Tangazo

Pages

Thursday, January 31, 2013

TIMU YA ASHANTI BOXING YAANZA VEMA KLAB BINGWA YA MASUIMBWI

Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili Picha na www.Superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili Picha na www.Superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia wa Klabu Ya Ashanti ya Ilala Abdallah Shamte akipambana na Hamisi Matunda wa Mashine ya maji wakati wa mashindano ya klabu bingwaShamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili Picha na www.Superdboxingcoach.blogspot.com

Mashabiki wa ASHANTI BOXING YA ILALA WAKISHANGILIA

Wednesday, January 30, 2013

Idd Azan mgeni rasmi pambano la Kaseba na Maneno




Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MBUNGE wa Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idd Azan, amepangwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la Ubingwa wa Taifa, litakalowakutanisha Japhet Kaseba na Ramadhan Maneno, liliopangwa kufanyika Machi 2 mwaka huu, katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo ndilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa masumbwi, likiwakutanisha wakali wa ndondi, akiwamo Kaseba, aliyewahi kuwika pia kwenye ngumi za mateke.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Kaseba alisema kuwa pambano lao litahudhuriwa na mbunge wa Kinondoni, akiwa na shauku ya kutaka kujua nani mkali.
Alisema katika masumbwi hayo, kila mmoja anataka kuonyesha makali yake, huku yeye akiwa na hamu zaidi ya kuonyesha kwanini anakimbiwa na mabondia wengi.
“Nimekuwa nikikimbiwa sana na mabondia hapa nchini, hivyo naamini katika pambano hili ambalo mgeni rasmi atakuwa mbunge wa Kinondoni, nitaonyesha ukweli huo.
“Kila kitu kinaendelea vizuri kuelekea katika patashika hiyo itakayokutanisha pia mabondia wengine wenye uwezo, akiwamo Mtambo wa Gongo na wengineo,” alisema.
Mwaka jana Kaseba alishindwa kupigana na Francis Cheka, licha ya kutangazwa mno na wadau wa ngumi na kupangwa kufanyika katika Uwanja mpya wa Taifa

Tuesday, January 29, 2013

MABONDIA WAPIMA UZITO MASHINDANO YA KLABU BINGWA KUANZA KESHO

Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya ngome ambaye aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam Leo kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yanayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Abdallah Shamte wa Klabu ya Ashanti ya Ilala akipima uzito kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa yatakayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, January 28, 2013

masumbwi ngumi mawe yalivyofanyika tandale jana

Bondia Charles Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Adam Ngange wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumb i wa CCM Tandale Dar es salaam jana Mashali alishinda kwa point Picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com

Bondia Adam Ngange kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Charles Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika kwa mala ya kwanza katika ukumbi wa CCM Tandale Dar es salaam jana picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com
Bondia Athumani Pendeza kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Kalama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa CCM Tandele nyilawila alishinda kwa K,O raundi ya tatu picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com

Bondia Kalama Nyilawila kushoto akipambana na Athumani Pendeza wakati wa mpambano uliofanyika katika ukumbi wa CCM Tandale Dar es salaam jana Nyilawila alishinda kwa K,o raundi ya tatu picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com
Baazi ya wadau wa mchezo wa ngumi wakiwa na mabondia kutoka kushoto ni Kaike Silaju, Nassoro Choro,Selemani Kidunda, Thomas Mashali na Kibavu wakifatilia masumbwi
Bondia Fadhili Majia kushoto akikwepa konde la Antoni Mathias wakati wa mpambano wao uliofanyika CCM Tandale Dar es salaam jana Majia alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com
Bondia Hassan Mandula kushoto akimlushia makonde James Martini  wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mandula alishinda kwa point picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com

NGOWI MSIMAMIZI UBINGWA WA DUNIA


Na Elizabeth John
RAIS wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi anatarajia kuwa msimamizi Mkuu katika pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.

Ngowi anatarajiwa kuwa msimamizi Mkuu katika mpambano huo utakaowakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka Jamhuri ya Kidokrasia ya Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini na Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia.

Ngowi alisema, pambano la wawili hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight Februari 15 mwaka huu katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg.

Ngowi kama kamishena mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao ambapo mwamuzi ni Wally Snowball, Jaji namba moja Simon Xamlashe na namba tatu Jaap Van Niewenhuizen wote kutoka (Afrika Kusini) pamoja na  Jaji namba mbili Manuel Maritxalar (Spain).

Aliongeza kuwa pambano hilo ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya uradi wa IBF

Saturday, January 26, 2013

MABONDIA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WA KESHO

Bondia Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima uzito, Dar es salaam  kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Tandare.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima uzito, Dar es salaam  kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Tandare.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)    


Mabondia Hassan Mandulla na Jems Martin wanatarajia kupanda ulingoni  Kesho jumapili Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare Dar es salaam akizungumza mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta
amesema  wamepima uzito leo pamoja na kujua Afya zao mabondia wote watakaocheza kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipkizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine

Utamkutanisha Kalama Nyilawila atakaezidunda na Athumani Pendeza mpambano wa raundi nane kalama anapanda ulingoni baada ya mpambano wake wa mwisho kupondeza kwa K,O raundi ya sita na Francis Cheka

michezo mingine ni  Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Chaeles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwajempambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Anton na Rashid Mohamed Atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani


Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.

 michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.
 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

Friday, January 25, 2013

BONDIA SELEMANI GALILE AJIFUA KUMKABILI MBWANA ALLY FEBRUARY 2

Bondia Selemani Galile kushoto akijifua na Mohamed Mosco wakati wa mazozi yake ya kujitahalisha kupambana na Mbwana Ally mpambano utakaofanyika Yombo Dovya katika ukumbi wa Lupingu Pub February 2. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Selemani Galile akifanya mazoezi ya kukaza misuri ya tumbo wakati wa maandalizi ya mbambano wake na Mbwana Ally utakaofanyika Yombo Dovya katika ukumbi wa Lupingu February 2.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Selemani Galile kushoto akijifua na Mohamed Mosco wakati wa mazozi yake ya kujitahalisha kupambana na Mbwana Ally mpambano utakaofanyika Yombo Dovya katika ukumbi wa Lupingu Pub February 2. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu 

Bondia Selemani Galile yupo katika mazoezi ya maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Mbwana Ally utakaofanyika February 2 katika ukumbi wa Lupinga Pub uliopo Yombo Dovya

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Galile amesema yupo fiti kwa mpambano huo kwani kwa sasa anasubiri siku ya siku tu ili aweze kufanikisha

Galile aliongeza kuwa siku hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wakazi wa Yombo Dovya kupata burudani ya masumbwi itakayosindikizwa na mabondia chipukizi 

Antony Mathias atapambana na Abuu Mtambwe huku Ramadhani Mkundi akioneshana kazi na Kassim Gamboo na Mohamedi Zungu kutoka Zanzibar atapambana na Mbena Rajabu wa Dar

Siku hiyo ya Mpambano kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi atasambaza DVD zake mpya ikiwemo ya Marvin Hagler vs John Mugabi na Manny Pacuiao va Emanuel Juan Marquize ambazo atasambaza kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo DVD hizo zinazoelekeza mbinu na shelia za masumbwi zenye uwezo wa kuwajengea uwezo mabondia na mashabiki kujua sheria mbalimbali za masumbwi

Wednesday, January 23, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare


SUPER D BOXING COACH


Mabondia Hassan Mandulla na Jems Martin wanatarajia kupanda ulingoni Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare Dar es salaam akizungumza mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta
amesema kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipkizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine

Utawakutanisha Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Chaeles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwajempambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Anton na Rashid Mohamed Atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani


Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.

 michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.
 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

Floyd Mayweather, Jr.; bondia anayetikisa katika masumbwi

 floyd mayweather jr Floyd Mayweather, Jr.; bondia anayetikisa katika masumbwi
*Ameshinda mapambano 26 kwa Ko

KWA mabondia wengi, wanapopanda ulingoni huhitaji ushindi mzuri, ushindi ambao hautakuwa na utata katika maamuzi kwa wahusika wote wawili.

Marekani ni moja ya nchi zenye mabondia wengi wazuri duniani, ambao wamefanya vizuri katika mapambano mbalimbali yakiwemo makubwa ya mikana mbalimbali.


Floyd Joy Mayweather (Jr), ni mmoja wa mabondai waliofanya vizuri nchini Marekani na kuweka historia katika mchezo huo wa kibabe.

Bondia huyo alizaliwa Februari 24, 1977, ni bondia wa ngumi za kulipwa wa kimataifa wa Marekani, He is a five-division world champion, alishinda mataji mara saba, likiwemo la ubingwa wa lineal katika uzito wa aina tatu.


Alitwaa tuzo mara mbili ya mwaka, ikiwemo ubingwa mwaka 1998 na 2007, pia tuzo ya waandishi wa habari za ngumi za kulipwa Marekani (BWAA), bondia bora mwaka 2007. Ni bondia ambaye hajawahi kupigwa.


Kwa sasa, Mayweather anashikilia ubingwa wa WBC uzito wa welter.Ngumi ni sehemu ya maisha yake, Mayweather ambaye alianza akiwa mdogo. Wakati watoto wengine wakijiingiza kwenye mchezo wa baseballs au soka, alikuwa akijifunza kurusha ngumi na kukwepa.

Bondia huyo alikuwa ameiweka pembeni michezo mingine na kuzingatia zaidi ngumi pekee. "nadhani, bibi yangu alikuwa wa kwanza kukiona kipaji changu," alisema Mayweather, huku akitabasamu. "Wakati nikiwa kijana, nilimweleza, 'Nadhani utapata kazi.' alisema, 'Hapana, wewe zingatia ngumi.' "


"Wakati nikiwa na miaka kati ya nane au tisa, niliishi na mama katika mji wa New Jersey na mama, tukiwa saba katika chumba kimoja, wakati mwingine tulikosa umeme", alisema Mayweather. "Wakati wengine wakiniona nilivyo, hawajui nilikotokea wakati sikuwa na kitu."


Mayweather alizaliwa mjini Grand Rapids, Mich, katika familia ya mabondia. Baba yake, Floyd Mayweather Sr. alikuwa bondia mkongwe wa uzito wa welter aliyekuwa mpinzani wa Sugar Ray Leonard, mjomba wake Jeff Mayweather na Roger Mayweather, walikuwa mabondia wazuri, wakati Roger ni mkufunzi wa Floyd, aliyeshinda ubingwa wa ngumi mara mbili.


Mayweather limetokana na jina la mwisho la mama yake, lakini jina lake la mwisho lilibadilika na kuwa, Mayweather  muda mfupi baada ya hapo. Baba yake Mayweather, Floyd Sr., alikuwa upande wa kuuza madawa.


Ilikuwa siyo kitu cha ajabu kwa Floyd mtoto kurudi nyumbani na kujidunga sindano ya madawa ya kulevya, wakati mama yake pia alikuwa ameathiriwa na madawa hayo, huku shangazi yake alifariki kwa ugonjwa wa ukimwi kwasababu ya kutumia madawa ya kulevya.

Wakati wote, baba yake alikuwa akimpeleka gym kwa ajili ya mazoezi ya ngumi, kwa mujibu wa Mayweather. "Sikumbi kila alipokuwa akinichukua au kufanya chochote ama baba anachokifanya kwa mtoto wake, kwenye hifadhi au filamu au kula askrimu," alisema. "wakati wote alikuwa akisema anampenda mtoto wake wa kike.


Floyd Sr.  alisema hakuwahi kumweleza mapema uhusiano wake mapema. "Ingawa baba yake alijihusisha na kuuza madawa, sikuweza kumhusisha mwanangu," alisema Floyd Sr. . "Madawa niliyokuwa nauza ilikuwa sehemu ya maisha. Walikuwa na chakula cha kutosha. Walikuwa na mavazi mazurina nilikuwa nikiwa fedha. Kila mtu atakueleza kuwa, nilikuwa nikiwajali watoto wangu."


Mayweather ana rekodi ya kushinda mapambano 84–6, katika ngumi za ridhaa, na kutwaa tuzo ya dhahabu mwaka 1993, 1994 na 1996.


Kwa ushupavu wake, alipewa jina la utani "Pretty Boy" na marafiki zake wa ngumi za ridhaa, kwasababu alikuwa makjovu machache kutokana na kulinda na wapinzani wake wakati wa mapambano.

Uwezo wake huo ulitokana na mbinu alizokuwa akifundishwa na baba yake na mjomba wake Roger, ambapo katika michuano ya olimpiki ya mwaka 1996 iliyofanyika mjini Atlanta, Mayweather alitwaa medali ya shaba, baada ya kutinga hatua ya nusu fainali katika uzito wa feather kg 57.


Katika mapambano ya ufunguzi, Mayweather aliongoza kwa pointi 10–1, dhidi ya Bakhtiyar Tileganov wa Kazakhstan, kabla ya kushinda mzunguko wa pili kwa mwamuzi kusimamisha pambano.


katika mzunguko wa pili, Mayweather alimzima Artur Gevorgyan wa Armenia kwa pointi16–3. Katika hatua ya robo fainali , bondia huyo mwenye miaka 19,  Mayweather, alipigwa na bondia mwenye miaka 22, Lorenzo Aragon wa Cuba kwa pointi 12–11, na kuwa bondia wa kwanza wa marekani kuchapwa na biondia kutoka Cuba katika kipindi cha miaka 20. Kwa mara ya mwisho, hilo lilitokea mwaka 1976, kwenye michuano ya Olimpiki, wakati mabondia wa Marekani walitwaa medali tano za dhahabu, ikiwemo ya bondia nyota wa wakati huo, Sugar Ray Leonard.

Katika hatua ya nusu fainali ya kuwania medali ya shaba fedh dhidi ya Serafim Todorov wa Bulgaria, Mayweather alipoteza pambano kwa maamuzi ya utata kama ilivyokuwa kwa Roy Jones Jr.'s decision.


Kocha wa Marekani Gerald Smith alikata rufani, akilalamika kuwa, Mayweather alipiga ngumi, lakini hazikuhesabiwa, wakati Todorov aliongezewa pointi bila ya kurusha ngumi.

"Majaji walitoa hukumu kama inavyostahili," alisema Waeckerle. Majaji walishindwa kupunguza pointi mbili Todorov baada ya kufanya makosa mara tano.


"Kila mmoja anajua Floyd Mayweather, alikuwa bondia mwenye medali ya dhahabu katika uzito wa kg5 7," alisema Mayweather.

Mayweather alianza pambano lake la kwanza la ngumi za kulipwa Oktoba 11, 1996, dhidi ya Roberto Apodaca, na kumtwanga katika mzunguko wa pili.


Wakati huyo, kocha wake alikuwa mjomba wake Roger Mayweather, kwasababu Floyd Mayweather, Sr. alikuwa bado gerezani, baada ya kukamatwa na madawa ya kulebya mwaka 1993.

Mayweather, Sr. alichukua nafasi ya kumfundisha Mayweather, Jr.'s , baada ya kutoka gerezani, wakati huo mtoto wake tayari alikuwa amepanda ulingon mara 14, mara mbili akiibuka na ushindi wa mapema. Mwaka 1996 na mapema mwaka 1998, Mayweather alishinda baadhi ya mapambano kwa knockout au TKO.


Mayweather alikuwa bondia wa kwanza wa Marekani kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1996, nambapo promota wake Bob Arum alisema: "Tunaamini kutoka moyoni kuwa, Floyd Mayweather ni bondia anayefuata nyayo za Ray Robinson, na kufuatia Muhammad Ali, baadaye Sugar Ray Leonard," alisema Bob Arum.


Baada ya kutwangana na Gatti, Mayweather alihamia uzito mwingine, ambapo Novemba 19, 2005, alipigana na Sharmba Mitchell, pambano ambalo halikuwa la kuwania mkanda.


katika mzunguko wa tatu, Mayweather alimtwanga kwa Ko Mitchell kwa ngumi ya kulia iliyotua kichwani na kumpeleka chini, na katika raundi ya sita alimpiga tena Mitchell ngumi nzito iliyomta mchezoni na kumaliza pambano.

Aprili 8, 2006, Mayweather alimpiga Zab Judah na kutwaa mkanda wa IBF wa uzito wa welter. Kabla ya hapo, the fight baada ya Judah kupoteza mikanda yake ya WBA na WBC, lakini kambi ya Mayweather na Judah, waliingia makubaliano ya kuchapana makonde.


Mayweather katika pambano hilo alishinda kwa pointi 116–112, 117–111, na 119–109,ikionesha alirusha ngumi mara 188 dhidi ya  82 za Judah.


Siku tano baada ya pambano, Mamlaka ya ngumi ya Nevada iliamua kumpiga faini Roger Mayweather ya dola 200,000 na kumsimamisha kushiriki ngumi kwa mwaka mmoja.

Kusimamishwa kwake, kulikuwa na maana kuwa, Roger atakuwa akimfundisha Mayweather, Jr. katika gym, lakini hataruhusiwa kuwa katika kona ya bondia wake.


Bingwa mara saba, Manny Pacquiao iliripotiwa kuwa, yupo tayari kutwangana na Mayweather Machi 13, 2010, kwa kitita cha dola 50 milioni, huku mapromota wote wakikubaliana na hilo.

Pambano hilo halikufanyika baada ya Floyd Mayweather kutaka wapimwe damu zao kuchunguza matumizi ya dawa, lakini kambi ya Pacquiao ilikataa, na kuweka masharti kuwa,l itawezekana kama watapimwa kwa kuchukuliwa damu wiki moja kabla ya pambano.


Kwa hiyo, Januari 7, 2010, promota wa Pacquiao, Bob Arum alisema pambano hilo halitafanyika na kutoa nafasi ya kwa Pacquiao na Joshua Clottey, wakati Mayweather alikubali kupigana na Shane Mosley.


Julai 26, 2010, Ross Greenburg alisema katika taarifa yake kuwa, alizungumza na wawakilishi wa pande zote mbili tangu Mei 2, 2010, lakini pande zote mbili hazikuafikiana. Floyd Mayweather Jr., baada ya makubaliano ya mara ya pili kuvunjika, aliiambia Associated Press kuwa, alijua siku 60 kabla, hivyo hakuwa na mawazo ya kupigana na Pacquiao na hafikirii ngumi tena kwa wakati huo.

Mwaka mmoja baadaye, Julai 8, 2011, Manny Pacquiao, mshauri wake mkubwa Michael Koncz, alithibitisha kuwa, Pacquiao hakuwa tayari kuchunguzwa damu yake mpaka hivi sasa, kitu kilichoonekana kuwa, tofauti kwa Bob Arum na kambi ya Pacquiao, ilivyokuwa ikisema karibu mwaka wote.

Juni 7, 2011, Mayweather, aliatangaza kwenye mtandao wa  Twitter kuwa, atawania mkanda wa WBC katika uzito wa Welter dhidi ya Victor Ortiz Septemba 17, 2011. Ortiz lilikuwa chaguo la kwanza la Mayweather katika miezi 16.

katika pambano hilo, Mayweather salimtwanga Ortiz na kutwaa mkanda huo.


Makala haya yameandaliwa na Frank Balile kwa msaada wa mitandao mbalimbali, kama unahitaji historia ya mchezaji yoyote wa kimataifa, tutumie ujumbe mfupi wa maneno, 0713 405 652.
--

Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
           mhamila1@gmail.com
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Saturday, January 19, 2013

SHAURI, NJECHELE KUWANIA UBINGWA WA MABARA KESHO



Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF  INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa iringa katika pambano la kirafiki la raundi nane katika ukumbi wa  D.I.D Hall uliopo mabibo mwasho.

Mratibu  wa pambano hilo Charles Christopher mzazi  ameeleza kuwa maaandalizi ya pambano yapo kamili na mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani  na wamepima wapo sawa kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza  pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo sawa kwa kupambana.

Mabondia watakaocheza utangulizi ni kama ifuatavyo HAMIS MOHAMED na  HARUNA MNYALUKOLO, PENDEZA SHOMARI atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO na KARIMU RESPECT, DOTO MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku ISSA OMAR akizipiga na  JUMA J KASHNDE.

Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe  ama bigright amethibisha kuwa kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa  na mabondia wapo katika hali nzuri ya kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi wa DID HALL mabibo mwisho kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL RAMADHANI SHAURI  na  SAID  NJECHELE

Friday, January 18, 2013

SUPER D BOXING COACH


http://www.youtube.com/watch?v=tSv2IhXQ0lQ super d boxing coach




UNAWEZA KUANGALIA MAFUNZO MBALIMBALI YA MCHEZO WA MASUMBWI KWA KUBONYEZA HAPO JUU

Wednesday, January 16, 2013

BONDIA IDDY MNYEKE AJIFUA KUMKABILI SADIKI MOMBA FEBRUARY 14

Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Mussa Sunga katika Mazoezi yanayoendelea Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu Ilala
BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika maandalizi mazito ya kujiandaa na mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika  February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam

Bondia huyo kwa sasa ananolewa na kocha wa kimataifa wa Mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo wameweka kambi ili kumkabili Momba
Akizungumza Super D alisema kuwa amemwingiza kambini bondia wake ili aweze kumtengeneza vizuri kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba

Super D alisema kuwa mpambano huo utakuwa wa utangulizi kabla ya Deo Njiku na Omary Ramadhani kutwangana kugombea Ubingwa wa Taifa wa PST 
Kocha huyo alisema kuwa kambi yao itahakikisha inaendeleza ubabe baada ya bondia tegemeo wa kambi hiyo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kumdunda Saidi Mundi Kutoka Tanga
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.
 michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.

 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 
 
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana


MCHEZO WA DHUNA WAENDELEA KUAMASISHWA

Mchezaji wa mchezo wa Dhuna wa Klabu ya Mafia Mwinyi Hamisi (kushoto) akicheza na Sefu Fereji wakati wa mazoezi ya mchezo huo mtaa wa Mafia Dar es salaam jana.(Picha na www.burudan.blogspot.com

Monday, January 14, 2013

Mbabe wa Maoja kumvaa Ankrah wa Ghana




 Gottlieb Ndokosho akinyanyua mkanda wake
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Gottlieb Ndokosho kutoka nchini Namibia aliyemchapa kwa KO bondia Rajabu Maoja wa Tanzania, atapanda tena uliongoni Februari 2 mwaka huu katika jiji la Windhoek, nchini Namibia kupambana na bondia Prosper Ankrah kutoka nchini Ghana.
 
Wawili hao watapambana katika mpambano wa mwaka wakati Ndokosho wakati atakapotetea mkanda wa IBF wa bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito wa unyoya. Ndokosho aliupata mkanda huo tarehe 29 Septemba 2012 wakati alipomshinda Mtanzania Rajabu Maoja katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa SPK jijini Windhoek, nchini Namibia.
Akizungumzia mpambano huo, Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kimataifa Afrika (IBF) na  Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi, alisema pambano lingine Namibia litawakutanisha mabondia Albinus Felesianu wa Namibia atakapopambana na bondia Asamoah Wilson kutoka nchini Ghana katika uzito wa Super Featherweight.
Wakati huo huo bondia mkali wa Tunisia Ayoub Nefzi mwenye makao yake nchini Belgium atapambana na bondia Ishmael Tetteh wa Ghana kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG)
Bondia anayekuja juu kwa kasi wa Ghana Richard Commey atachuana na Mgahana mwenzake Bilal Mohammed kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mpambano huu utafanyika sambamba na ule utakaowakutanisha Mtanzania Fadhili Majia na Isaac Quaye wa Ghana. Mtanzania mwingine Allen Kamote atapimana nguvu na bondia machachari na bingwa wa WBA wa mabara Emmanuel Tagoe wa Ghana siku hiyo hiyo tarehe 22 Februari.
Naye bondia mwana dada Helen Joseph wa Nigeria atapambana na bondia Mariana Gulyas wa Hungary kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Unyoya. Mpambano wa wanadada hao utafanyika katika jiji la Accra, nchini Ghana tarehe 30 mwezi wa March, 2013.
Hili litakuwa pambano la kwanza kwa bondia Helen Joseph tangu apoteze pambano la IBF la ubingwa wa dunia nchini Dominican Republic alipokutana na bondia Dahianna Santana wa Domoinican Republic.
Mapambano hayo yote yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi.

Saturday, January 12, 2013

BONDIA Mtanzania Thomas Mashali ALIVYOMGALAGAZA Bernad Mackoliech WA KENYA

Bondia Mtanzania Thomas Mashali kushoto akiwa amemgalagaza bondia Bernad Mackoliech na kwenda chini akimsubili ili amwendelezee kipondo wakati wa mchezo wao wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam na Mashali kuibuka na ushindi wa K,O katika raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 Bondia Bernad Mackoliech wa kenya na Mtanzania Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mchezo wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki Mashali alishinda kwa K,O raundi ya sita Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo wa ubingwa wa Afrika Mashariki

Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamulu Thomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela akimvisha ubingwa wa Afrika Mashariki bondia Thomas Mashali baada ya kumpiga Bernad Mackoliech wa Kenya kwa K,O Raundi ya 6 picha na wwww.superdboxingcoach.blogspot.com

Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamulu Thomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, January 11, 2013

Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania na Benard Mcociech wa Kenya wapima uzito


Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania (kushoto) na Benard

Mcociech wa Kenya wakitunishiana Misuli baada ya kupima

Uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao wa

Ubingwa wa Afrika Mashariki utakaofanyika leo katika

ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na www.superdboxing coach.blogspot.com


Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania (kushoto) na Benard

Mcociech wa Kenya wakitunishiana Misuli baada ya kupima

Uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao wa

Ubingwa wa Afrika Mashariki utakaofanyika leo katika

ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na www.superdboxing coach.blogspot.com

Wednesday, January 9, 2013

MABONDIA DEO NJIKU NA OMARY RAMADHANI KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA February 14

Rais wa PST Emanuel Mlundwa katikati akiwa na mabondia Deo Njiku kushoto na Omary Ramadhani baada ya kusaini mkataba wa kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Omary Ramadhani kushoto na Deo Njiku wakitunishiana misuri baada ya kusaini mkataba kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Rais wa PST Emanuel Mlundwa katikati akiwa na mabondia Deo Njiku kushoto na Omary Ramadhani baada ya kusaini mkataba wa kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, January 8, 2013

Wafanyabiashara wa Tanzania kuula Ujerumani




Onesmo Ngowi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati limewaalika wafanyabishara wa Tanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia Mei 21-25 mwaka huu.
 
Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200 duniani watahudhuria.
 
Taarifa iliyotumwa na Rais wa IBF Bara la Afrika na Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi, ilisema hiyo ni fursa pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huo kutangaza biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii, TEHAMA, usafirishaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini.
 
Mkutano wa mwaka wa IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta mbalimbaki za kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao mzuri wa biashara.
   
Aidha, Ngowi anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya shughuli za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia fursa mbalimbali za biashara.
 
Ngowi ataongoza ujumbe nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati wakiwamo Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.

Thursday, January 3, 2013

BONDIA LULU KAYAGE AJIANDAA KUMKABILI SALMA KIHOBWA WA MOROGORO


Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia lulu Kayage 'kulia' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, January 2, 2013

MPAMBANO WA KUFUNGUA MWAKA 2013 KUFANYIKA FRIENDS CORNER MANZESE


DAR ES SALAAM,
 Bondi wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali anatarajiwa kupanda ulingoni Januari 12 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Jijini Dar es Salaam kutetea Ubingwa wa Afika  Mashariki.
 Akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa pambano hilo Aisha mbegu alisema mashali atapambana kuzipiga na Mkenya Bernard Mackoliech mpambano utakaokuwa wa raundi 10.
 Alisema maandalizi yamekamilika ikiwa pia na kutumiwa tiketi kwa bondia huyo mkenya ambaye anatarajiwa kuwasili januari nane kwa ajili ya kupima uzito na kupanda ulingoni.
 “tunataraji mpambano utakuwa mkali wa kukata na shoka ukizingatia mashali ameweka kambi kwa muda mrefu nje ya mkoa lakini pia Mackoliech ni bondia mahiri ambaye anasaka rekodi ya kwenda kucheza nje ya nchi”,alisema Aisha.
 Alisema nafasi iko wazi kwa watu wanaotaka kudhamini ili kuhakikisha mpambano huo unafanikiwa ukizingatia ndio mpambano wa kwanza kwa mwaka 2013 na pia mashali anavutia mashabiki wengi.
 Kwa upande wake rais wa TPBO amesema mapambano ya utangulizi yanatarajiwa kuwa manne na mabondi tayari wamesaini mikataba na watatangazwa hivi karibuni.
 Bondia Thomas Mashali anatetea ubingwa huo wa Afrika mashariki na kati ambao aliupata baada ya kumpiga Mganda Medi Sebyala Jijini Dar es salaam mpambano uliohudhuriwa na mashabiki lukuki.

Tuesday, January 1, 2013

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA BONDIA DOTO KIPENGA

Waumini wa dini ya Kislam wakiombea duwa jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Doto Kipenga
Bondia wa timu ya Taifa Selemani Kidunda mbele akiwa amebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Doto Kipenga aliyekuwa bondia wakati wa uhai wake kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika makabuli ya Kigogo Mburahati siku ya Januar Mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia wa timu ya Taifa  ya Masumbwi Selemani Kidunda akiwaongoza wenzie kulibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Doto Kipenga aliyekuwa bondia wakati wa uhai wake kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika makabuli ya Kigogo Mburahati siku ya Januar Mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia wa ngumi za kulipwaJaphert Kaseba akiwaongoza wenzie kulibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Doto Kipenga aliyekuwa bondia wakati wa uhai wake kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika makabuli ya Kigogo Mburahati siku ya Januar Mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia wa ngumi za kulipwaJaphert Kaseba akiwaongoza wenzie kulibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Doto Kipenga aliyekuwa bondia wakati wa uhai wake kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika makabuli ya Kigogo Mburahati siku ya Januar Mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com