Tangazo

Pages

Thursday, October 4, 2012

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AJIFUA KUMKABILI JONAS SEGU


KING CLASS MAWE AKINOLEWA NA HABIBU KINYOGOLI
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' yupo katika mazoezi mazito kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Jonas Segu litakalofanyika October 14 siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese

Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' 'amesema kuwa tuna muhandaa 'King Class Mawe'  kwa ajili ya mpambano wake huo

Tunamuhandaa vizuri ili aje kuwa bondia bora wa masumbwi hapa nchini unajua kuna stail nyingi sana za mazoezi ambazo anapewa ili kumkabili mpinzani wake kwa kuwa tunamjua vilivyo

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mazoezi anayofanyishwa 'King Class Mawe' kwa sasa akuna mtu anaeweza kumfikia kwa kuwa kashavuka viwango bondia huyo anaecheza katika uzito wa Kg 60 amekuwa tishio kwa mabondia wezake baada ya mchezo wake wa mwisho kumdunda SakoMwaisege  kwa K,O raundi ya tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, Dar-Es-Salaam

Na ataendeleza kupiga wapinzani wake kwa K,O katika raundi za mwanzo bila kuwachosha majaji pamoja na refarii wake

Aliongeza kwa Super D kuwa wanamfanyisha mazoezi ya kupiga kwa K,O ili aweze kuendeleza  rekodi aliyonayo kwa sasa kwani mapambano yako yote matatu aliyocheza kapiga wapinzani wake wa K,O

No comments:

Post a Comment