MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi
Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D
No comments:
Post a Comment