Tangazo

Pages

Sunday, January 29, 2012

FRANCIS CHEKA AMDUNDA KALAMA NYILAWILA KWA POINTI


Bondia Francis Cheka akinyoshwa mkono juu na refarii Nemesi Kavishe wakati wa mpambano wake na Kalama Nyilawila ambaye mpaka sasa aamini matokeo hayo
Askali wa usalama wakiendeleza ulinzi wakati wa mpambano huoo jana
Bondia Kalama Nyilawila Kushoto akioneshana ufundi na Frenisic Cheka
Fransic Cheka akinyosha mikono juu baada ya kuibuka mshindi
Francis Cheka kushoto na Kalama Nyilawila wakioneshana umwamba wa kutupa masumbwi jana
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza wakati wa mpambano huu
Mawe ngumi makonde Boxing kushoto ni Francis Cheka na Kalama Nyilawila
Bondia Francis Cheka (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Kalama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro mwishoni mwa wiki cheka alishinda kwa pointi.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Madaraka Nyerere kushoto akifatilia mpambano huo jana
Baadhi ya wadau wakubwa wa mchezo wa ngumi wariofunga safari kutoka Dar kwenda Moro kuangalia mpambano kushoto ni kocha wa masumbwi nchini, Habibu Kinyogoli, Issa Malanga,Rashidi Mtulumla na Hssani Matumla
Bondia Ibrahimu Class (kushoto) akipambana na Venasi Mponji wakati wa mpambano wUtangulizi walitoka droooo
Bondia Ibrahimu Class akisikiliza maelezo toka kwa kocha wake habibu kinyogoli
Bondia Ibrahimu Class (kushoto) akipambana na Venasi Mponji wakati wa mpambano wUtangulizi walitoka droooo

Saturday, January 28, 2012

SUPER D BOXING C OACH KUSAMBAZA DVD ZA MAFUNZO LEO KATIKA UWANJA WA JAMHURI WAKATI CHEKA NA KALAMA WAKIPAMBANA


KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO leo JANUAR 28

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila hawajawahi kutwangana mpambano ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Philemon Kyando 'Don King' alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Cheka.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa kg 72

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Alisema kutakuwa na pambano kati ya Maneno Osward [mtambo wa gongo] na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.

Promota huyo alisema lengo la kumuandalia pambano Nyilawila na Cheka ni kuondoa uvumi kuwa mabondia hao wanaogopana lakini pia ni kuurudisha mchezo wa ngumi katika chati

Friday, January 27, 2012

FRANCIS CHEKA KALAMA NYILAWILA WAPIMA UZITO KWA AJIRI YA MPAMBANO WAO KESHO

FRANCIS CHEKA KALAMA NYILAWILA WAPIMA UZITO KWA AJIRI YA MPAMBANO WAO KESHO




Bondia Kalama Nyilawila (kushoto) akitunishiana misuri na Francis Cheka baada ya kupimauzito leo kwa ajiri ya mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro kesho.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Wednesday, January 25, 2012

SUPER D BOXING COACH AWANG'ARISHA MAKOCHA WENZIE NCHINI BAADA YA KUITIMU MAFUNZO YA KIMATAIFA




Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya chezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani Jana huku wakiwa wameng'alishwa na flana zilizotolewa na SUPER D BOXING COACH kama zawadi kwa makocha hao nnchini.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya chezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani Jana.(Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com)

Mkufuzi Mkuu wa Makocha wa ngumi toka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani Joseph Diouf (kulia) akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa , Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa ufungaji wa mafunzi hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani
katikati ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini Makore Mashaga
Mkufuzi Mkuu wa Makocha wa ngumi toka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani Joseph Diouf, akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa , Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa ufungaji wa mafunzi hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani
kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini Makore Mashaga
Makocha wakiwa na Vyeti Vyao

KOZI YA MCHEZO WA NGUMI KIMATAIFA YAMALIZIKA KIBAHA MKOA WA PWANI


Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya chezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani Jana.(Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com)

Mkufuzi Mkuu wa Makocha wa ngumi toka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani Joseph Diouf (kulia) akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa , Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa ufungaji wa mafunzi hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani
katikati ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini Makore Mashaga
Mkufuzi Mkuu wa Makocha wa ngumi toka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani Joseph Diouf, akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa , Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa ufungaji wa mafunzi hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani
kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini Makore Mashaga
Makocha wakiwa na Vyeti Vyao

KITU KIMETUA MBAVUNI...AKA!


Derry Mathews, kushoto, katika pambano lake Mtaliano Emiliano Marsili, kulia kuwania taji la IBO uzito wa Light lililofanyika kwenye ukumbi wa Liverpool Olympia, Liverpool, England, Ijumaa ya Januari 20, mwaka huu. Marsili alishinda.

Saturday, January 21, 2012

KOZI YA YA KIMATAIFA YA KUFUNDISHA MCHEZO WA NGUMI

BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
                                                                           SLP 15558
                                                                                              DAR ES SALAAM
                                                                                     Email;bft.tanzania2009@gmail.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

     KOZI YA YA KIMATAIFA YA KUFUNDISHA MCHEZO WA NGUMI

Kozi ya Makocha wa Ngumi inayoendelea Kibaha, Pwani katika shule ya Filbart Bayi, inaendelea vema chini ya mkufunzi aliyeletwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Josef Diouf kutoka Senegal.

Ikiwa imefika siku ya sita makocha wanaohudhuria  mafunzo hayo ya siku kumi, wamelizika na kiwango cha mkufunzi huyo kwa kusema kuwa mbinu za kiufundi na ujanja wa  ufundishaji wa mchezo wa ngumi anazo wafundisha ni za kisasa na kwamba kwa sasa wameelewa msingi wa ufundishaji,hasa kwa kumwanzisha, kumwendeleza mchezaji hadi kufikia kuwa mchezaji wa kimataifa toufauti na awali ambapo walikuwa wanafundisha kwa mazoea bila kuwa na mbinu za kuwafanya wachezaji ili kuleta upinzani hasa katika mashindano ya kimataifa.
Lakini pia wamejifunza namna ya kuandaa ratiba za ufundishaji za siku kwa siku ,wiki,mwezi na ratiba ya mashindano yanayowakabili
Kwa kujigamba Makocha kutoka mikoani wamesema ujuzi wao wataanza kuonyesha katika mashindano ya Taifa yatakayofanyika katikati ya mwezi wa February ya kuwa  kutakuwa na ushindani mkali sana hasa kwa kuzingatia mikoa mingi makocha wake wamepata mafunzo hayo,na sasa timu za vyombo vya ulinzi na usalama  na zile za Dar es salaam ziwe tayari kupata upinzani wa hali ya juu kwa kuwa sasa hata vilabu vya kutoka mikoani pia  zina mbinu na ujanja wa ufundishaji kulingana na mabadiliko ya mchezo wa Ngumi Duniani.
Kozi hiyo inatazamiwa kumalizika tarehe 24/01/2012 na walimu watakaokuwa wamefaulu watatunukiwa vyeti vya kimataifa vya daraja la kwanza(level 1) na kuingizwa katika Database za Chama cha Ngumi cha Dunia AIBA na kwamba watakuwana haki ya kufundisha mchezo wa Ngumi popote Duniani

Wakati huo BFT kwa masikitiko makubwa inasikitika kupatwa na msiba wa bondia wa timu ya Taifa Godfrey Mbunda aliyefariki kwa kugongwa na gari wakati yeye akiwa anaendesha pikipiki maeneo ya mbezi.ni pigo kubwa katika medani ya mchezo wa ngumi kwa kuwa bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa suala la maendeleo ya mchezo wa ngumi Tanzania

Makore Mashaga
KATIBU MKUU
                         MOB. 0713 588818

KOZI YA MCHEZO WA NGUMI KWA MAKOCHA YAENDELEA KIVITENDO KIBAHA PWANI

Kocha wa Tmu ya JKT, Saidi Omari 'Gogo Poa' (kushoto) wakioneshana ufundi wa kutupa makonde na Kocha wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya
Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' wakati wa mazoezi ya vitendo yanayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani leo kwenye kozi ya kimataifa ya mchezo wa ngumi.(Picha na
http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)


kocha wa Mkoa wa Pwani, Gaudence Uyaga wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa makocha hawo ambao wapo katika kozi ya kimataifa ya mchezo wa
masumbwi Duniani.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)






kocha wa Mkoa wa Pwani, Gaudence Uyaga wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa makocha hawo ambao wapo katika kozi ya kimataifa ya mchezo wa
masumbwi Duniani.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)






Kocha wa Tmu ya JKT, Saidi Omari 'Gogo Poa' (kushoto) wakioneshana ufundi wa kutupa makonde na Kocha wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu yaMkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' wakati wa mazoezi ya vitendo yanayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani leo kwenye kozi ya kimataifa ya
mchezo wa ngumi.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)




Mkufazi wa kimataifa wa makocha kutoka chama cha ngumi za ridhaa Duniani (AIBA) Josephe Diof (kushoto) akimpatia maelekezoKocha mchezo wa ngumi wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' wakati wa mazoezi kwa vitendo
katika kozi ya kimataifa ya mchezo wa ngumi duniani(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)




SUPER D BOXING COACH AKIWA MAPUMZIKO





MAPUMZIKO





MAPUMZIKO YA MDA



Baadhi ya makocha wakiwa na mkufuzi wao wa kimataifa Joseph Diof katikati kushoto na Lema ,Super D boxing Coach na Mohamedi wa timu ya polisi


Super D Boxing coach akiwa na Josephe Diof wakati wa Kozi ya Kimataifa ya Mchezo wa Ngumi





Super D bOXING cOACH NA jOSEPHE dIOF



lEMA kUSHOTO NA MOHAMED




kATIBU WA TOC AKIWA NA BAADHI YA MAKOCHA





MAKOCHA WA MIKOA MBALIMBALI YA TANZANIA BARA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA




MAKOWA MASUMBWI WAKIWA KATIKA KOZI YA KIMATAIFA

Wednesday, January 18, 2012

KOZI YA KIMATAIFA YA UKOCHA WA MASUMBWI INAENDELEA KIVITENDO HUKO KIBAHA MKOANI PWANI


 


Baadhi ya Makocha wa Mchezo wa Ngumi nchini wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa kozi ya kimataifa ya mchezo huo kwa makocha inayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani.Picha na Rajab Mhamila

Sunday, January 15, 2012

mkufunzi wa kimataifa ,Josef Diouf kutoka Shirikisho la masumbwi Dunia (AIBA) atua nchini


Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga majinamatano kati ya 5 ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi yakimataifa ya mchezo huo iliyopangwa kufannyika kesho Januari 16 mwaka huu.BFT imewakata washiriki hao baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki kutokana na hasarailiyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya awali iliyokuwaifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana.TOC ambayo huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzukuinayotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshekozi hiyo tangu mwaka jana lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wakozi hiyo kutoka nchini Algeria kuingia mitini, Kozi hiyo ya Kimataifa ya Mchezo wa masumbwi kwa mara ya mwisho ilifanyika nchini mwa 2002 ambapo ni ngazi ya juu kabisa ya ukocha Duniani kote
TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka nje yaDar es Salaa kutoka katika fungu la pesa za kuendeshea kozi hiyohivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale waliofanyautovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa kilichobakikutosheleza mahitaji wa kozi itakayoendeshwa Januari 16 mwaka huu.Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisemaidadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana nabajeti waliobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matanoya washiriki walioachwa .Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni mpiga picha waMagazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la Maishaambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord Ngumbi,Moses Lema, Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es Salaam).Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria Mwaseba(Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee (JKTMbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso (MagerezaKigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari (Tanga).Wengine ni Mohamed Hashim (Polisi Dar es Salaam), David Yombayombam,Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ), Mazimbo Ally, Rogated Damian naFatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban (Magereza Dar esSalaam).Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf kutokaShirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana namakamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe.Kozi hiyo itafanyika latika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi KibahaMkoani Pwani na itafikia tamati Januari 24 mwaka huu.