Tangazo

Pages

Wednesday, March 14, 2012

Bondia wa UKRAINE VITALI Klitschko kujikita kwenye siasa

KIEV, Ukraine
BINGWA wa uzani wa juu unaotambuliwa na Chama cha Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC), Vitali Klitschko amesema hana mpango wa kuwa bondia mwenye umri mkubwa kushikilia ubingwa huo na badala yake, amepanga kujikita kwenye ulingo wa siasa nchini Ukraine.
Shirika la Habri la Marekani (AP), lilimnukuu bondia huyo juzi alipohojiwa kwamba ataendelea kuzichapa kwa muda gani.
Akijibu swali hilo, bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 alisema haitakuwa muda mrefu na badala yake, atajikita kwenye siasa kutokana na kwamba nchini Ukraine kuna nafasi nyingi.
Mwaka 1994 bondia George Foreman, ndiye aliyeweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kutwaa ubingwa huo, akiwa na umri mkubwa wa miaka 45 na Klitschko, alisema kwa ujumla hataki kuvunja rekodi hiyo ya Foreman.
Kwa sasa Klitschko ndiye kiongozi wa chama cha upinzani kiitwacho 'Udar' (mgomo) na anataka kuwa meya wa mji wa Kiev nafasi ambayo aliikosa mwaka 2006, wakati alipowania kwa kauli mbiu ya kupiga vita rushwa ambapo amepania kuwa tena katika uchaguzi ambao utafanyika baadaye mwaka huu.

No comments:

Post a Comment