Tangazo

Pages

Friday, March 9, 2012

WANAFUNZI WA SHULE ZA MOSHI WAMWANDIKIA BARUA RASHID MATUMLA!!

Wanafunzi wanne wanaosoma katika shule za msingi na sekondari za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wamemwandikia barua bondia Rashid “Snake Man” Matumla wakimtakia kila la kheri katika mpambano wake na Vitaly “Siberia Tiger” Shemetov wa Urusi. Wanafunzi hao Levina Joachim(Shule ya Msingi Mwereni), John Makupa (Mawenzi Secondary), Ashura Omari (J.K Nyerere Secondary) na Oliva Philip (Shule ya Msingi ya Majengo) wamemwelezea Rashid “Snake Man” Matumla kama tegemeo kubwa la Taifa. Ifuatayo ni baadhi ya sehemu za barua zao:

“Mpendwa Golden Man, kama katika riwaya ya Sinderela natamani ungekuwa Prince wangu ninayekungojea unichukue katika mikono yako” alisema Ashura Omari katika barua yake. “Nakutakia ushindi mnono ili utimize ndoto zangu za wewe kuwa shujaa wangu kwa kumwonyesha Tiger huyo wa Siberia kuwa Tanzania tuna mabingwa wa kweli” Ashura Omari alimalizia katika barua yeke.
Oliva Philip alisema “Ni muda mrefu mji wa Moshi haujaweza kushughudia burudani kama utakayoileta wewe hivi karibuni. Naamini kuwa utaendelea kuungarisha mji wa Moshi ili kweli ujulikane kuwa ni kilele cha Afrika”
Naye Levina Joachim alisema “Golden man wewe ni nuru ambayo Tanzania iliipoteza kwa muda mrefu na tunakutegemea kuwa utairudisha na kuifanya ingare kila siku, nakutakia ushindi mzuri”
John Makupa alisema “Ningekuwa na uwezo ningekuja ulingoni siku hiyo nikakusaidia kushika mguu mmoja wa Tiger huyo wa Siberia ili umchakaze vizuri, lakini naamini kuwa utamuonyesha kuwa kweli wewe ni moto wa kuotea mbali”alisema Makupa.
Mpambano wa ngumi kati ya Rashid “Snake Man” Matumla na Vitaly “Siberian Tiger” Shemetov wa Urusi umeanza kuwa ni gumzo kubwa katika Manispaa ya Moshi huku wenyeji wengi wakifurahia na kungojea kwa matumaini makubwa ushindi wa Matumla siku ya tarehe 22 Juni mwezi wa sita.
Mpambano huo ambao utakuwa ni wa TPBC International Title katika uzito wa Super Middleweight utawakutanisha miamba miwili ya ngumi duniani. Mgeni mashuhuri katika mpambano huo atakuwa mcheza sinema mashuhuri wa Marekani Deidre Lorenz toka katika jiji la New York.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mpambano wa ngumi hapa Tanzania na Afrika nzima kuhudhuriwa na mcheza sinema mashuhuri kutoka Hollywood, nchini Marekani hivyo kulipa pambano hili sura mpya kabisa.
Bibi Deidre Lorenz atakuwa njini Moshi kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 17 Juni na pia kushiriki katika mbio za 22 za Marie Frances Mount Kilimanjaro Marathon ambazo zimepewa hadhi ya kuwa “Mbio za Marathon za kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB).
Mpambano huu una promotiwa na kampuni ya ASMM Peak Gemstone Traders LTD ya mjini Moshi na utajumuisha pia mabondia kadhaa kwenye mapambano ya utangulizi:
Pascal “Prince Kilimanjaro” Bruno atapambana na James “Sura Mbaya” Kitasi wa Kenya katika uzito wa Light Middle raundi 10 ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Bruno atakuwa anatetea mkanda wake wa ubingwa wa Afrika ya Mashariki.
Naye Alibaba “Dragon” Ramadhani atatetea mkanda wake wa Afrika ya Mashariki akichuana na Sebyala Med toka nchini Uganda katika uzito wa Middle

No comments:

Post a Comment