Tangazo

Pages

Tuesday, October 16, 2012

WALIOMPORA AMIR KHAN KUKIONA CHA MOTO




LONDON, England
“Ni suala la wakati tu, vijana wote waliohusika watakamatwa, kabla ya kutambuliwa. Walichofanya ni kitendo cha jinai, tena watajutia aibu yao kwa kumshambulia mtu wa kupigiwa mfano nchini”
BINGWA wa zamani wa IBF na WBA katika uzani wa ‘light welterweight,’ Amir Khan anajiandaa kukagua gwaride la utambulisho hivi karibuni, kuwatambua majambazi waliojaribu kumuibia gari lake lenye thamani ya pauni 100,000 aina ya Range Rover.
Khan alikuwa njiani akisafiri kwa gari hiyo akitokea jijini Birmingham, wakati aliposhambuliwa na genge la majambazi sita waliokuwa kwenye jaribio la kumpora gari hilo akiwa na ndugu yake Haroon, ambaye pia ni bondia wa ngumi za kulipwa.
“Ni suala la wakati tu, vijana wote waliohusika watakamatwa, kabla ya kutambuliwa. Walichofanya ni kitendo cha jinai, tena watajutia aibu yao kwa kumshambulia mtu wa kupigiwa mfano nchini,” alisema mshirika wa Khan katika mahojiano yake na The Sun.
Tukio hilo limetokea wiki iliyopita na hivi karibuni video yake ikaingizwa kwenye mtandao wa YouTube na mmoja wa majambazi hao, ili kumtisha Khan kwa uamuzi wake wa kuliacha sakata hilo mikononi mwa upelelezi wa polisi. 
Jambazi huyo aliyevalia kinyago kuficha sura yake, katika video hiyo ameonesha pochi na funguo ya gari vyote vya Khan, akidai kuwa nyota huyo alivitelekeza vitu hivyo na sio wao waliopora.
Mshirika wa Khan akaongeza: “Sisi tumekuwa tukipata habari nuyingi tofauti tofauti tangu gazeti la The Sun lilipoitoa habari za uwapo wa upepelezi wa tukio hilo. 
“Sisi tuna mamlaka na tuna taarifa kwamba, kundi jingine la vijana wanaomheshimu Khan, wanalisaka kwa udi na uvumba kundi lililotaka kumpora ‘mtu wao,” aliongeza mshirika huyo wa Khan.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Khan na nduguye walilazimishwa kushuka garini wakati mmoja wa majambazi alipomtishia Khan kwa kisu. 
Ndugu hao wakajisalimisha kwa kukimbia na kutoweka eneo la tukio, wakati tayari mashuhuda hao wamewasilisha maelezo yao polisi juu ya walichokiona.

No comments:

Post a Comment