Tangazo

Pages

Saturday, November 28, 2015

KOCHA SUPER D AMNOWA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfanyisha mazoezi ya nguvu  na kujenga misuli bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro desemba 25 Picha na SUPER DBOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifundishwa jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'UpCat' wakati wa mazoezi ya bondia huyo kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER DBOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' juu akimfanyisha mazoezi ya misuli ya shingo kupandisha na kushusha shingo uku akiwa juu ya bondia  Ibrahimu Class 'King class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano ya kitaifa na kimataifa ya bondia huyo Picha na SUPER DBOXING NEWS 
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amendelea kuwamwagia sumu mabondia Ibrahimu Class 'king Class Mawe' na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

wakati Class akimvaa Twaha Kassimu bondia vicent Mbilinyi atavaana na bondia mkongwe kabisa Deo Njiku wa Morogoro

akizungumzia mazoezi ambayo anampa bondia bigwa wa mikanda miwili ya U.B.O na WPBF Afrika Ibrahimu Class ambapo kwa sasa anamfanyisha mazoezi ya kumjengea nguvu pamoja na akili kwa ajili ya mchezo wake ujao

ambapo amekuwa akimfanyisha mazoezi mbalimbali ya nguvu yakiwemo ya kujenga misuli ya tumbo pamoja na shingo ambapo bondia huyo kwa sasa anafanya mazoezi mara tatu kwa siku na kusimamiwa vizuri

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

KOCHA SUPER D AMNOWA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifundishwa jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'UpCat' wakati wa mazoezi ya bondia huyo kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER DBOXING NEWS

KOcha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfanyisha mazoezi ya nguvu  na kujenga misuli bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro desemba 25 Picha na SUPER DBOXING NEWS

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfanyisha mazoezi ya nguvu  na kujenga misuli bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro desemba 25 Picha na SUPER DBOXING NEWS

Ibrahimu Class king class mawe akiwa na kocha Rajabu Mhamila Super D
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' juu akimfanyisha mazoezi ya misuli ya shingo kupandisha na kushusha shingo uku akiwa juu ya bondia  Ibrahimu Class 'King class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano ya kitaifa na kimataifa ya bondia huyo Picha na SUPER DBOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila' Super D' akimfanyisha mazoezi ya tumbo bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassim utakaofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER DBOXING NEWS

Saturday, November 21, 2015

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AJIFUA KUMKABILI TWAHA KIDUKU DESEMBA 25 MOROGORO

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akifundishwa ngumi za kwenda kasi zilizo nyooka na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Class anajiandaa na mpambano wake na  Twaha Kassimu 'Kiduku' Desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akielekezwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' jinsi ya kupiga ngumi za tumbo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassim 'Kiduku' wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika uwanja wa basketboll shule ya uhuru Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' NA KOCHA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'

Bondia ibrahimu Maokola kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya Class kujiandaa na mpambano wake wa desemba 25 kupambana na Twaha Kassimu mpambano utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia ibrahimu Maokola 'kushoto' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya Class kujiandaa na mpambano wake wa desemba 25 kupambana na Twaha Kassimu mpambano utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro katikati  ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwasimamia mazoezi haya ya kupigana Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na mabondia kutoka kushoto Ibrahimu Class 'King clas Mawe' Ibrahimu Maokola na Yusuph Kasimu wakati wa mazoezi yanayoendelea katika uwanja wa basketboll shule ya uhuru Dar es salaam
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kutupa makonde makali  wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake desemba 25 na Twaha Kassim 'Kiduku'  yanayoendelea katika uwanja wa basketboll shule ya uhuru Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA TAMBA NA MWAKANSOPE KUPIGANA KESHO JUMAPILI MANZESE

Mabondia Ibrahimu Tamba kushoto akitunishiana misuli nas Baraka Mwakansope baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa utakaofanyika manzese frends corner siku ya jumapili picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA Ibrahimu Tamba wa Dar es salaam na Baraka Mwakansope wa Mbeya wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 72 utakaofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese mpambano uho wa raundi kumi utanza saa kumi za jioni

wakisindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Pius Kazaula wa Morogoro atapambana na  Chisora Mawe na Vicent Mbilinyi atapambana na Said Tompoo wa Bagamoyo 

na Julius Kisarawe atapambana na Ramadhani Kumbele mpambano wa ubingwa kg 51

na Mfaume Mfaume atamenyana na Mrisho Adam katika mpambano kg 63 raundi nne

Mohamed Kashinde atakabiliana na Twawabu Issa na Iddi Kayumba atamenyana na Manny Issa 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Tuesday, November 17, 2015

MABONDIA WA MOROGORO WATAMBA KUWASAMBALATISHA WA DAR

Mabondia kutoka morogoro wakiwa katika pozi mara baada ya kuongea na wahandishi wa habari juu ya mpambano wao wa desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro kutoka kushoto ni Epson John atakaezipiga na Sadik Momba, Kudra Tamimu atakaezipiga na Mohamed Matumla na Twaha Kiduku atakaezipiga na Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Promota wa mpambano wa masumbwi Kaike Siraju kushoto  akimwinua mkono juu bondia Twaha Kiduku wakati wa utambulisho wa mpambano wake wa desemba 25  na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' utakaofanyika uwanja wa Jamuhuri Morogoro mwingine ni bondia Kudra Tamimu atakaezipiga na Mohamed Matumla Siku hiyo Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Kaike Airaju akimwinua mkono juu  Bondia Epson John kwa ajili ya utambulisho wa mpambano wake wa Desemba 25 na Sadiq Momba utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Monday, November 16, 2015

MJUWE BONDIA LULU KAYAGE ANAETAMBA KATIKA ANGA ZA KIMATAIFA

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimnowa bondia Lulu Kayage wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa kugombania mkanda wa taifa desemba 25 na bondia Mwanne Haji mpambano utakaofanyika mkoa wa Morogoro katika uwanja wa jamuhuri picha na SUPER D BOXING NEWS

BONDIA LULU KAYAGE

 Katika kipindi cha hivi karibuni wamewika mabondia wengi sana nchini lakini kwa sasa mabondia wanaotamba na kufanya vizuri wana hesabika ukiondoa kwa upande wa wanaume bondia anaekuja juu zaidi kwa sasa kwa upande wa wanawake ni Lulu Kayage 

akizungumza na mwandishi wa makala haya 
bondia huyo kwa ajili ya kuelezea maisha yake  nje ya ulingo. Yafuatayo ni mahojiano hayo:

 mwandishi, Unajihusisha na mchezo  wa ngumi ambao wengi wanaona ni wa kiume, je kama msichana ni changamoto gani unakumbana nazo katika maisha?

Lulu: Kwa kawaida unapokuwa kwenye mchezo wa masumbwi  mtaani watu wengi wanakuogopa wanakuchukulia   kama mgomvi muda wowote unaweza  kupigana na mtu lakini ni tofauti  kwa sababu ukishaingia huku hupigani hovyo.  Changamoto nyingine mimi  nikiongea  sauti yangu  ya asili ni kubwa hivyo ninapokuwa kwenye biashara zangu mtu anaweza akaja kununua kitu nikimjibu anaona naongea kwa hasira wakati sio hivyo.
 mwandishi: Ni kweli huwa mnakuwa wababe na wewe uliwahi kupigana  na mtu mtaani huku ukiwa bondia?
Lulu: Zamani nilikuwa napenda ugomvi  na mtu akinichoza nampiga kweli  lakini  tangu  nimeanza mazoezi ya ngumi hali hiyo iliondoka na kama kupigana najisikia raha nikiwa ulingoni ni kupigana  na bondia mwenzangu. Hata sasa akitokea  mtu aseme tupigane hadharani  tofauti na mchezo naogopa na ninaweza kupigwa  kwa kuwa nitapigana kwa hofu ya kuwa  ninayepigana naye nitamuumiza endapo  nitampiga sehemu mbaya kwa sababu uwezo wa kunipiga hana.
mwandishi: Familia inachukuliaje kazi unayofanya ya kupigana ngumi  na wewe ni mtoto wa kike?
Lulu: Wamepokea vizuri tu na wananiaunga mkono kwa sasa lakini nilivyoanza niliwaficha na walifahamu kuwa nacheza ngumi baada ya kuona picha yangu kwenye gazeti  napigana  wakashangaa na  kuniuliza imekuwaje  nimeingia huko wakati wanajua mimi nafanya riadha.
mwandishi: Kama watu wanakuogopa rafiki zako  wa karibu ni kina nani?
Lulu:Mimi marafiki zangu ni watoto wa kiume kwa bahati mbaya au nzuri sina rafiki wa kike, ukiniona nimeongozana na msichana ujue ndugu yangu. Sina mazoea na wasichana tangu nilipokuwa shuleni.
mwandishi: Kwa nini hupendi kuwa na marafiki wa kike?
Lulu: Wanawake mara nyingi wanakuwa na midomo  ya kuzungumza mambo ya watu yasiyowahusu sasa mimi sipendi. Hata  nyumba niliyopanga wanajua kama rafiki zangu wanaofika nyumbani kwangu ni wavulana. Imefikia hadi wasichana wenyewe wanashindwa kunizoea hawajui  waanzie wapi  kuwa na urafiki na mimi  kwa sababu mambo ya kujadili watu siayapendi  lakini nikiwaona mahali wamekaa nawasalimia kama kawaida.
mwandishi: Kuna vitu vingine  katika maisha lazima umshirkishe msichana mwenzako,  huwa unafanyaje wakati watu wako wa karibu wavulana?
Lulu: Nikihitaji  ushauri au vitu vinavyohusu msichana huwa nawashirikisha wasichana ambao ni ndugu zangu.

mwandishi: Mara nyingi mavazi yako huwa kama ya kiume, je hiyo inatokana na  unavyokaa  karibu nao?
Lulu: Nahisi hivyo kwa sababu  siku nikivaa gauni sijui kuna nini sio rahisi. Lakini Kikubwa  kilichochangia  kupenda mavazi haya ni kwa sababu nimelelewa na baba  tangu nikiwa na miezi mitano baada ya mama yangu kufariki. Unajua  mwanaume anavyolea mtoto huwa hamvalishi sketi kutokana na mazingira na ikawa nikivalishwa sketi nalia kutwa nzima  hata nilivyoanza  shule nguo niliyoshonewa juu sketi ndani imetengenezwa kama suluari
mwandishi: Umeolewa, una mchumba au unaishi na nani?
Lulu: Sijaolewa na wala sina mchumba, ninaishi mwenyewe.
mwandishi: Kwa nini au ndio  hivyo wanakuogopa?
Lulu: Nadhani muda bado haujafika na wapo wanaonifuata nakataa kwa sababu  wengi ni vijana ambao siwaelewi kwa kuwa haiwezekani mtu aje amevaa suluari mlegezo halafu nimkubali. Mimi navaa suluari lakini sipendi mtu anaevaa mlegezo.
mwandishi: Maisha ya kuishi msichana peke yake yana changamoto gani?
Lulu: Binafsi nayaona ni mazuri kwa kuwa napenda kujishughulisha na kazi. Nilikuja mjini nikiwa mdogo nikitokea Iringa na kufanya kazi za ndani kwa miaka miwili bila malipo.
mwandishi: Uliwezaje kufanya kazi bila malipo na ulikuja kulipwa fedha zako baadaye?
Lulu: Nilikuja kuondoka, bahati nzuri mama niliyekuwa naishi naye alikua anafuga ng’ombe  akawa ananipa maziwa nauza hivyo nikawa napata hela kidogo  ambazo nabakisha sokoni  nikafungua akaunti benki nikawa naweka hadi  nikafikisha 600,000 nikaondoka  nikatafuta chumba. Kutokana na utoto nilipata shida kupata kwa kuwa kila ninapokwenda kwa mwenye nyumba ananikataa hadi  nikatafuta msaada polisi wakaniasaidia.
mwandishi: Ilikuwaje ukaingia kwenye ngumi?
Lulu: Ni mchezo niliokuwa naupenda, kwa kuwa nilikuwa nafanya mazoezi ya riadha nikakutana na kijana mmoja  anaitwa Omari Bai nikamuuliza  wapi wanafundisha ngumi akanipeleka kwa mzee Habibu Kinyogoli 'Masta'.
mwandishi: Unafanya mazoezi mara ngapi kwa siku?
Lulu: Mazoezi nafanya mara mbili.
mwandishi: Unapendelea chakula gani?
Lulu: Napenda ugali maharage na mboga za majani na asubuhi napendelea kula matunda.
mwandishi: Kitu gani kinakuongezea kipato?
Lulu: Nafanya biashara ya matunda. Nina genge langu la kuuza matunda lipo maeneo ya  Mkwajuni, Kinondoni.
mwandishi: Kuna  vishawishi vingi kwa vijana kama vile matumizi ya dawa za kulevya  hasa ukiwa kwenye michezo, wewe unajizuaje?
Lulu: Namshukuru Mungu malezi ya baba yamenilinda kwa kuwa sijawahi kumuona akivuta sigara, kunywa pombe au kuingiza mwanamke ndani  hivyo ni ngumu mimi kufanya vitu hivyo. Nikiwa na rafiki anatumia vitu hivyo naepukana naye.
Bondia huyo kwa sasa anasimamiwa mapambano yake ya ndani na nje ya nchi na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchinin 

MBILINYI ATAMBA KUENDELEZA UBABE JUMAPILI

Na Mwandishi Wetu 

BONDIA Vicent Mbilinyi ametamba kumsambalatisha Said tompoo wa bagamoyo wakati wa mpambano wao utakaofanyika novemba 22 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam

bondia huyo alieweka kambi nje ya jiji la Dar es salaam amesema kuwa ajakikisha anacheza kufa na kupona kwa ajili ya kumsambalatisha bondia huyo

Mbilinyi aliyopo katika usimamizi wa Super D Boxing Promotion amesema kwa sasa ni wakati wake kwani akina wa kumsimamisha kabisa katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha bondia Pius Kazaula wa morogoro atakaezipiga na Abdalla Ruwanje na

Ramadhani Kumbele atakabiliana na Julius Kasarawe wakati Ibrahimu Tamba atamenyana na Baraka Mwakansope wa mbeya

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

BONDIA MESHACK MWANKEMWA BINGWA MPYA WA KG 66 TPBC

Refarii wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Kondo Nassoro kulia akimnyoosha mkono juu bondia Meshack Mwankemwa baada ya kumnyuka bondia Hamisi mwakinyo katikati ni Promota wa ngumi za kulipwa Jay Msangi akimvalisha mkanda bingwa huyo mpya wa Kg 66 anaetamuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC kulia ni Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Meshack Mwankemwa kushoto akiwa na bondia Hamisi Mwakinyo na viongozi na kulia ni Shomari Kimbau wa pili kulia ni rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa na Jay Msangi
Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Asha Nzowa 'Asha Ngedere' jkulia akipambana na Joyce Awino wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam mpambano uho ulimalizika kwa sare  picha na SUPER D BOXING NEWS

Refarii Kondo Nassoro katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kutoka droo picha na SUPER D BOXING NEWS

Friday, November 13, 2015

MABONDIA HAMISI MWAKINYO NA MESHACK MWANKEMWA KUPIGANA KESHO JUMAMOSI

Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC  katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NESW

Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau akiwa na mkanda utakaogombaniwa Picha na SUPER D BOXING NESW

Mabondia Hamis Mwakinyo na Meshack Mwankemwa wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa KG 66 utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam jumamosi Picha na SUPER D BOXING NESW

Bondia Joyce Awino akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Asha Nzoa kushoto mpambano utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Dar es salaam kulia ni Rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa Picha na SUPER D BOXING NESW

Bondia Asha Nzowa kushoto akitunishiana misuli na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NESW

Promota Shomari Kimbau akiwainua mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho

Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam

NA Mwandishi Wetu

MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66 unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa utapiganiwa na mabondia hawo kesho

akizungumza wakati wa upimaji wa uzito promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66

mpambano uho utasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za utangulizi za mabondia mbalimbali

Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed

na mpambano mwingine wa kusisimua utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi  

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Wednesday, November 11, 2015

BONDIA VICENT MBILINYI KUPANDA TENA URINGONI NOVEMBA 22 MANZESE

BONDIA VICENT MBILINYI

BONDIA VICENT MBILINYI

bondia vicent mbilinya atamba

VICENTI MBILINYI
Na Mwandishi Wetu 

BONDIA Vicent Mbilinyi ametamba kumsambalatisha Said tompoo wa bagamoyo wakati wa mpambano wao utakaofanyika novemba 22 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam

bondia huyo alieweka kambi nje ya jiji la Dar es salaam amesema kuwa ajakikisha anacheza kufa na kupona kwa ajili ya kumsambalatisha bondia huyo

Mbilinyi aliyopo katika usimamizi wa Super D Boxing Promotion amesema kwa sasa ni wakati wake kwani akina wa kumsimamisha kabisa katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha bondia Pius Kazaula wa morogoro atakaezipiga na Abdalla Ruwanje na

Ramadhani Kumbele atakabiliana na Julius Kasarawe wakati Ibrahimu Tamba atamenyana na Baraka Mwakansope wa mbeya

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

CHEKA NA MASHALI KUMALIZANA DESEMBA 25 JAMUHURI MOROGORO

MABONDIA WA DAR WATAMBA KUWASAMBALATISHA WA MOROGORO

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Kaike Siraju katikati akimwinua mkono juu bondia Thomas Mashali wakati wa utambulisho wa mpambano wake na Fransic Cheka utakaofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro kushoto ni bondia Lulu Kayage atakaezipiga na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota Kaike Siraju akimwinua mkono juu bondia Lulu Kayage wakati wa kutambulisha mpambano wake wa ubingwa na Mwanne Haji mpambano utakaofanyika Jamuhuri Mkoa wa Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA wa Dar watamba mabondia hawo wanaotarajia kupanda uringoni desema 25 mkoa wa morogoro wakiongozwa na Thomas Mashali aliye jiakikishia ushindi wa mapema kwa kumtwanga Fransic Cheka wa morogoro katika raundi za awali

mpambano wa raundi kumi utakaopigwa katika uwanja wa Jamuhuri morogoro bondia huyo mwenye mashabiki lukuki nchini aliendelea kujitamba kuwa anakwenda morogoro kufanya kazi aliyotumwa na wapenzi wa ngumi ivyo ato waangusha

kwa kuwa  wapenzi wa ngumi watakuja kuangalia mchezo nitakao mchezea ni tofauti na yote ninayochezaga dozi ya cheka ni maalumu kwake tu

nae bondia bingwa wa mikanda miwili wa WPBF na U.B.O Africa Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amejigamba kumtwanga bondia Twaha Kiduku kwani bado ni kinda sana kwa ata hivyo wembe kaulilia mwenyewe asubili kukatwa tu siku hiyo

nae bondia pekee wa kike nchini anaekuja kwa kasi ya ajabu baada ya kufanya vizuri katika michezo yake ya kimataifa Lulu Kayage amejigamba kuwa atamsambalatisha vibaya Mwanne Haji kwani atofika katika raundi ya sita ambapo kwa sasa sio lulu yule wa zamani 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Tuesday, November 10, 2015

BONDIA MICHAEL YOMBAYOMBA AZIKWA KIBAHA MKOA WA PWANI

Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini BFT Wililo Lukelo akitoa salam za lambilambi kutoka kwa wadau wa mchezo wa masumbwi mbalimbali nchini wakati wa mazishi ya bondia Michael Yombayomba yaliyofanyika Kibaha mkoa wa Pwani jana Picha na SUPER D BOXING NEWS
Promota wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Jay Msangi akiwa akiwa amebeba jeneza la marehemu Michael Yombayomba kwa ajili ya kwenda kuzika mazishi yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani jana Picha na SUPER D BOXING NEWS

WAOMBELEZAJI WAKIPELEKA JENEZA LA MArehemu kwenda kuzika

Mtoto wa marehemi Michael Yombayomba Zakaria Yombayomba akiwasha mshumaa katika kaburi la baBA YAKE JANA

WADAU MBALIMBALI WA MCHEZO WA MASUMBWI WAKIWA KATIKA KABURI LA BONDIA MICHAEL YOMBAYOMBA BAADA YA KUMALIZA KUZIKA KATIKA MAKABURI YALIYOPO KIBAHA MKOA WA PWANI WA TATU KUTOKA KUSHOTO NI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' DAVID YOMBAYOMBA, OSCAR MANYUKA NA JAY MSANGI