Tangazo

Pages

Saturday, April 6, 2013

ZAIRA YA NGOWI NCHINI BOTSWANA YAIWEKA MAHALI PAZURI

                                                              International Boxing Federation Africa
                                                                                       IBF/AFRICA
FOR IMMEDIATE RELEASE – Saturday April 6th, 2013 -Dar-Es-Salaam - Ziara ya Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi, imeiweka nchi ya Botswana mahali pazuri kwa kuiingiza kwenye kundi la nchi nane (8) za Afrika zitakazofaidika na progra mu ya “IBF ya Utalii wa Michezo”.
Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau wa michezo alipokuwa anahitimisha ziara yake iliyomchukua kwenye majiji ya Francistown na Gaborone, Rais Ngowi aliweka bayana furaha yake kwa jinsi serikali ya Botswana kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BNSC) ilivyompa mapokezi mazuri.
Ngowi aliitembelea Botswana kuanzia tarehe 31 Machi mpaka tarehe 5 April ambapo aliweza kutembelea majiji mawili ya Francistown na Gaborone. Aidha, Ngowi aliitembelea pia miji midogo ya Molopolole,Kanye, Kang, Jwaneng na Ghanzi.
Katika miji midogo ya Ghanzi na Kanye Ngowi alijionea jinsi Botswana inavyotunza na kuendeleza vivutio vya kitalii na hivyo kuweza kujipatia pesa nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaotembelea nchi hiyo!
Programu ya “IBF ya Utalii wa Michezo” itaifanya Botswana kufaidika na ujio wa watalii kutoka nchi zaidi ya 144 ambazo ni wanachama wa IBF. Pia kutakuwa na wawekezaji watakaowekeza kwenye vivutio mbalimbali na kuifanya Botswana kuwa moja ya nchi zinazofaidika na “Utalii wa Michezo”(Sports Tourism).
Rais Ngowi aliishauri serikali ya Botswana umuhimu wa kuwekeza kwenye sekta ya michezo hususan mchezo wa ngumi na kutoa mfano wa namna nchi zinavyotumia mabilioni ya dola za Kimarekani kuandaa michezo ya kimataifa kama vile michezo ya Olimpiki na Kombe la Dunia.
Katika hotuba yake rasmi (Key Note Speech) aliyoitoa kwenye ukumbi wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha Botswana (BFA), Ngowi alieleza jinsi bondia mmoja anavyoweza kuitangaza nchi kwa kiasi kikubwa na kumtolea mfano bondia wa Botswana Lesley Sekotswe ambaye aliiwakilisha nchi vizuri alipopambana na bondia Immanuel Naidjala wa Namibia hivi karibuni.
Nalo Barala la Michezo la Botswana BNSC limemhakikishia Ngowi kuwa litafanya kila liwezalo kuuendeleza mchezo wa ngumi ambao ndio unaoitangaza vyema Botswana kwenye medani ya kimataifa. Mwenyekiti wa BNSC bwana Solly Reikeletseng pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa BNSC bwana Perscy Raditladi walitoa ahadi ya kushirikiana na IBF katika kuuendeleza mchezo wa ngumi kwa kiwango ha kimataifa.
Ngowi alimaliza ziara yake nchini Botswana jana siku ya Ijumaa na kuelekea nchini Afrika ya Kusini ambako atakuwa na ziara ya siku nne itakayoisha tareeh 9 April. Akiwa nchini Afrika ya Kusini Ngowi atafanya mazungumzo ya serikali ya nchi hiyo hususan serikali ya jimbo la Mpumalanga ambalo limekuwa likidhamini mapambano mengi ya ngumi.
Mwishini mwa April Ngowi atafanya ziara nyingine katika nchi za Ghana, Cameroon, Misri na Tunisia kujenga uwezo wan chi hizo katika kuitumia programu ya “IBF ya Utalii wa Michezo” (IBF Sports Tourism)
Picha 1: Ngowi akihutubia katika ukumbi wa BFA jijini Gaboone, Botswana!
Picha 2: Ngowi akiwa amesimama na wadau mbalimbali wa Ngumi wakiufurahia mkanda wa IBF wa Kimataifa.
Picha 3: Ngowi akiwa amesimama na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Almasi la Botswana DEBTSWANA Bi. Lesedi Rakola katika mkutano huo.
IMETOLEWA NA:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Benjamin William Mkapa Pension Towers
Tower B, Mezzanine Floor, Azikiwe Street

Dar-Es-Salaam - Tanzania

No comments:

Post a Comment