Tangazo

Pages

Sunday, November 30, 2014

DVD MPYA YA MANNY PACQUAIO VS CRIS ALGIERI SASA INAPATIKANA


DVD MPYA YA MASUMBWI AMBAYO WAMEPIGANA MACAU CHINA AMBAPO BONDIA MTANZANIA FADHILI MAJIHA ALICHEZA UTANGULIZI SASA ZINAPATIKANA UHURU NA MSIMBAZI ZAIDI PIGA SIMU 0754406938 / 0787406938

BABU WA MIAKA 63 AMPIGA KO RAUNDI YA PILI 'DOGO' WA MIAKA 33


KAMA ingekuwa sinema ya Hollywood, ingekuwa bomba sana.
Lakini Mickey Rourke hakuwa anaigiza jana wakati alipopanda ulingoni baada ya miaka 20 ya kuachana na ndiondi na kumpa mtu kichapo.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 62 alizipiga na Elliot Seymour, mwenye umri wa miaka 33, katika pambano la raundi tano Moscow, Urusi. Rourke alihitaji randi mbili tu kumsimamisha mpinzani wake ambaye alianguka chini baada ya kupewa 'mkono mkali' wa mtu mzima huyo.
Baada ya mapambano 30 katika ngumi za Ridhaa, miaka ya 1960 hadi 70, ambayo alipoteza matatu tu, Rourke alihamia kwenye kucheza filamu Hollywood, kabla ya kurejea kwenye mchezo kama bondia wa kulipwa miaka ya 90, ambayo ilimsababisha athari usoni mwake na kulazimika kufanyiwa upasuaji uliobadilisha mwonekano wa sura yake. Alishinda pambano moja tu kati ya tisa ya kulipwa.
Hollywood star Mickey Rourke made a victorious return to the ring as he beat Elliot Seymour in two rounds
Nyota wa Hollywood, Mickey Rourke akiinuliwa mkono kutangazwa mshindi baada ya kumkalisha Elliot Seymour raundi ya pili

TYSON AMSHINDA CHISORA, SASA KUMVAA KLITSCHKO


Fury lands an uppercut on his way to a decisive victory over Chisora to set himself up for a shot at Wladimir Klitschko next year
Bondia Tyson Fury (kulia) akimchapa konde la uppercut mpinzani wake Dereck Chisora katika pambano la uzito wa juu usiku wa jana ukumbi wa ExCel, Docklands mjini London. Fury alishinda kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya 10 na sasa anaweza kupambana na bingwa wa dunia, Wladimir Klitschko mwakani.

TOTO LA CHRIS EUBANK LACHAPWA NA MZUNGU


Saunders (right) uses his quick feet to escape from Eubank Junior's left hook in front of a capacity crowd at the ExCeL centre
Bondia Billy Joe Saunders (kulia) akipambana na Chris Eubank Junior kushoto usiku wa jana ukumbi wa ExCeL mjini London, katika pambano la uzito wa Middler. Saunders alishinda kwa pointi na kutetea mataji yake ya Uingereza, Jumuiya ya Madola na Ulaya- na sasa amepewa nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia wa WBO mwakani.
Chris Eubank (centre) congratulates Saunders on his victory against his son by shaking his hand after the final bell
Chris Eubank (katikati) akimpongeza Saunders kwa ushindi dhidi ya mwanawe jana

Saturday, November 22, 2014

BONDIA MTANZANIA FADHILI MAJIHA ALIVYOKUTANA NA WATU MAARUFU MACAU CHINA

 
KUTOKA KULIA: Emmanuel Mlundwa ; Fadhili Majiha NA MTANGAZAJI MAARUFU WA MASUMBWI DUNIANI Michael Buffuer AMBAYE HUSEMA :" AND MILLIONS OF VIEWERS AROUND THE WORLD, GET READY TO RUMBLE "

 
FROM LEFT: Emmanuel Mlundwa; Fadhili Majiha AND Freddie Roach Official THE TRAINER OF Manny Pacquiao . 22/11/2014 AT THE CAPRI ARENA, MACAU
Fadhili Majiha [LEFT] WITH Roy Jones Jr AT THE CAPRI ARENA, MACAU 22/11/2014

BONDIA MANNY PACQUAIO AMPIGA KWA POINT CHRIS ALGIERI MACAU CHINA



Friday, November 21, 2014

BONDIA ZUMBA KUKWE KUZIPIGA NA SWEET KALULU



Bondia wa ngumi za kulipwa nchini mwenye machachali mengi na ngumi nzito awapo ulingoni  Zumba Kukwe “chenji dola” anatarajia kupanda ulingoni alhamis ya tarehe 27/11/2014 kuzipiga na bondia mkongwe Sweet kalulu katika ukumbi wa kontena uliopo kibaha maili moja, Watacheza pambano la raundi nane, lisilo la ubingwa ila mshindi kati ya sweet kalulu na zumba kukwe atacheza na mshindi kati ya Thomas Mashali na dula mbabe katika pambano la ubingwa, mashali na dula wao wanacheza decemba.
Akilizunguzia pambano hilo kwa wanahabari kiongozi wa ngumi za kulipwa na mratibu wa pambano hilo alisema “pambano la Zumba kukwe na sweet kalulu maandalizi yanakwenda vema  chini ya udhamini wa George Nyasulu aliependekeza mchezo upigwe kibaha maili moja alipotokea zumba kukwe na kutanua wigo wa masumbwi nchini ,ngumi ziwe zinachezwa kila kona ya nchi sio kila siku mabondia kucheza mjini dar e salaam tu, watu  wa mkoa wa pwani nao wapate nafasi  ya   kuwaona vijana wao wanaotikisa mjini kwani kibaha kuna mabondia wengi wazuri na wakali ambao hawajawahi cheza kwao , hivyo katika mapambano ya utangulizi kutakuwepo na mabondia wote wakali wa mkoa wa pwani wakicheza na wenzao toka sehemu mbalimbali za jiji kama vile Mustafa doto atazipiga na ramadhan max, huku shadrack ignas akioneshana kazi na  fredy masinde,nae dogo janja Issa omar nampepeche atazipiga na Rajabu miafro na mapambano mengine mengi ya utangulizi .kiingilio kimepangwa kuwekwa kidogo ili watu wengi wapate kuja shuhudia pambano hilo la aina yake  ambalo si la kukosa

BONDIA MTANZANIA FADHILI MAJIHA KUMSINDIKIZA MANNY PAQUAIO NOVEMBA 22 MACAO CHINA

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Fadhili majiha kwa mara ya kwanza ataiwakilisha nchi ya tanzania akicheza katika mpambano wa utangulizi wa bondia mkubwa duniani Manny Paquaio na Chris Algieri mpam
bano utakaofanyika 


Cotai Arena, Venetian Resort, Macao, Macao S.A.R., China mpambano ambao bonia mtanzania Fadhili Majiha atavaana na Jerwin Ancajas kutoka Philippines mpambano utakaokuwa wa raundi 8 

mch
ezo uliopowa hadhi ya nyota mbili ambapo watanzania wote wanapaswa kumuombea duwa bondia nambari moja kwa ubora nchini tanzani kwa ajili ya kutuwakilisha katika mpambano uho mkubwa wa kimataifa ambapo zaidi ya watu wengi duniani watakuwa wakiangalia mojakwa moja kupitia luninga zao

Majiha ambaye hivi karibuni ametokea nchini Bangkok, Thailand alipocheza mpambano wake wa mwisho wa raundi 12 na kupoteza kwa pointi amewakikishia wa

tanzania kuwa bado yupo fiti na atafanya maajabu siku hiyo kwa kumtwanga MPhilippines huyo ambaye atakutana nae siku  hiyo
 

Monday, November 17, 2014

Laila Ali 'She Bee Stingin'' BONDIA PEKEE WA KIKE ALIYECHUKUA KIWANGO CHA JUU CHA FEDHA KATIKA WANAMASUMBWI


Laila Ali Curtis Conway Curtis Jr.
Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao
Kwa sasa unakadiriwa pia utajiri wake unafikia kiasi cha dola za kimarekani milioni kumi ambazo ni zaidi ya fedha za kitanzania bilioni 16, ambazo ambazo amezitengeneza kutoka katika mchezo wa masumbwi duniani,

Matangazo ya bihashara, pamoja na kazi ya uwanamitindo 
Kutokana na umaarufu wake katika masumbwi , alijikuta akipata mikataba mbalimbali mikubwa ya matangazo ya biashara  katika makampuni na maduka makubwa Duniani, kama maduka ya kuuza vyakula,nguo na vifaa vya michezo hali iliyompatia nafasi ya kujiongezea kipato chake kwa haraka  leila alianza kujihusisha na masumbwi akiwa na umri wa miaka 15, huku msaada wake mkubwa ukitokea kwa baba yake mzazi ambapo baada ya kuonesha uwezo wake kwa mda mfupi arianza kuingia kwenye mapambano ya kimataifa 



Baada ya kupata ubingwa huo mwaka 2005 aliweza kutoa ubingwa mwingine unaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la ngumi za wanawake ' IWBF kwa kumtwanga Nikki Eplion kwa K,O ya raundi ya nne katika uzito wa female super middleweight title 

Pamoja na uwezo huo, Wapo baadhi ya mabondia wa kike kama Vonda Ward, Leatitia, Robinson na Ann Wolfe wamekuwa wakilalamika kuwa Leila anawakwepa kwa kupangiwa vibonde na kuhofia kupigwa.

Licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa masumbwi, mitindo na matangazo ya biashara kwenye runinga lakini mara kadhaa amekua akialikwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kwa ajili ya vipindi hali inayomfanya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha 

Baadhi ya vipindi hivyo maarufu ni pamoja na agaeorgr Lpez, Dancing with the Stars, American Gladiators,Celebrity Family. The Early Show

Katika historia ya  maisha yake ya ndoa ,leila amesha olewa mara mbili ambapo kwa mara ya kwanza aliolewa na Johnny Mcclain Agost 27,2000,ambaye walikutana kwenye sharehe ya kuzaliwa baba yake mzazi Mohamed Ali wakati anatimiza umri wa miaka 57.

Kabla ya kuoanaMacClain ndiye aliyekuwa promota wake katika michezo ya ngumi za kulipwa jambo ambalo lilimsaidia kufanya vizuri katika mapambano yake yote ambayo ajapigwa wala kutoa droo ata mpambano mmoja akiwa na alama won 24 (KO 21) + lost 0 (KO 0) + drawn 0 = 24  

Baada ya kuoana mwaka 2000 walikuja kuhachana mwaka 2005. mwaka 2007, leila alifunga ndoa na Curtis Conway , ikiwa ni ndoa yake ya pili . wadadisi wa mambo ya kimapenzi wanaeleza kuwa kilichomfanya kuolewa tena ni kutokana na kuwa na mvuto wa kimapenzi alionao mwana dada huyo maili awapo ulingoni,

Leila amefanikiwa kupata watoto watatu akiwa na McClain ambao ni Leilani,Cameron na Kelton. Baada ya kuolewa tena alipata watoto wawili ambao ni Curtis Muhame Conway Aliyezaliwa mwaka 2008 na Sydney  mwaka 2011

Kwa sasa leila amestafu kucheza mchezo wa masumbwi tangu acheze mchezo wake wa mwisho Tareha 3 -2-2007  na Gwendolyn O'Neil na kufanikiwa kumpiga kwa K,O raundi ya kwanza na kutangazwa kuwa bingwa wa mikata miwili ya WBC female super middleweight title
WIBA Women's International Boxing Association super middleweight title
Ingawa kazi kubwa anayofanya kwa sasa ni kutangaza vipindi mbalimbali kwenye television pamoja na mitindo 
Moja ya mambo ambayo yalishangaza ulimwengu katika fani ya mitindo mwaka 2012 akiwa na mimba ya miezi 9, aliweza kushiriki kikamilifu katika maonesho ya mavadhi aliweza kuonesha umahiri wake kwenye jukwaa kwa kupita akiwa kwenye tamasha la mavazi lililofanyika jijini London Nchini Uingereza Novemba 20, 2012

Amestaafu akiwa na rekodi ya kutopigwa ata mchezo mmoja ambapo alicheza michezo  24 alishinda kwa  KO 21 ambapo mabondia watatu pekee ndio aliwashinda kwa point 
huyo ndio leila Muhamed Ali
kwa mahitaji ya DVD ZAKE KWA AJILI YA KUONA MAPAMBANO YAKE MBALIMBALI LIVE TUWASILIANE KUPITIA


Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao

Thursday, November 13, 2014

BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUAR MOSI FRENDS CORNER

Bondia Thomasi Mashali kushoto akitia saini ya kupigana na Abbdallah Pazi kulia baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Abbdallah Pazi kulia akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG

Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG
Promota Kassim Texas katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Picha na SUPER D BLOG



Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG

Monday, November 10, 2014

MABONDIA IBRAHIMU TAMBA NA JULIUS KISARAWE WANYAKUWA MIKANDA YA TPBO


Bondia Mrisho Adam  kushoto akipambana na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Adam alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Mrisho Adam  kulia akipambana na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Adam alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Karim Ramadhani Kushoto akipambana na Stevin Kobelo wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mchazo huo ulimalizika kwa droo picha na   SUPER D BLOG
Bondia Hassani Kiwale kushoto akipambana na Julius Kisarawe wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa wa chama cha TPBO Kisarawe aluishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG


Bondia Maisha Samson kushoto akipambana na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wili iliyopita Tamba alishinda kwa K,O ya raundi ya Pili na kunyakuwa ubingwa  Picha na SUPER D BLOG
Refarii Sako Mtlya akimnyoosha mkono juu bondia Ibrahimu Tamba baada ya kumgalagaza Maisha Samsoni kwa K,O ya raundi ya pili katika mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BLOG

Friday, November 7, 2014

MABONDIA SAMSON MAISHA NA IBRAHIMU TAMBA WATAMBIANA KUZIDUNDA JUMAPILI NOVEMBA 9 MANYARA PARK MANZESE

Bondia Maisha Samson kushoto wakitunishiana misuli na Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Bondia Maisha Samson kushoto wakitunisha misuli na Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Samson Maisha
Ibrahimu Tamba
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar kushoto  na Samson Maisha wa Kyela Mbeya wakinyoshwa mikono juu na mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM  Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar na Samson Maisha wa Kyela Mbeya wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM katikati ni mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame Picha na SUPER D BLOG


NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Samsoni Maisha wa kyela Mbeya amewasili jijini Dar es salaam na kutamba kunyakuwa ubingwa wa TPBO kwa kumpiga Ibrahimu Tamba  wakati wa mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam

mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa  unaotambuliwa na TPBO utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na

Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

































mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd









Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Thursday, November 6, 2014

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Samsoni Maisha wa kyela amewasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa TPBO na Ibrahimu Tamba mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam

mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na


Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Tuesday, November 4, 2014

BONDIA IDDI PIALALI AIBEBA KIWANGWA BAGAMOYO KWA KUNYAKUWA UBINGWA WA KANDA YA MASHARIKI



Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Piyalali akiwa na mkanda wa ubingwa wa Kanda ya Mashariki Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Pialali

Bondia Iddi Pialali
Bondia Hashimu Zuber kushoto akipambana na Ally Mahiyo wakati wa mpambano wao uliofanyika kiwangwa bagamoyo mkowa wa pwani Zuber alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia mchezo huo uliopigwa siku ya jumatatu kiwangwa bagamoyo mkoa wa pwani 
Bondia Ally Bugingo kushoto akimtupia konde Twalibu Tuwa wakati wa mpambano wao Bugingo alishinda kwa point
Picha na SUPER D BLOG






Said Yazidu akiongea na mashabiki wakati wa mpambano huo

BAADHI YA WATU AMBAO WALIKOSA KUINGIA UKUMBINI KWA KUTOKUWA NA PESA WAKIPIGA CHAPO KWENYE DIRISHA

Na Mwandishi  Wetu

BONDIA Iddi Pialali mwanzoni mwa wiki hii aliwainuwa mikono juu wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani baada ya kunyakuwa ubingwa wa kanda ya mashariki kwa kumtwanga kwa K,O  ya raundi ya tano bondia Fadhili Mkundi

mpambano huo uliofanyika siku ya jumatatu ulikuwa na shamlashamla nyingi tangia mwanzoni mwa mchezo huo ambapo watu walifulika kuona ndonga zikipigwa Kiwangwa
mpambano huo wa ubingwa ulianza mnamo saa 4 na dakika 20 usiku

uku mashabiki wakimshangilia Pialali kwa furaha mwanzo mwisho raundi ya kwanza ilianza kwa mashambulizi ya kutupiana makonde ya uku na kule ambayo yaliwavutia sana wakazi wa kiwangwa ilipofika raundi ya tatu mashambulizi yakawa kwa upande mmoja ambapo Pialali alibadilisha mchezo kwa kupiga ngumi za tumbo yani juu na chini kufika raundi ya tano Pialali aliongeza mashambulizi hayo kwa kasi na kumfanya refarii wa mpambano huo Pembe Ndava  kumuhesabia mpinzani ambaye alikuwa akivuja damu puani na mdomoni ambapo mpinzani huyo alisalimu amri na Pialali kuibuka kidede kwa kushinda K,O raundi ya tano

kabla ya mpambano huo kulikuwa na mapambano ya utangulizi yaliyowakutanisha mabondia Hashimu Zuber aliyempiga kwa pointi Ally Maiyo na Ally Bugingo alimsambalatisha kwa pointi Twalibu Tuwa


mwisho wa mchezo huo promota wa mpambano huo Bernard Mwakyusa amewahaidi wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo kuwa atapeleka burudani ya masumbwi mara kwa mara kwa kuwa sasa kuna bingwa anayetambulika rasmi katika tasnia ya masumbwi nchini