto) akiwaelekeza
babondia Rashidi Mhamila, YOhana Robart na Omari Bai jinsi ya
kupishana na kumi pamoja na kupiga wakati wa mazoezi ya kambi ya Ilala
yanayofanyika Amana CCM