|
Mapambano ya utangulizi yakaanza
. |
|
Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi
ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akizungumza
wakati wa mapambano hayo kati ya Bondia Said Yazidu(Tanzania) na
Djamel Dahou(Aljeria) . |
|
Muandaaji wa Pambano hilo,Andrew George
akionesha mkanda wa Ubingwa wa Afrika ulikuwa ukigombewa na Bondia
Alibaba Ramadhan(Tanzania) na Aleck Mwenda(Malawi). |
|
Mgeni rasmi ,Novatus Makunga akonesha mkanda
huo kwa mashabiki. |
|
Pambano likaanza kati ya
Bondia,Alibaba(Mwenye Bukta nyekundu) na Aleck Mwenda(Mwenye Bukta
nyeusi) |
|
Alibaba akajaribu kupiga ngumi kadri
alivyoweza. |
|
Aleck Mwenda pia akajibu mapigo ingawaje
yake yalionekana makali zaidi. |
|
Bondia Mwenda alikuwa mzuri sana katika
kujikinga. |
|
Mwenda akamsukumia Alibaba ngumi za
kutosha. |
|
Alibaba akaenda chini mara kadhaa lakini
alinyanyuka. |
|
Round 10 zikamalizika uamuzi wa majaji
ukingojewa. huku dalili zikionesha dhahiri ,Aleck Mwenda atakuwa
ameshinda. |
|
Akiwa amebebwa na wamalawi wenzake na
kushangilia ,hakuamini alichosikia masikioni mwake baada ya mshindi
kutangazwa Alibaba. |
|
Furaha ikahamia kwa
Alibaba. |
|
Mashabiki wakaingia ulingoni kwa Bondia na
Chupa za Bia. |
|
Kamanda wa Polisi wa wilaya OCD, Deodatus
Kasindo akamkabidhi mkanda Alibaba. |
|
Alibaba akifurahia mkanda wake wa Kwanza
baada ya kutangazwa Bingwa wa Ngumi
Afrika. |
|
Furaha ya Ushindi. |
|
Likafuatia Pambano la Ubingwa wa Dunia Kati
ya Bondia ,Djamel Dahou(Aljeria) na Said Yazidu . |
|
Bondia Said Yazidu wa Tanzania akapanda
ulingoni. |
|
Mpambano ukaanza. |
|
Kila mmoja akamvizia
mwenzake. |
|
Bondia Yazidu akapigwa vitasa
kadhaa. |
|
Akakaaa kwa mara ya kwanza. |
|
Akasimama kisha akajitutumua ,akapigwa
kitasa tena , |
|
Akakaa kwa mara nyingine. |
|
Akasimama tena akachezea ngumi za kutosha
. |
|
Zikampeleka chini kwa mara ya
tatu. |
|
Akanyanyuka kwa Mbinde . |
|
Ikashindikana na Bondia ,Dahou akashinda kwa
KO ndani ya dakika 2 na sekunde 7 katika round ya
kwanza. |
|
Dahou akatangazwa Bingwa. |
|
Mgeni rasmi ,mkuu wa wilaya ya Hai,Makunga
akamkabidhi mkanda ,Bondia Dahou. |
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii
kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment