Tangazo

Pages

Friday, November 21, 2014

BONDIA ZUMBA KUKWE KUZIPIGA NA SWEET KALULU



Bondia wa ngumi za kulipwa nchini mwenye machachali mengi na ngumi nzito awapo ulingoni  Zumba Kukwe “chenji dola” anatarajia kupanda ulingoni alhamis ya tarehe 27/11/2014 kuzipiga na bondia mkongwe Sweet kalulu katika ukumbi wa kontena uliopo kibaha maili moja, Watacheza pambano la raundi nane, lisilo la ubingwa ila mshindi kati ya sweet kalulu na zumba kukwe atacheza na mshindi kati ya Thomas Mashali na dula mbabe katika pambano la ubingwa, mashali na dula wao wanacheza decemba.
Akilizunguzia pambano hilo kwa wanahabari kiongozi wa ngumi za kulipwa na mratibu wa pambano hilo alisema “pambano la Zumba kukwe na sweet kalulu maandalizi yanakwenda vema  chini ya udhamini wa George Nyasulu aliependekeza mchezo upigwe kibaha maili moja alipotokea zumba kukwe na kutanua wigo wa masumbwi nchini ,ngumi ziwe zinachezwa kila kona ya nchi sio kila siku mabondia kucheza mjini dar e salaam tu, watu  wa mkoa wa pwani nao wapate nafasi  ya   kuwaona vijana wao wanaotikisa mjini kwani kibaha kuna mabondia wengi wazuri na wakali ambao hawajawahi cheza kwao , hivyo katika mapambano ya utangulizi kutakuwepo na mabondia wote wakali wa mkoa wa pwani wakicheza na wenzao toka sehemu mbalimbali za jiji kama vile Mustafa doto atazipiga na ramadhan max, huku shadrack ignas akioneshana kazi na  fredy masinde,nae dogo janja Issa omar nampepeche atazipiga na Rajabu miafro na mapambano mengine mengi ya utangulizi .kiingilio kimepangwa kuwekwa kidogo ili watu wengi wapate kuja shuhudia pambano hilo la aina yake  ambalo si la kukosa

No comments:

Post a Comment