Tangazo

Pages

Tuesday, April 30, 2013

MABONDIA WATUNISHIANA MISULI KUZIDUNDA KESHO KWENYE MEI MOSI PTA SABA SABA


Bondia Amosi Mwamakula kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Rais wa IBF Africa Onesmo Ngowi katikati akionesha mzani waliopimia mabondia Thomasi Mashali kushoto na Fransic Cheka kulia katikati ni Promota wa mpambano huo Adamu Tanaka picha na mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Amosi Mwamakula kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Yusuph Jibaba kushoto akitunishiana misuli na Shabani Mhamila 'Star Boy' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa mei mosi utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipimwa afya katikati ni mpinzani wake Amosi Mwamakula picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' akipimwa Afya leo kwa ajili ya mpambano wake
Bondia Amos Mwamakula akipimwa Afya
Baadhi ya mabondia watakaopambana kesho wakiwa katika picha ya poz wa pili kushoto ni Thomas Mashali,,Shabani Mhamila 'Star Boy' Ibrahimu Class' King class Mawe' wengine ni wapambe wao katika mchezo huo

Bigright amrudisha kaseba Ulingoni


bondia kamandawamakanda kushoto akitunishiana misuli na ibrahim maokola baada ya kusaini pambano lao
bingwa wa kike na msaidizi wa promota pendo njau akisimamia zoezi la usainishaji wa mikataba ya mabondia,likiwemo pambano la kuondoa utata kati ya kamanda na maokola,.bigright jafet kaseba na mabondia wengi walishuhudia

Bondia jafet kaseba anategema kupanda tena ulingoni mwanzoni mwa mwezi wa sita kuzipiga na bondia toka kenya joseph magudha katika mpambano wa kimataifa. hivyo maandalizi yamekwishaanza kwa kuwaanda mabondia watakaocheza utangulizi,kwa kuweka mapambano makali likiwemo la kamanda wa makamanda atakaezipiga na ibrahim maokola. mwanzoni maokola alikuwa amepangwa azipige na bondia toka moro na kamanda kupewa bondia mwingine, lakini kulitokea kupishana kwa maneno kati ya mabondia hao kiasi cha kutaka kupigana kavu, mabondia na viongozi waliokuwepo hapo akiwemo ibrahim kamwe walipendekeza ibadilishwe wapinzani na wawili hao wazipige kukata ngebe na majigambo ya ubabe waliyokuwa wakitupiana.mpaka sasa mapambano ya utangulizi inategemea kuwa juma seleman atazipiga na issa omar,juma fundi atapigana na moro best, yohana mathayo atazipiga joseph onyango toka kenya. na mapambano mengine yatajulishwa hapo baadae zoezi la usainishaji mikataba likikamilika

Friday, April 26, 2013

GARI LITAKALOGOMBANIWA MEI MOSI

Msemaji wa mbambano wa Thomasi Mashali na Fransic Cheka akiwa nyuma ya gari kuwaonesha wana habari gari hilo litagombaniwa kama zawadi na mabondia hawo

Tuesday, April 23, 2013

SHABANI MHAMILA 'STAR BOY' AJIFUA KUMKABLILI JIBABA MEI MOSI


Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila 'Star Boy'  katika kambi ya Ilala iliyopo Amana CCM jana Sta Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' mabondia wote wanajiandaa kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Shabani Mhamila 'Star Boy'
Ibrahimu Class 'King Class Mawe akioneshana ujuzi wa kutupiana makonde na Shabani Mhamila 'Star Boy'
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Chalo Issa wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na MWANDISHI WETU
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' anaendelea kujifua kwa ajili ya 


kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na  Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa
bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya  kujiandaa kumchakaza Jibaba ili
kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya .won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga  Theodor Luanda
Frebruary 2,1996 na kutetea vema
10 Februar1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa 
Super D
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila,Japhet Kaseba,Hassani Matumla,Rashidi Matumla dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' pamoja na mabondia mabingwa wa dunia

Sunday, April 21, 2013

MCHEZO WA MASUMBWI ULIPO HAMASISHWA CHALINZE MKOA WA PWANI



Bondia Amos Thomas  kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Edrew Joseph wakati wa mpambano wa kuamasisha mchezo wa masumbwi Chalinze Mkoa wa pwani  Juzi mchezo huo ulitoka droo picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com
Baazi ya mashabiki wakiwa na Diwani wao
Bondia Said Minyusi wa Chalinze kushoto akirusha konde ambalo alina madhala kwa Zumbe Kukwe wa Dar wakati wa mpambano wa kuamasisha masumbwi Chalinze mkoa wa Pwani juzi  Kukwe alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com
Baazi ya mashabiki waliojitokeza kuhamasisha mchezo wa masumbwi wakiangalia burudani hiyo
Mabondia walio itimisha mpambano huo wakati wa kuhamasisha masumbwi Chalinze
Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar akizungumza kabla ya mpambano wa mwisho kwa ajili ya kuhamasisha ngumi katika kata hiyo
Mwaite Juma wa Chalinze kushoto akimwangalia bondia Mussa Ali baada ya kupiga konde zito na kwenda chini
Na Mwandishi Wetu

ZAIDI ya mashabiki 300 wamejitokeza kuangalia mpambano wa Masumbwi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi Chalinze  Mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake mashindano hayo ya masumbwi yaliyoandaliwa maalumu kuhamasisha mchezo uho katika vitongoji maarufu.

Uliwakutanisha mabondia wa Dar es salaam na Chalinze na mabondia wanaotamba katika kitongoji hicho mpambano huo wa masumbwi ulioanza saa tatu ya usiku na kumalizika saa nne na nusu uliwakutanisha bondia Amos Thomas aliye toka sare na Edrew Joseph uku mpambano mwingine ukiwakutanisha Zumbe Kukwe wa Dar es salaam aliye mgalagaza bila huruma Said Minyusi wa chalinze

Mpambano mwingine ni Alex Kado wa chalinze alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Nassoro Khatibu na kupigwa kwa ponti

Pambano lililokuwa likisubiliwa na watu wengi zaidi ni mpambano uliowakutanisha Mwaite Juma wa Chalinze na Mussa Ali ambapo mwaite aliweza kumsambalatisha ali kwa TKO ya raundi ya kwanza na kupeleka shwangwe kwa wapenzi waliojitokeza katika mpambano huo

Baada ya kumalizika kwa mpambano huo Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mpambano huo alisema yupo tayali kuwanunulia vifaa vya mchezo huo ili kuendeleza masumbwi katika kata hiyo

Ambapo ame haidi kuongeza ushirikiano wa wataalamu wa masumbwi kwa kushilikiana na viongozi ili chalinzi kiwe kitovu cha masumbwi nchini

Thursday, April 18, 2013

NGUMI KUPIGWA CHALINZE


Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar
Mabondia Mwaite juma,cosmas kibuga na shabani kaoneka ni baadhi ya mabondia wa dar es salaam watakaokwenda chalinze kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa chalize.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia machipukizi ya Bigright Promotion, imaeandaa pambano hilo  litakalofanyika mei 20 ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimchezo ikiwemo chalinze.
Tumeamua kufanya chalinze kwa sababu tunataka chalinze iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa dar na wakali wa chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu. ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi Mkwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa  Chalinze bwilingu bw Nasser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka dar es salaam kwenda kushangilia na kurudi.
wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wangumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo 
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya ma bondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali
 
 
ibrahim kamwe

NGOWI KUONGOZA UJUMBE WA AFRICA AND GHUBA YA UAJEMI NCHINI UJERUMANI

Presenting report for Africa, Middle East & Persin Gulf.JPG
FOR IMMEDIATE RELEASE – WEDNESDAY 17, 2013 - Dar Es Salaam - Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye ndiye ni Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ataongoza ujumbe mzito kutoka bara la Afrika na Ghuba ya Uajemi kwenye mkutano wa 30 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA).

Mkutano huo utafanyika katika hotel ya nyota tano ya Concorde Berlin iliyo karibu na Kanisa la kumbukumbu la Kaiser Wilhelm pamoja na taasisi ya Helmut Newton na Jumba la ukumbusho wa Picha jinini Berlin, Ujerumani.
 
 
Ujumbe atakaoongoza Ngowi utajumuisha wajumbe kutoka katika nchi za Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati na mpaka sasa ni nchi 31 zitakazo jumuika katika ujumbe huo ambao utajumuisha viongozi wa mashirika mbalimbali ya kusimamia utalii, biashara na michezo.
 
 
Mbali na kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika kwa siku sita kuanzia Mei 21 mpaka Mei 26, ujumbe wa Ngowi utafanya pia mazungumzo na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali zinazosimamia Utalii, Uwekezaji pamoja na Utalii wa Michezo katika nchi ya Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya ambazo zitatembelewa na ujumbe huo.
 
 
Katika msafara huo ambao utajumuisha pia viongozi wa bodi za Utalii na Michezo kutoka katika nchi za Botswana, Afrika ya Kusini, Ghana, Misri na Falme za nchi za Kiarabu (UAE),ujumbe huo utatembelea pia nchi za Ufaransa, Ubeljiji, Uhispania pamoja na Uholanzi!
 
 
Ngowi amewahimiza watanzania juu kuchangamkia fursa za kujitangaza kibiashara nje ya nchi na kuwataka kujituma. “Ni muhimu Watanzania wakafungua macho na wajue kuwa dunia sasa ni kijiji na wasipoangalia watajikuta wanabaki nyuma kila mara” aliema Ngowi ambaye kwa ujumla alionyeha kusikitishwa na muitikio mdogo wa watanzania kwenye masuala ya kujitangaza kibishara nje ya nchi.
 
 
Ujumbe wa Ngowi utaondoka barani Afrika tarehe 17 Mwezi Mei na kuelekea Dubai ambako ndipo wajumbe wote watakapokutana tayari kwa msafara wa kuelekea jijini Berlin, Ujerumani!


Imetolewa na;

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRIKA (IBF/AFRIKA)
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Wednesday, April 17, 2013

BONDIA FADHILI MAJIHA ARUDI NA UBINGWA KUTOKA INDONESIA BAADA YA KUMDUNDA Heri Amol



Bondia Fadili Majia akiwa na kombe la ubintaifa wa wa ngumi kimaifa alililinyakua nchini Indonesia wiki iliyopita alipo mpiga bondia Heri Amol  hapa alipo rakiwa baada ya kurudi dar es salaam jana kutoka kushoto ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wengine ni mabondia Japhet Kaseba, Kanda Kabongo na Pendo Njau picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akifuraia na bondia pendo Njau baada ya kumpokea bondia Fadhili Majiha katikati aliyerudi na kombe la ubingwa aliouchukua Indonesia wiki iliyopita  baada ya kumtwanga bondia Heri Amol wa pili ni Japhet Kaseba mwingine ni Kanda Kabongo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MASHINDANO YA NGUMI TEMEKE YANAENDELEA BILA WADHAMINI

 Na Mwandishi Wetu

Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala
MASHINDANO ya klabu  bingwa ya Mkoa wa Temeke yameanza jana jijini, Dar es Salaam huku
yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati  Aprili 19 mwaka huu.
 
Lengo la mashindano hayo yaliyoanza jana ni kuinua vipaji vya mabondia chipukizi na kupata vipaji bora watakaokuwa chachu ya maendeleo ya mchezo nchini.
 
Kocha wa kimataifa wa mchezo huo nchini Rajabu Mhamila 'Super D' alisema vijana wanakaoshiriki mashindano hayo walipima uzito katika Ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke Dar es Salaam.
 
Super D ambaye pia ni kocha wa timu ya Mkoa wa Ilala ambao ni waalikwa katika michuano hiyo alisema vijana wake kutoka klabu ya Amana na Ashanti watafanya vema katika mashindano hayo.
 
Mkoa wangu umetoa vijana sita ambao naamini watafanya vizuri katika mashindano hayo na kutoa upinzania mkubwa ambao utakuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huo nchini.
Super D aliwataja baadhi ya mabondia hawo kuwa ni Hussein Mawimbi na Said Hamisi kutoka klabu ya Amana na Athumani Yanga pamoja na Said Mabunda kutoka klabu ya Ashanti.
 
Pia aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano hayo yanayofanyika katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke ili kuhakikisha hamasa ya kuendeleza mchezo huo inapatikana yatakayofanikisha mafanikio ambalo ndilo lengo kubwa. la mashindano hayo

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali

MASHINDANO YA NGUMI TEMEKE YAFANA INGAWA HAYANA WADHAMINI

Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Yusuph Saidi wa Kokoto wakati wa mashindano ya Klabu bingwa ya wilaya ya temeke yaliyoanza jana Yanga alishinda kwa point na kupereka shagwa katika klabu ya Ashanti Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala akioneshwa mkono juu baada ya kumpiga Yusuph Saidi wa Kokoto wakati wa mashindano ya Klabu bingwa ya wilaya ya temeke yaliyoanza jana Yanga alishinda kwa point na kupereka shagwa katika klabu ya Ashanti Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Husein Mawimbi wa Amana akinyooshwa mkono juu baada ya kumpiga kwa point bondia Said Mabunda wakati wa Mashindano ya Klabu bingwa wilaya ya temeke Dar es salaam jana Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, April 16, 2013

TANGAZO LA MASUMBWI MEI MOSI


GHANA KUTAWAKA MOTO MEI 3, MAPAMBANO MATATU YA IBF YAJA


FOR IMMEDIATE RELEASE – MONDAY 15, 2013 - Dar Es Salaam - Nchi ya Ghana ambayo ni moja ya nchi zenye vipaji vingi vya wanamichezo mahiri na majina makubwa hususan mchezo wa ngumi, itawaka moto tarehe 3, Mei wakati mabondia mahiri sita watakapogombania mataji ya IBF katika ubingwa mbalimbali.

Bondia atakayeanza kupanda ulingoni kufukisha moto huo ni “Mtoto wa Kijiweni” Albert Mensah ambaye amejizolea sifa kemkem za kupambana na mabondia mahiri duniani. Mensah yuko kwenye viwango vya IBF vya dunia na amewekwa namba 7 kwa ubora duniani katika uzito wa Welter.
 
                 Helen Joseph
Mbabe huyu atakumbana na bondia mwenye maringo na “Mtoto wa Mjini” Ben Odamettey ambaye amekulia katika viunga vya Jamestown katika kata ya Bukom jijini Accra, ambayo ni maarufu kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na Poison Kotey. Wawili hawa watapambana kugombania ubingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa Junior Middleweight.
               Marriana Gulyas (kushoto)
 
Mpambano wa pili na unaongojewa kwa hamu kubwa ni ule wa mwanadada na mrembo kutoka Nigeria ambaye anaishi nchini Ghaba, Helen Joseph atakapombana na binti Mfalme kutoka Himaya ya Austrohungrian (Hungary) bi. Marianna Gulyas. Warembo hawa wanagombania mkanda wa IBF wa Mabara wa wanawake katika uzito wa unyoya (Featherweight) na moto mkubwa unategemewa kuwaka kutokana na umahiri wa warembo hawa wa kurusha makonde ulingoni.

Helen atakuwa anarudisha heshina yake baada ya kupoteza pambano la ubingwa wa dunia kwa mwanadada Dahianna Santana wa Dominican Republic mwezi wa Desemba mwaka jana. Hii ni heshima pekee kwa kina mama kutoka bara la Afrika wa kuonyesha umahiri wao kwa binti huyo wa Kifalme kutoka Hungary.
 
                                                          Albert Mensah (kulia)
Ndipo litakapokuja pambano la kukata na shoka kati ya mbabe kijana anayeinukia katika ulimwengu wa masumbwi nchini Ghaha na Afrika kwa ujumla bondia Issa Samir kutoka Ghana atakapopambana na mbabe kutoka kwenye jangwa la barafu la Siberia, bondia Robison Omsarashvili kutoka katika nchi ya Georgia ambayo ni moja ya nchi zilizokuwa kwenye Muungano wa Kishoshalisti wa Sovieti ya Urusi (USSR).

Ni nderemo na vifijo kwa Waghana na watu wote wa Afrika wakati mabondia hawa watakapo pambana kugombea mataji haya makubwa kabisa ya IBF na kuliwakilisha bara la Afrika katika ramani ya dunia.

Mapambano haya yanaandaliwa na kampuni ya GoldenMike Boxing Syndicate ya Accra, Ghana chini ya Henry Many-Spain na Michael Tetteh na yatafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Accra (Accra International Conference Center) na yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.

IMETOLEWA NA:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Sunday, April 14, 2013

KING CLASS MAWE AJIPANGA KUMUHADHIBU MWAMAKULA



Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kupiga maumbwi ku kupangua ngumi za mpinzani wake
BONDIA Ibrahim  Class 'King Class Mawe' amendelea kujifua na kujiandaa 
kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi  Siku ya jumatano , linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa
bondia wake anajiandaa vema na matumaini yanaonekana baada ya kucheza Sparng na watu watano tofauti tofauto ambapo alianza kupambana na Abuu Mtambwe raundi 4,Kassimu Gamboo, nae vile vile na Ibrahimu Toll pamoja na Ally Masaga kitu ambacho kimenipa moli wa kumchakaza Mwamakula ili
kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D.
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali

BONDIA STAR BOY apania kumgalagaza jibaba


Na MWANDISHI WETU
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' ameingia kambini kujiandaa 
SHABANI MHAMILA 'STAR BOY'
kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na  Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa
bondia wao ameingia kambini juzi kujiandaa kumchakaza Jibaba ili
kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya .won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga  Theodor Luanda
Frebruary 2,1996 na kutetea vema
10 Februar1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa 
Super D
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mjapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe

Thursday, April 11, 2013

KING CLASS MAWE AJIANDAA KUMKABILI AMOSI MWAMAKULA MEI MOSI



Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ally Masaga wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi dhidi ya Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde naIbrahimu Toll wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Kasimu Gamboo wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Kasimu Gamboo wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, April 9, 2013

DVD MPYA KUTOKA SUPER D BOXING COACH


MOJA YA DVD MPYA ZILIZOWASHILIKISHA WATANZANIA PEKEE

DVD PEKEE YA WANAWAKE YA BONDIA LAILA ALI