Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini akimwelekeza bondia Lulu Kayage jinsi ya kukupa ngumi wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu mpambano utakaofanyika September 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kulia akielekezwa jinsi ya kupiga makomde mazito na Kocha Habibu Kinyogoli 'Masta' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu Septermber 27 katika ukumbi wa frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Juma Biglee kushoto akioneshana umwamba na Lulu Kayage wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Amana Dar es salaam Lulu anajiandaa na mpambano wake na Fatuma Yazidu utakaofanyika Septermber 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Juma Biglee wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu september 27 Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage kushoto akifanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Fatuma Yazidu september 27 katika ukumbi wa frends corene manzese Dar es salaam kushoto ni Titus Jonson Picha na SUPER D BLOG
Na Mwandishi Wetu
lulu kayage |
akizungumza wakati akiwa mazoezini katika kambi ya ilala amana Dar es salaam amemtahadhalisha mpinzani wake kufanya mazoezi ya kutosha kwani yeye kwa sasa yupo fiti kupita kiasi na akuna bondia wa kike kwa Tanzania hii mwenye uzito wake anaeweza kumsumbua kwa sasa kwani ana uzoefu mkubwa na wakutosha
aliongeza kwa kusema kuwa jinsi anavyosimamiwa mazoezi na jopo la makocha wake wanao ongozwa na kocha mkongwe nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro ambao wanamuhimiza kila wakati kufanya mazoezi ya kutosha na ndio wana muongeza moyo zaidi kwa ajili ya kufanya mazoezi
Lulu aliongeza kuwa mchezo wa masumbwi nchini wasichana wanaojitokeza ni wachache sana hivyo kukosa msisimko wa kila wakati kucheza wasichana kwa wasichana hivyo kuomba wasichana mbalimbali wajitokeze kufanya mazoezi na kucheza mchezo kwa ajili ya afya pia ni kwa ajili ya ajira kumbuka mchezo wa ngumi ni ajira kama una uwezo wa kufanya vizuri
siku hiyo pia kutakuwa na mpambano mkali utakao wakutanisha Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla mwingine ni Sadiki Momba na Adam Ngange, Issa Omari na Juma Fundi
No comments:
Post a Comment