Tangazo

Pages

Tuesday, September 30, 2014

MPAMBANO WA NGUMI KUPIGWA SIKU YA NYERERE DAY TANDIKA

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Imani Daudi anatarajia kupigan
a na Patrick  Amote kutoka kenya kwenye mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi utakaofanyika katika ukumbi wa musoma bar Tandika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Nyerere Day tarehe 14 mwezi huu mpambano huo unaoratibiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO chini ya Rais wake Yassin Abdallah 'Osthadhi'

lina marengo ya kumkumbuka baba wa taifa katika siku hiyo ya kipekee kabisa kwa nchi yetu ya Tanzania

akizungumza na mwandishi wa habari hizi Abdallah amesema kuwa kila mwaka wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkumbuka baba wa taifa hili ambaye alipenda michezo mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote hile ingawa kwa sasa michezo inabaguliwa kwa mingine kupewa ufadhili na mingine kupewa kidogo na mingine kunyimwa kabisa ufadhili

aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mbalimbali ya utangulizi moja likiwa bondia Shomari Milundi atamenyana na Suma Ninja na mapambano mengine mbalimbali

nae bondia Imani Daudi amejidhatiti kufanya kweli kwa kumsambalatisha Amote wa kenya ili aendeleze wimbi lake la ushindi na kuvutia mashabiki zaidi katika mchezo huo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Monday, September 29, 2014

Bondia wa Kike mwafrika Bintou Schmill Bingwa mpya wa ngumi Ulaya



 
,Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill,mkazi wa Ujerumani siku ya ijumaa 26.September 2014 alifanikiwa kuchukua taji la ubingwa wa ngumi za kulipwa unatambuliwa na IBF,Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake bondia Mirjana Vujic   kwa K.O katika raundi ya 3,. Pambano hilo lilionyeshwa Live katika TV channel ya euro sport na ktazamwa na maelfu ya watu wakishuhudia bondia wa kike mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radu.Bintou Schmill (30) aka The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,Katika pambano la Ijumaa 26.September 2014 liliofanyika kwenye ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied,lifanikiwa  kumpa wakati mgumu mpinzani wake kuanzia round ya kwanza hadi ilipofika raund 3 bondia Mirjana Vujickatika alipigwa kwa KO na Bintou Schmill aka "The Voice" kutangazwa ndie bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani ulaya na kuvikwa mkanda huo unatambuliwa na IBF.Bintou Schmill aka 'The Voice' anaye fananishwa na Simba Jike (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !
Mengi kuhusu bondia Bintou Schmill aka 'The Voice" usikose at For more information write to
http://www.facebook.com/schmillbintou but first all visit the lion queen

on http://www.bintouschmill.de/     also   http://www.twitter.com/schmillbintou
Vijimambo

BOXING FEATURE: KUELEKEA PAMBANO LA ALIBABA DHIDI YA THOAMS MASHALI OKTOBA 5


Allybaba Ramadhani

Masumbwi ni miongoni mwa michezo nchini Tanzania iliyowahi kuiletea nchi hii medali nyingi kutokana na umahiri wa watupa makonde kujituma vilivyo wawapo ulingoni katika mapambano yao.
Ninapozugumza hivi ninawakumbuka baadhi ya makocha na waliopo kwenye benchi kwenye mchezo wa soka wakati mwingine hutaka kurusha makonde pindi waonapo hali ni ngumu kwa timu zao.
Unamkumbuka kocha Jose Mourinho? kama sio sheria za FIFA kuwa kali angemtwanga kocha wa zamani wa Barcelona, marehemu Tito Vilanova aliyefariki mwaka huu kwa matatizo ya kansa akitoka kuachiwa mikoba na kocha wa sasa wa Bayern Munich, Pep Guardiola.
Mwingine ni German Burgos, kocha msaidizi wa Atletico Madrid akiwa na mtata mwenzake mwenye wenge la hatari, Diego Simeoni wote wakiwa waargentina waliotoka mbali lakini kwenye suala la kurusha ngumu hawajambo.
Unaweza kusema waache kufundisha soka waje, kipande hiki cha urushaji wa makonde, ha ha haaaa! Unacheka?
Hapa nchini tuna wanamasumbwi wengi ambao wamekuwa wakijitahidi kufanya mazoezi lakini hatma yao huwa ni kazi bure wafikapo katika medani ya kimataifa kutokana na mipango mibovu ya kuukuza mchezo huu.
Wapo mabondia wakali nchini wakitiwa moyo kama ilivyo katika soka wanaweza kuitangaza Tanzania kimataifa kwani hakuna kinachoshindikana.
Hata hivyo kuna madaraja ambayo mwanamasumbwi ni lazima apambane ili aweze kusonga hadi kujulikana kimataifa yakiwemo Superfeatherweight, Lightweight, Junior welterweight, welterweight, na Super welterweight.
Sijui kama watoto wetu wanajua haya!
Nchini Marekani miaka ya nyuma kabla ya mwaka 1950 kulitokea kizazi cha warusha mawe wa ukweli Willie Pep, Chalky Wright miaka ya 1944 na rekodi zinaonyesha mchezo huu ndio ulikuwa wa kwanza kurushwa moja kwa moja (live) katika luninga.
Walikuwepo George Foreman, Joe Frazier, na Muhammad Ali waliofanya vizuri katika medani hii na kulitangaza taifa la Marekani baada hapo kikaja kizazi cha kina Mike Tyson, Evander Holyfield na sasa ni kina Floyd  Mayweather.
Kimataifa zaidi wengineo ni Amir Khan, Manny Pacquiao, Marcos Maidana, Rocky Marciano na Oscar de la Hoya.
Leo, tutamwangazia bondia Alibaba Ramadhani wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro anayetarajiwa kutifuana na bondia Thomas Mashali wa Dar es Salaam hapo Jumapili Oktoba 5 mwaka huu katika pambano litakalofanyika Mkwakwani Mkoani Tanga.
HISTORIA YA ALIBABA RAMADHANI
Jina kamili anaitwa Alibaba Ramadhani (37), alizaliwa katika Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi, mkoa Kilimanjaro t
arehe 23 Machi 1977.
Alianza elimu ya msingi mwaka 1984 na kuhitimu mwaka 1990 katika shule ya msingi Korongoni iliyopo Manispaa ya Moshi.
Mwaka 1991 aliingia kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Mlite iliyopo wilayani Rombo mkoni humu.
Hata hivyo hakufanikiwa kuhitimu elimu ya sekondari kwani mwaka 1992 alifukuzwa shuleni hapo kutokana na utovu wa nidhamu.
Baada ya hapo ajitupa katika shule ya ufundi na udereva mjini Moshi akisomea masuala ya ufundi makenika katika gereji moja ambako alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika fani hiyo.
Wakati akiendelea na mafunzo ya ufundi na udereva, Alibaba alijitumbukiza katika michezo mbalimbali ikiwemo utunishaji wa misuli kwa wanaume ambapo mwaka 1998 alishiriki shindano la kumtafuta Mr. Kilimanjaro na kumaliza nafasi ya 5.
Akiwa katika michezo mbalimbali ikiwemo kurusha tufe, mpira wa kikapu mwaka 1999 alikutana na Mwalimu Yasint ambaye alimshauri atinge CCP kwa ajili ya masumbwi.
Ndipo Oktoba 1999 alipoanza mazoezi makali, ilipofika Desemba 1999 alifuzu kushiriki michuano ya masumbwi kwa timu za majeshi yaliyofanyika CCP mjini Moshi na kuishia Nusu fainali.
Mpambano anaoukumbuka ni ule aliomchana sehemu ya jicho bondia Stanley Ernest katika raundi ya nne, hivyo kushinda kwa TKO hii ilikuwa mwaka 2000 na kutwaa mkanda wa mkoa.
Pia amewahi kupambana na Joshua Onyango mzaliwa wa Kenya anayeishi Marekani hii ilikuwa mwaka 2008, pambano hilo la kirafiki lilivunjika katika raundi ya tano.
Mwaka 2014 amepambana na Erick Mwenda katika ubingwa wa UBO-Africa raundi 10 na kumtwanga kwa pointi katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Alibaba amepambana mapambano 22 akitoka sare pambano moja tu mengine akifanya vizuri.
BONDIA WA KIMATAIFA KIVUTIO
Akizungumza Alibaba alisema bondia Floyd Mayweather (37) wa nchini Marekani ndiye anayemvutia zaidi na hujisikia vizuri akimwona akishinda mapambano yake, hasa ikizingatiwa kwamba majuma machache yaliyopita amemtusua Muargentina Marcos Maidana.
KUELEKEA PAMBANO DHIDI YA THOMAS MASHALI
Wakali hawa watakuwa wakiwania mkanda wa UBO  Africa uzito wa kilogramu 72 .
Viunga vya mji wa Tanga vitarindima vigelegele na vifijo pale mabondia Ali Baba na Thomas Mashali watakapopanda ulingoni.
WITO KWA MABONDIA MAPROMOTA
Alibaba aliwataka mabondia wenzake  kufanya mazoezi na kuacha starehe na kujikita kufanya mazoezi kwa bidii zote ili kuurudisha mchezo huu kwenye zama zake.
Pia aliongeza kusema wanamasumbwi za zamani na wa kizazi cha sasa kuna utofauti mkubwa sana ikiwemo kupunguzwa kwa raundi kutoka 15 hadi kuwa chini ya 12 kutokana na wengi wao kukosa chakula cha kutosha na kujikita katika starehe badala ya mazoezi.
Hata hivyo Alibaba anayenolewa na Kocha Pascal Bruno kutoka Nairobi aliwataka mapromota wa mchezo kuacha tamaa ya fedha na badala yake wajikite kuwasaidia mabondia wao hali ambayo itaongeza hamasa kwa chipukizi.
WITO KWA SERIKALI
Aidha bondia huyo aliitaka serikali kuangazia mikoani na sio Dar es Salaam pekee kwani mikoani kuna wengi wenye uwezo wa kutosha hivyo mazingira yakiboreshwa yatasaidia kuinua mchezo huo kimataifa na kuachana na tabia ya kuwa wasindikizaji michuano mbalimbali.
Alibaba alihitimisha kwa kuwataka wakazi na wadau wa mkoa wa Kilimanjaro kuachana na dhana ya michezo hailipi na badala yake wawekeze katika m
chezo wa masumbwi badala ya kujikita katika masuala yasiyo ya kimichezo ili kuendeleza masumbwi.
Imetayarishwa na Jabir Johnson, barua pepe:jaizmela2010@gmail.com, cell: 0768 096 793

Sunday, September 28, 2014

NASSIBU RAMADHANI ADROO NA MOHAMED MATUMLA




Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana point Picha na SUPER D BLOG

Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana point Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fatuma Yazidu wakati wa mpambano wao Yazidu alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage akilalamikia matokeo ya kupigwa na Fatuma Yazidu kulia ni bondia Ibrahimi Class 'King Class Mawe' Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo pamoja na mashabiki mbalimbali
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo
 
Mabondia Juma Bigilee kushoto,Ibrahimu Class ; King Class Mawe' na Rashidi Mhamila wakiwa katika pozi baada ya mchezo kwumalizika

Friday, September 26, 2014

MAYWEATHER FULL DOLA


MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA JUMAMOSI SEPTEMBE 27 KESHO

 Bondia Nasibu Ramadhani Kushoto akitunishiana misuli na Mohamed Matumla baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho jumamosi september 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Mratibu wa mpambano wa ngumi Ibrahimu Kamwe katikati akiwangalia mabondia wa kike Lulu Kayage kushoto na Fatuma Yazidu wanavyo tunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao
Lulu Kayage na Fatuma Yazidu wakitambiana baada ya kupima uzito
Bondia Nassibu Ramadhani akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mohamedi Matumla



Mohamed Matumla akipima uzito
Bondia Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na SUPER D BLOG
Bondia Juma Fundi na Issa Omari wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage akipimwa na Daktali baada ya kupima uzito kushoto ni m,pinzani wake Fatuma Yazidu

Wednesday, September 24, 2014

PECHE BOY KUMKABILI JUMA FUNDI

Bondia Juma Fundi na Issa Omari wakitunisha misuli baada ya makubariano yakuzipiga kwa mara ya pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa

friends corner hotel manzese Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Bondia anayechipukia kwa kasi issa omar nampepeche au  “Peche boy” kama wengi wanavyomwita, ataoneshana umwamba na bondia mkongwe mwenye rekodi nzuri ya kuwapiga kina nasibu ramadhan,majia na kupoteza kwa tabu kwa miyeyusho pia ana  historia ya kuwa bondia wa kwanza  Tanzania kuwasumbua wafilipino na kucheza mapambano mengi ya ubingwa,nae  Issa Omar “peche boy” bondia wa mwananyamala anayejifua katika gym ya bigright boxing, ni kijana mwenye kipaji cha mchezo tangu mdogo na  mwenye rekodi ya kushinda mapambano yote 18  huku moja likikosa mshindi. Issa Nampepeche  baada ya kuwapiga kitandula,moro best na juma seleman, inaonekana amekwishaa komaa na sasa anakabiliana na mtihani mwingine mgumu wa juma fundi katika pambano la round nane litakalopigwa siku ya jumamosi tarehe 27/ 9/ 2014 katika ukumbi wa friends kona uliopo manzese huku yakifuatiwa na mapambano mengine ya kina Mohamed Rashid Matumla atayeminyana na Nasibu Ramadhan, Sadiki Momba na Adam Ngange pia kutakuwepo na mchezo mwingine wa kina dada nao ni kati ya lulu kayage atakayezipiga na mtoto wa bondia mkongwe Fatuma Omar yazidu.
Akizungumza na vyanzo vya habari kiongozi wa ngumi na msemaji wa pambano  Ibrahim Kamwe alisema  “ni kuwa maandalizi ya pambano zima yamekamilika na mabondia wote wapo katika hari nzuri ya mchezo huku dogo issa nampepeche akijiamini zaidi kumshinda juma fundi, na Nasibu Ramadhan akijigamba kulipa kisasi kwa muddy matumla kwa kipigo cha mbwa mwizi,. Ibrahim kamwe aliongeza kwa kusema kuwa yale malalamiko ya watu kuwa friends corner hotel viti huwa vichache yamefanyiwa kazi na katika pambano hili viti vitakuwa vingi na askari watakuwepo wengi kulinda watu na mali zao na kiingilio kimewekwa kizuri ili watu wenye heshima zao waweze kuja na kufurahia mashindano haya yenye kushirikisha mabingwa vijana wenye vipaji na  uwezo wa hali ya juu katika masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani



DVD MPYA KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION



DVD MPYA YA MSUMBWI


WBA/WBC welterweight champion Floyd Mayweather Jr (47-0, 27 KOs)
win by
Pointi 115-112, 116-111, 116-111.
 Marcos Maidana
(35-5, 31 KOs)
SASA ZINAPATIKANA KWA WEPESI ZAIDI KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO  PIGA SIMU 0754/0787/0713-406938
 DVD YA MABONDIA MOHAMED MATUMLA VS NASSIBU RAMADHANI LILILOFANYIA  DESEMBA 25/ 2013 SASA ZIPO MTAANI KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO  PIGA SIMU 0754/0787/0713-406938
DVD MPYA YA BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' VS
Mwansa Kabinga WA ZAMBIA
 08-06-2014
LILILOFANYIKA
Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia NA
KURUDI NA UBINGWA WA WPBF AFRICA  SASA ZINAPATIKANA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO  PIGA SIMU 0754/0787/0713-406938

Monday, September 22, 2014

MGM Grand ilivyotokea kuwa makao makuu ya ndondi

MGM Grand ilivyotokea kuwa makao makuu ya ndondi - 1
*Floyd Mayweather amepageuza kuwa nyumbani kwake
*Ni hoteli ya pili kwa ukubwa duniani, eneo kubwa USA
LAS VEGAS, Marekani
FLOYD Mayweather (zamani Floyd Joy Sinclai ) amepigana mara 12 mfululizo jijini Las Vegas na kati ya mapigano hayo, 10 ni katika Ukumbi wa MGM Grand Garden Arena.
Alirudiana hapo wikiendi iliyopita na raia wa Argentina, Marcos Maidana na kumshinda.
"Floyd anapopigana hapa mambo ni tofauti kabisa. Kuna miale ya umeme usiyoweza kusimulia. Kuandaa pambano kama hili ni muhimu, si tu kwa hoteli yetu lakini pia kwa jiji zima. Kuna matukio mengi makubwa, na yote ni muhimu kwetu lakini pambano la Mayweather linaacha alama yake hapa," anasema Rais wa Michezo na Matukio wa MGM, Richard Sturm.
MGM Grand ni hoteli ya pili kwa ukubwa duniani kwa idadi ya vyumba, na kwa maana ya eneo - migahawa, maeneo ya kupumzikia na kadhalika ndiyo kubwa zaidi kote nchini Marekani, ikifuatiwa na The Venetian.
MGM ilipoanzishwa 1993 ilikuwa ndiyo hoteli kubwa zaidi duniani.
Mayweather ameifanya Las Vegas kuwa nyumbani kwake, binafsi lakini pia katika tasnia ya ngumi na unaweza kumwona hapa mwaka mzima kwenye jengo kubwa lenye ghorofa 20, iwe mchana au usiku.
Kila pambano lake lina thamani ya walau dola milioni 100 kwa uchumi wa Las Vegas lakini pia kuna mapato mengine ya pauni milioni 11 yasiyohusiana na kamari za kutabiri bingwa hapa, na mamilioni hayo yanaingizwa kutokana na mapato ya kwenye migahawa, vyumba vya hoteli na mengineyo.
"Las Vegas ni Jiji la mwanga, kila kitu ni kizuri, hapa ndipo nilipoanzia tasnia ya ngumi na hapa ndipo itakapoishia. Ni moja ya sehemu nzuri zaidi nilizopata kuona duniani," anasema Mayweather.
Lakini si huyu tu anayependa hapa, wanamasumbwi wengi wamekuwa wakipigana hapa, na kama mtakumbuka tangu zamani pamekuwa kama kivutio kikubwa cha mabondia chini ya wadhamini maarufu.
Nyota wengine waliopigana katika jiji hili ni pamoja na Mohammed Ali, Sugar Ray Leonard hadi akina Mike Tyson , Oscar De La Hoya na wengine wengi ambao wamekuwa wakiziba ombwe mara tu linapotokezea, kuhakikisha burudani zinaendelea, pesa zinachumwa na raha zinapondwa.
Baada ya kushinda pambano lake la wikiendi iliyopita, Mayweather sasa anafikiria nani tena amwite hapo MGM.
Mayweather anayejulikana pia kama Pretty Boy ni Mmarekani mwenye umri wa miaka 37 na ambaye hadi sasa ana utajiri wa dola milioni 295, alizaliwa Grand Rapids, Michigan.
Katika muda wake wa kucheza ngumi za kulipwa, ameshinda mara sita ubingwa katika madaraja matano tofauti ya uzani, rekodi ambayo haikupata kuwekwa na bondia mwingine.
Madaraja hayo ni Super Featherweight, Lightweight, Junior Welterweight, Welterweight mara mbili na Super Welterweight. Hadi sasa ameshinda mapambano yake yote 47 ya ngumi za kulipwa; hajui kupoteza pambano ni nini.
Miongoni mwa mapambano hayo, 28 amewaponda wapinzani wake kwa Knockout (KO) na kwa kiasi kikubwa ni mmoja wa wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani, kama si kwamba yupo juu ya wengine.
Licha ya kutokuwa na wadhamini wengi anaoingia nao mkataba ili kuvaa vifaa vyao au kuwatangazia bidhaa zao, kwa mwaka dili za aina hiyo zinamwingizia dola milioni 80 anapopambana.
New York ndiyo ilikuwa ikitamba zamani kama makao makuu ya ndondi za ulimwengu, kwani kwa miongo mingi hapo ndipo redio, baadaye televisheni zilijenga mvuto mkubwa sana kwa watu katika sayansi tamu ya kupigana makonde.
Rekodi zinaonesha kwamba, ndondi ndio mchezo wa kwanza kabisa kurushwa kwenye televisheni moja kwa moja na hapo ni wakati Willie Pep alipohifadhi taji lake kwa kumchapa Chalky Wright mwaka 1944.
Katika baadhi ya maeneo ndondi zilipigwa karibu kila wikiendi usiku, zikawa maarufu lakini zikiandamana na machafuko mitaani, vioo vya nyumba za makazi na maduka vikivunjwa na mashabiki wanazi.
Yanakumbukwa maeneo kama  Garden  na Eastern Parkway Arena pamoja na St. Nick's na Sunnyside Gardens. Kadhalika hatutasahau Gillette na Pabst Blue Ribbon ambamo mabondia walizichapa na kuna wakati mara tatu kwa wiki pangekuwa na mapigano.
The Gillette Cavalcade of Sports yalirushwa kutoka Madison Square Garden, na ilianza rasmi kitaifa kwenye kituo cha televisheni cha NBC mwaka 1946, kabla ya kuzoeleka, kupendeka na kuwa maarufu kila Ijumaa usiku ukumbini lakini pia kwenye televisheni. ITAENDELEA WIKI IJAYO.
CHANZO: GAZETI LA SPOTILEO

Sunday, September 21, 2014

MASHINDANO YA NGUMI YA KUMI BORA YAENDELEA KUSHIKA KASI


Bondia Saleh Said wa Magereza 'kulia' akioneshana umwamba na Sudi Mohamed wa Mavituzi wakati wa mpambano wa kumi bora yanayoendelea kila jumamosi katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam Said alishinda mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Juma wa Midizini akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Jumanne Mashombo wa Ndame wakati wa mpambano wa kumi bora uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Manyara Park Mahombo alishinda kwa point
Bondia Julius Kisalawe kushoto akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi wakati wa mapumziko bondia Jumanne Mashombo wa ndame
Bondia Iddi Juma wa Midizini akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Jumanne Mashombo wa Ndame wakati wa mpambano wa kumi bora uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Manyara Park Mahombo alishinda kwa point
SUPER D BLOG
Bondia Muhsin Hashim kustoto kutoka ndame akipambana na James Edmond wakati wa mashindano ya kumi bora yaliyofanyika katika ukumbi wa manyara park Edmondi alishinda mpambano huo
Bondia Justin Alyce kushoto akipambana na Stevin Anastazia
Mkuu wa majaji Remy Ngabo akiakikisha matokeo
Bondia Ibrahimu Bakari wa Urafiki akipambana na Maulid Athumani wa JKT wakati wa mashindani ya kumi bora kwa kila uzito katika mkowa wa dar es salaam picha na SUPER D BLOG
Bondia Shabani Mohamed kushoto akipambana na Undele Langson wakati wa mashindano ya kumi bora katika kila uzito yanayo endeshwa kila wiki na chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es Salaam DABA .Langson alishinda kwa point picha na  SUPER D BLOG



Saturday, September 20, 2014

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AKIZIPIGA NA YUSUPH MNYETO KATIKA KAMBI YA ILALA AMANA


 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba na Yusuph Mnyeto wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam jana picha picha na SUPER D BLOG
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba na Yusuph Mnyeto wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam jana picha picha na SUPER D BLOG
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba na Yusuph Mnyeto wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam jana picha picha na SUPER D BLOG
Bondia Yusuph Mnyeto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class ' King Class Mawe' baada ya kumaliza kupigana katika mazoezi yanayoendelea kwenye kambi ya Ilala Dar es salaam jana
picha picha na SUPER D BLOG
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' katikati akijazwa katika fomu uku akiulizwa maswali mbalimbali kuhusu upimaji VVU UKIMWI wakati wa kuamasisha wakazi wa magomeni kagera kupima kwa hiali jana


Bondia Ibrahimu Class' King Class Mawe' baada ya kupima vvu ukimwi wakati wa kuamasisha wakazi wa magomeni kagera kupima afya zao jana

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia na Mikidadi Boika  wakati wa kampeni ya kupima vvu ukimwi iliyokuwa ikifanyika magomeni kagera Dar es salaam jana Super D na king class walipima kwa ajili ya kuamasisha wakazi wa kagera kutambua afya zao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com