Tangazo

Pages

Thursday, March 21, 2019

NGUMI KUPIGWA MAGOMENI MAPIPA 20/04/2019 UKUMBI WA CCM MWINYIMKUU

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Idd Mkwera na Rojas Masamu wamesaini kuzipiga April 20 kaika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu uliopo magomeni Mapipa akizungumzia mpambano uho Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku hiyo kwa kupewa nguvu na 

Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia  bondia huyo ndie aliesababisha mabondia hawo wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio mana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia Hussein Pendeza atamkabili Juma Ramadhani 'Choki' na Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Azizi Iddi Hussein Shemdoe na Jitu Rajabu

Mapambano yote hayo yanaletwa kwenu na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa

na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana mbalimbali kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini

NGUMI KUPIGWA CCM MWINYIMKUU APRIL 20 MAGOMENI MAPIPA
Friday, March 1, 2019

SUNDAY KIWALE 'MORO BEST' NA IBRAHIMU MAKUBI KUPIGANA MOROGORO MARCH 2 MSAMVU TERMINAL

Bondia machachali nchini Tanzania Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto kutoka Dar es Salaam Tanzania akitunishiana misuli  na mpinzani wake Said Chalachim kutoka Ifakala mabondia hawo watazipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal Pub ulipo msamvu Morogoro

Promota wa masumbwi nchini Kaike Siraju akiwainua mikono juu bondia Ibrahimu Makubi na Chales Chilala baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuzipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal pub ulipo msamvu morogoro    
Na
Mwandishi Wetu

MABONDIA kutokwa kwa Super D Coach Uhuru GYM Sunday Kiwale  'Moro Best' na Ibrahimu Makubi wapo mkoani morogoro kwa ajili ya mpambano yanayo wakabili ambapo Sunday Kiwale 'Moro Best' atamkabili Said Chalachim kutoka Ifakara wakati Ibrahimu Makumbi atazipiga na Charles Chilala nae kutoka Ifakara

akizungumza baada ya kupima uzito kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wake wapo vitani hivyo awatofanya ajizi wala kuwa na msalia Mtume kwani kazi waliyotumwa na mashasbiki zao kutoka Dar es Salaam si yakitoto na awatotaka kuwangusha kwa kuwa wao ni watu wa kazi kazi

nae bondia kiwale anaetamba katika uzito wake amesema kuwa mabondia wengi nchini wanamuogopa ndio mana amekuja kucheza Mkoani ili kuendeleza kipaji chake kisije kikapotea bule kwa sababvu ya kuogopewa na mabondia wa Dar es salaam katika uzito wake kwani kazi yangu wanaijua na kuitambuwa niwapo ulingoni

na bondia Makubi alisema kuwa yeye ni bondia mchanga sana katika ngumi za kulipwa ila ni motto mkali katika masumbwi hivyo nawaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kwa wingu kushudia kazi atakayo ifanya

Mabondia hawo wote watakuwa wakisindikiza mpambano wa ubingwa kati ya Twaha Kiduku wa Morogoro na Mada Maugo watakaozipiga raundi kumi kugombea ubingwa wa Taifa nchini

Promota wa mpambano uho kaike Siraju alieleza kwa kusema kuwa ameandaa mapambano mengi sana nchini ususani Morogoro sasa baada ya kumuibua Fransic Cheka sasa ameibuwa mabondia wengine mbalimbali kutoka moro pamoja na vitongoji vyake hivyo kazi kwao mashabiki kutoa sapoti

aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mitanange mingine ya kukata na shoka ambapo bondia Epson John atazipiga na Adamu Ngange na Cosmasi Cheka atakabiliana na Amani Bariki na kingilio katika mapambano yote hayo ni tsh 7000 na V.I.P 15000  na nyote mnakaribishwa

MADA MAUGO KUZIPIGA NA TWAHA KIDUKU MSAMVU MOROGORO MARCH 2

Bondia Twaha Kiduku kushoto akiwa ameshika mkanda wa Taifa watakaogombania yeye na Mada Maugo March 2 Morogoro katika ukumbi wa Terminal Pub uliopo Morogoro Msamvu Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Amani Bariki 'Manny Chuga' kushoto akinyooshwa mkono juu na mpinzani wake Cosmas Cheka na promota wa masumbwi nchini Siraju Kaike baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika march 2 katika ukumbi wa terminal pub uliopo msamvu Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia machachali nchini Tanzania Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto kutoka Dar es Salaam Tanzania akinyooshwa mkono juu na mpinzani wake Said Chalachim kutoka Ifakala mabondia hawo watazipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal Pub ulipo msamvu Morogoro katikati ni promota wa mpambano huo Kaike Siraju

Bondia machachali nchini Tanzania Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto kutoka Dar es Salaam Tanzania akitunishiana misuli  na mpinzani wake Said Chalachim kutoka Ifakala mabondia hawo watazipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal Pub ulipo msamvu Morogoro

Bondia Twaha Kiduku kushoto akiwa ameshika mkanda wa Taifa watakaogombania yeye na Mada Maugo March 2 Morogoro katika ukumbi wa Terminal Pub uliopo Morogoro Msamvu Picha na SUPER D BOXING NEWSPromota wa masumbwi nchini Kaike Siraju akiwainua mikono juu bondia Ibrahimu Makubi na Chales Chilala baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuzipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal pub ulipo msamvu morogoro
BONDIA SUNDAY KIWALE 'MORO BEST' AKIPIMA UZITO
BONDIA IBRAHIMU NMAKUBI AKIPIMA UZITO

Sunday, December 30, 2018

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA DESEMBA 31 KINESI


Bondia Mussa Msabaha kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Makubi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kufunga mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika viwanja vya Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki Picha na Super D Boxing News
Bondia AZizi Uliza akingia na Farasi kwa ajili ya kupima uzito kupambana na Ramadhani Shauri desema 31 katika mpambano wa kufunga mwaka 

Bondia Azizi Uliza akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kufunga mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa kinesi uliopo Shekilango akizipiga na Ramadhani Shauri mpambano wa Raundi kumi Picha na Super D Boxing News


MABONDIA WA KIKE WAKITUNISHIANA MISULI


Na Mwandishi Wetu

Mabondia Azizi Uliza na Ramasdhani Shauri wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Desema 31 mpambano wa kufunga mwaka na kufungua mwaka

alikuwa wa kwanza kabisa kuingia katika viwanja vya las vegasi Mabibo kwa ajili ya kupima uzito ni Azizi Uliza aklieingia uwanjani kwa shangwe na ndelomo uku akisindikizwa na wapambe wake pamoja na vigoma vilivyoleta radha misri ya kuwa mpambano upo siku hiyo ya kupima kumbe ilikuwa siku ya kupima uzitio na Afya kwa mabondia wote watakaocheza

baara ya saa moja bondia Ramadhani Shauri nae akaingia na shangwe na ndelemo vifijo zaidi ya mwenzake ata hivyo nani zaidi ya mwenzie itajulikana katika uwanja wa kines Shekilango ambapo mtanange uho utapigwa kwa raundi 10

akizungumzia mpambano uho Promota  Josepher Nyilawila kutoka kampuni ya Ijuka Sports amesema kuwa ulizi utakuwa ni wa kutosha kupita mahelezo ambapo mtu anaweza kuja na baiskeri yake na kuikuta salama baada ya mpambano

amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali 

 Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni
alisema mapambano yote hayo yatakuwa kwa kingilio cha tsh 6000 na kwa V.I.P 10000 utaweza kuangalia mapambano yote hayo yani kama vile bule


Wednesday, December 19, 2018

BONDIA AZIZI ULIZA AJIFUA KUMKABILI RAMADHANI SHAURI DESEMBA 31 KINESI SHEKILANGO

Bondia Azizi Uliza 'Kulia' akioneshana umwamba wa kutupiana Makonde na Mohamedi Selemani wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Ramadhani Shauri mpambano utakaofanyika Desema 31 katika uwanja wa Kinesi Shekilango Picha na Super D Boxing News'
Bondia Azizi Uliza akifanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo kwa ajili ya kujiandaa na mpmbano wake na Ramadhani Shauri utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango Picha na Super D Boxing News'

Bondia Azizi Uliza akijifua kwa kupiga spidboll wakati wa mazoezo yake ya kujiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauri utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango Picha na Super D Boxing News'

Bondia Azizi Uliza 'Kulia' akioneshana umwamba wa kutupiana Makonde na Mohamedi Selemani wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Ramadhani Shauri mpambano utakaofanyika Desema 31 katika uwanja wa Kinesi Shekilango Picha na Super D Boxing News'


Na Mwandishi Wetu


BONDIA AZIZI ULIZA amendelea kujifua kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauri utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango nyuma ya urafiki

akizungumza na mwandishi wa habari hizi uliza amesema kuwa Shauri asumbui ata siku moja kwani yeye ni mkongwa na mimi ndio nachpkia hivyo sio kazi rahisi kushindana na mimi ingawa anatamba katika vyombo vya habari ikiwa kapigwa K,O mbaya na Idd Mkwera raundi ya 9 kwangu mimi asitegemee kuwa upenyo nitamwadabisha vya kutosha kwani nimejiandaa kwa ajili ya kupigana

hivyo nawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi mje muone Uliza namfanya nini Shauri nitampiga kipigo ambacho akijawai kumtokea tangu aanze ngumi

alimaliza kwa kusema Azizi Uliza

nae Promota wa mpambano uho Josepher Nyilawila kutoka kampuni ya Ijuka Sports  amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali 

 Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingineMonday, December 17, 2018

MABONDIA WAJIANDAA KUZIPIGA DESEMBA 31 KINESI SHEKILANGO

Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' kushoto akimsimamia bondia Ramadhani Shauri kupiga beg wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki Picha na Super D Boxing News'
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Ramadhani Shauri amendelea kujifua kwa ajili ya mpambano wake wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa kinesi shekilango maeneo ya urafiki Dar es salaam akimkabili Azizi Uliza katika mpambano wake wa raundi kumi

akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika kambi yake iliyopo mabibo mwembeni amesema kuwa yupo fiti kwa asilimia mia hivyo sasa anasubili mpambano tu yana natamani iwe ata leo tupate kumalizana mana nitampa kipigo ambacho si chakawaida alisema Shauri

aliongeza kwa kusema mashabiki wake wajitokeze kwa wingi waje kumwangalia kwani sasa anapigana ngumi za moto hatari kwani mpinzani wake atofika raundi ya sita hivyo nawaomba mashabiki wawai kuingia uwanjani mapema kabla mpambano aujaisha


nae Promota wa mpambano uho Josepher Nyilawila kutoka kampuni ya Ijuka Sports  amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali 

 Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni


siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine