Tangazo

Pages

Saturday, April 6, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA APRIL 7 JUMAPILI MWANANYAMALA CCM


Mabondia Issa Omar na Shaban Madilu ambao wanacheza pambano lao la raundi kumi  ubingwa wa UBO international, wakisindikizwa na wakongwe wa masumbwi nchini Joseph Marwa atakaezipiga na amour mzungu katika pambano la kisasi ,baada ya mzungu kupigwa na marwa miaka saba iliyopita jumapili hii ndani ya ccm mwinjuma anataka ajiulize ilikuwaje na amepata uzoefu wa kutosha wa kulipa kisasi.
Mabondia wote hao pamoja na uzito wa juu Ramadhan kido na musa mbabe wamekupima afya zao na uzito siku ya jumamosi saa 4


hapohapo ukumbini CCM Mwinjuma – mwananyamala zoezi zima la upimaji liliongozwa na dr donard Madono akisaidiwa na Emanuel mlundwa.
Mpambano huo ulioandaliwa na bigright promotion na  kusimamiwa na PST kama mwakilishi wa UBO nchini unategemea kuwakutanisha mabondia mbalimbali wenye uwezo mzuri na kuwavutia washabiki wa mchezo huo kwa kushuhudia mapambano zaidi ya tisa kwa wakati mmoja na mabondia wanaotegemea kupigana siku hiyo ni Ide mnali toka mtwara atakaezipiga na zumba kukwe wa dare s salaam, Husein Mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atapigana na Faraji Sayuni, Salum Chandonga atazipiga na  amour mzungu ,Mohamed mzungu. Herman Richard na kade hamis, kani west na Nasor Hatibu,james Edmond na julias anastaz .pia kutakuwa na maonesho ya ngumi za watoto wenye vipaji.
Mpaka leo hii haijaripotiwa kama kuna tatizo lolote na mabondia  karibu wote wapo katika hali nzuri na wapo tayari kwa mpambano
 Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD  za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Fransic Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. nyingine zitakuwa
zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
 

No comments:

Post a Comment