Tangazo

Pages

Thursday, October 4, 2012

Sadiki momba na alen kamote kuzipiga mwisho wa mwezi


Bondia mwenye manjonjo,mbwembwe na vituko vingi ulingoni Sadiki Momba"kijotijoti". Amesema anamtaka Ramadhan Shauri(ambae ni bingwa waIBF Afrika)'.sio alen kamote wa tanga ambae ni bingwa wa Afrika mashariki anaetegemea kucheza nae tarehe 27 octoba 2012,pambano hilo linaloandaliwa na ally mwanzoa na kuratibiwa na bigright promotion katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese.
Sadiki momba anasema bondia anayemfikiria ni Ramadhan Shauri  na ni bingwa wa kupewa kwa kutengenezewa mazingira ,"shauri haniwezi na yeye mwenyewe anajua hata mapromota wakitokea wa kutukutanisha mie nakuwa tayari kwa gharama zozote lakini Mzazi kocha wa shauri hukataa au utaja dau kubwa la mamilioni ili promota akimbie,Shauri amecheza mapambano 13,kapigwa matatu,kadroo moja tisa kashnda wakati mie nimecheza mapambano kumi na nane(18) droo moja,nimepigwa moja na mudy matumla kwa kubebwa na yaliyobaki 16 yote nimeshinda hivyo mie nina rekodi nzuri ulingoni kuliko Shauri.sijapata tu nafasi ya hizo mechi za ubingwa lakini hao mabingwa wao wanaowapa mechi za kimataifa mie nimeshawapiga sana mpaka kuokolewa na refa au kufikishwa mahospitalini wakiwa hali mbaya kwa kipigo.njooni mumuangalie kamote nitakavyomfanya ndio maana simzungumzii sana najua nitampiga kirahisi sana akakate viuno vyake kwao tanga.
.Naomba promota yoyote ajitokeze kutuandalia mchezo kati yangu na shauri wasimtengenezee mazingira na vibonde,
Tunajua kocha Mzazi na mabondia wake wanaabudu uchawi hivyo nitawaomba chama kitakachosimamia mchezo kiwaruhusu waganga wao waroge mpaka ulingoni siku ya mchezo- nasema hivyo ili mzazi asiogope sana akubali kucheza na mimi kwa imani zake za kichawi.mimi nijiamini kwa mazoezi yangu na kipaji nilichonacho na nina uwezo wa kulifanyia taifa letu makubwa kama nitawezeshwa kwa kuandaliwa mapambano ya kimataifa na ya nje ya nchi, kwani hapa Tanzania karibu mabondia wote wa uzito wangu nimeshawamaliza,bado sijulikani kwa wakubwa kwa sababu sijapata mechi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment