Tangazo

Pages

Saturday, December 12, 2015

BONDIA VICENT MBILINYI ANA UCHU WA KUWA BINGWA WA DUNIA

BONDIA VICENT MBILINYI


KATIKA miaka ya hivi karibuni takwimu zinaonesha mchezo wa masumbwi 'Boxing'  ndio mchezo wenye kuingiza pesa nyingi kuliko mchezo wowote Duniani ambapo kwa hivi sasa utajili huo unashikiliwa na bondia Floyd Mayweather akifuatiwa na Manny Paquaio ambao wote ni mabondia na namba zote mbili za juu wamechukuwa wao  michezo mingine ikifuata

hii yote ni dondoo tu zaidi hapa nataka kumzungumzia bondia chipkizi Vicent Mbilinyi 

bondia huyu alizaliwa tarehe 05/09/1992 Musoma Mara ni mtoto wa nne  katika  watoto sita wa familia ya Alphonce Mbilinyi

alipata elimu yake ya msingi kuanzia mwaka 1999 katika shule ya mzimuni iliyopo magomeni Dar es salaam na kumaliza mwaka 2015

ajapata bahati ya kuendelea na masomo kutokana na ukata wa familia kuwa na maisha magumu

Mbilinyi alianza kupenda mchezo wa masumbwi tangu anasoma darasa la kwanza ambapo alivutiwa sana na kocha Sako Mwaisege 'Dungu' ambaye alikuwa akifanya mazoezi ya ngumi na kujiunga nae kama kocha wake wa mtaani pale maeneo ya magomeni ambapo walikuwa wakijifunza mchezo uho kupitia Sako

baada ya kujifua sana kwa mazoezi na mbinu mbalimbali kutoka kwa kocha  aliamua kumpeleka katika timu ya ngome pale mwenge alipokutana na kocha Thimos Kingu na baada ya kupigana sana katika mashindano ya ridhaa na kukomaa katika mchezo wa masumbwi

baadae mazoezi ya ngome yakanishinda ambapo nilikuwa naishi Kibaha mkoa wa Pwani kwa hiyo nilikuwa natumia shilingi 5000 nikawa nimeshindwa kutokana sijakuwa na mtu yoyote wa kuniwezesha katika swala la nauli ambalo lilikuwa likinigalimu kila siku hata hivyo akuishia hapo

Mbilinyi anaeleza kuwa baada ya kutoka Ngome kocha Sako Mwaisege akampeleka moja kwa moja kwa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye mpaka sasa anafanya nae kazi ya ngumi kwa kumfundisha na kumtafutia mapambano mbalimbali nchini na nje ya nchi japo ajanza kutoka nje ya mipaka ya tanzania ila anategemea ipo siku atakuja kuvuka mipaka hiyo kwa ajili ya mchezo wa masumbwi

Mbilinyi alicheza mpambano wake wa kwanza katika ngumi za kulipwa january 30 katika ukumbi wa Manyara Park alipambana na Kulwa Bushiri mpaka sasa Mbilinyi amecheza mapambano 8 akishinda 5 droo 2 na sale 1

baadhi ya mabondia aliocheza nao ni Kelvin Majiba,Khalid Hongo,Saidi Mundi,yusufu Mkali,Epison John, Haridi Manjee,,

bondia huyo ambaye anapenda kuyaona makampuni mbalimbali yakijitokeza kufadhili mchezo wa ngumi kama wanavyofanya katika michezo mingine ambayo mpaka sasa ina wafadhili wengi ivyo kuwataka wengine wageukie katika mchezo wa masumbwi kwani kwa vijana kwa sasa ni ajira yao ambayo wanaitegemea kujikwamua kimaisha

bondia huyo pia ametoa wito kwa vijana mbalimbali kujiunga na mchezo wa ngumi kwani kwa sasa unalipa kwani wengi wa mabondia wameanza kufanikiwa kupitia ngumi

alitoa wito kwa vijana wenzie kuacha huasherati matumizi ya dawa za kulevya na uvutaji wa bangi kwani unapunguza nguvu kwa mwanamichezo yoyote yule awezi kujihusishwa na maswala hayo


KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA SUPER D AKIMNOWA BONDIA VICENT MBILINYI







No comments:

Post a Comment