Tangazo

Pages

Monday, November 16, 2015

MBILINYI ATAMBA KUENDELEZA UBABE JUMAPILI

Na Mwandishi Wetu 

BONDIA Vicent Mbilinyi ametamba kumsambalatisha Said tompoo wa bagamoyo wakati wa mpambano wao utakaofanyika novemba 22 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam

bondia huyo alieweka kambi nje ya jiji la Dar es salaam amesema kuwa ajakikisha anacheza kufa na kupona kwa ajili ya kumsambalatisha bondia huyo

Mbilinyi aliyopo katika usimamizi wa Super D Boxing Promotion amesema kwa sasa ni wakati wake kwani akina wa kumsimamisha kabisa katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha bondia Pius Kazaula wa morogoro atakaezipiga na Abdalla Ruwanje na

Ramadhani Kumbele atakabiliana na Julius Kasarawe wakati Ibrahimu Tamba atamenyana na Baraka Mwakansope wa mbeya

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile


Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment