LONDON, England
BONDIA Amir Khan aliyepoteza makali katika mapambano yake ya
karibuni na kuamua kumtimua kazi mkufunzi wake, amesisitiza kutorejea tena
makosa yatakayomnyima ushindi ulingoni wakati atakapomvaa Carlos Molina.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia uzani wa ‘light-welterweight,’
anhaha kulizika jinamizi la kuvurunda lililomfanya apoteze mapambano yake
mawili ya mwisho alipoangukia pua dhidi ya Lamont Peterson na kisha Danny
Garcia.
Na sasa Khan anatambua fika kuwa kukubali kichapo cha tatu
mfululizo atakapopambana na Molina hapo Desemba 15 jijini Los Angeles, Marekani, sio tu kutaporomosha
heshima yake ulingoni, bali pia kutampotezea matumaini ya kuzichapa na Ricky
Hatton.
Tangu alipochapika kwa KO dhidi ya Garcia, Khan alijikuta
akipoteza heshima yake ulingoni, kabla ya kuamua kuachana na mkufunzi wake Freddie
Roach na kumpa kazi Virgil Hunter – aliyemuita kocha bora duniani katika kumpa
bondia uwezo wa kujilinda ulingoni.
Khan, 25, alifichua: “Sitaki kamwe kupoteza pambano hili. Sitaki
tena kuwa katika nafasi hiyo ya kupoteza pambano tena, kama
nitapoteza, basi nitafikiria, ‘Wapi napoweza kwenda kufanya kitu baada ya hapa?’
“Presha yangu ya mchezo iko juu kushinda pambano hili. Ni
kufa au kupona. Hilolimenifanya nibadilike kwa asilimia 100 katika kila idara, kila
kitu kiko kwenye mstari. Nataka kuhakikisha sifanyi tena makosa ulingoni.”
Hatton anarejea rasmi ulingoni baada ya kutoonekana huko kwa
miaka mitatu tangu Novemba 24 alipopanda ulingoni MEN Arena katika mji wa
kuzaliwa wa Manchester
na tayari amejinasibu kuhakikisha anamtandika Khan Desemba 15.
No comments:
Post a Comment