Bondia Juma Fundi na Issa Omari wakitunisha misuli baada ya makubariano yakuzipiga kwa mara ya
pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa
friends corner hotel manzese Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia
anayechipukia kwa kasi issa omar nampepeche au “Peche boy” kama wengi wanavyomwita,
ataoneshana umwamba na bondia mkongwe mwenye rekodi nzuri ya kuwapiga kina
nasibu ramadhan,majia na kupoteza kwa tabu kwa miyeyusho pia ana historia ya kuwa bondia wa kwanza Tanzania kuwasumbua wafilipino na kucheza
mapambano mengi ya ubingwa,nae Issa Omar
“peche boy” bondia wa mwananyamala anayejifua katika gym ya bigright boxing, ni
kijana mwenye kipaji cha mchezo tangu mdogo na mwenye rekodi ya kushinda mapambano yote
18 huku moja likikosa mshindi. Issa
Nampepeche baada ya kuwapiga kitandula,moro
best na juma seleman, inaonekana amekwishaa komaa na sasa anakabiliana na
mtihani mwingine mgumu wa juma fundi katika pambano la round nane litakalopigwa
siku ya jumamosi tarehe 27/ 9/ 2014 katika ukumbi wa friends kona uliopo
manzese huku yakifuatiwa na mapambano mengine ya kina Mohamed Rashid Matumla atayeminyana
na Nasibu Ramadhan, Sadiki Momba na Adam Ngange pia kutakuwepo na mchezo
mwingine wa kina dada nao ni kati ya lulu kayage atakayezipiga na mtoto wa
bondia mkongwe Fatuma Omar yazidu.
Akizungumza
na vyanzo vya habari kiongozi wa ngumi na msemaji wa pambano Ibrahim Kamwe alisema “ni kuwa maandalizi ya pambano zima
yamekamilika na mabondia wote wapo katika hari nzuri ya mchezo huku dogo issa
nampepeche akijiamini zaidi kumshinda juma fundi, na Nasibu Ramadhan akijigamba
kulipa kisasi kwa muddy matumla kwa kipigo cha mbwa mwizi,. Ibrahim kamwe
aliongeza kwa kusema kuwa yale malalamiko ya watu kuwa friends corner hotel
viti huwa vichache yamefanyiwa kazi na katika pambano hili viti vitakuwa vingi
na askari watakuwepo wengi kulinda watu na mali zao na kiingilio kimewekwa
kizuri ili watu wenye heshima zao waweze kuja na kufurahia mashindano haya
yenye kushirikisha mabingwa vijana wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu katika masumbwi
No comments:
Post a Comment