Tangazo

Pages

Saturday, March 31, 2012

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA



MABONDIA Selemani Galile na
Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa
wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika
ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa
kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es
Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha
anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika
atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue
kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo
najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali
alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa
kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka
bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote
raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa
TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia
mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo
hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri
mpinzani


Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na
huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis,
Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roj Jones na wengine wengi

Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa
mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani
ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu
Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

No comments:

Post a Comment