Tangazo

Pages

Monday, October 22, 2012

TPBO, PST na TPBC ZATOA UFAFANUZI





Onesmo Ngowi
OKTOBA 22, 2012
Gazeti la Mwananchi ni moja ya magazeti yenye wasomaji wengi sana hapa Afrika ya Mashariki kutokana na uandishi wake uliobobea kwenye utafiti. Mara nyingi gazeti hili limekuwa linaibua ukweli kwenye masuala mengi yanayohusu jamii. Hili linalipa heshima pekee kama gazeti la watu na sio tu hapa Tanzania bali ni Afrika hata dunia nzima.
Kazi kubwa ya uandishi ni kuandika ukweli na ni muhimu kwanza ukafanyika utafiti ili ukweli wenyewe usije ukawaumiza wake ambao unataka kuwasaidia. Ni muhimu habari yenyewe inayoandikwa iwatendee haki wale wote unaowagusia.
Pamoja na heshima hii ya gazeti la Mwananchi tuna shaka na uandishi wa mwandishi mmoja anayeitwa Imani Makongoro ambaye anajaribu sana kujihesabu kama mwandishi mtaalam wa wasuala ya ngumi. Mwandishi huyu amekuwa anaandika habari ambazo hazina ukweli na hazikufanyiwa utafiti.
Aidha amekuwa anakurupuka kuandika habari ambazo haziwatendei haki wale anaowaandika kwa maana ya kuwahoji kwanza kabla ya kuandika kama yalivyo maadili kwa mwandishi yeyote aliyesomea kazi ya uandishi wa habari.
Pamoja na habari zake nyingi ambazo hazima kichwa wala miguu kuhusu tasnia ya ngumi, leo hii amekuja na habari (piece) inayosema “TPBO, PST na TPBC achene kuwadanganya mabondia wa Tanzania”.
Mwandishi huyu amedai kuwa TPBO, PST na TPBC vimekuwa vinawatengenezea mabondia wa Tanzania mikanda isiyo na maana ya heshima stahiki. Ameendelea kuorodhesha umbumbumbu wake kwa makala ndefu isiyo na kichwa wala miguu kuhusu mchezo wa ngumi za kulipwa. Hii ni hatari kubwa sana kwa mwandishi anayeliandikia gazeti linalioheshimiwa kama Mwananchi kuandika habari asizosijua.
Makongoro amekuwa na tabia ya kupekua sana kwenye internet na kudurufu habari zilizoandikwa na wengine huko kwa mtindo wa “copy and paste” au “bandua bandika” na huu umekuwa ndio mtindo wake wa uandishi wa habari siku zote! Ukisoma kwa uangalifu makala zake ni zile ambazo hazijafanyiwa utafiki ila ni za umbea wa juu juu tu!
Imani Makongoro kweli kafulia kwa maana hata hajui duniani kuna mashirikisho mangapi ya ngumi za kulipwa. Hajui hata sababu ni kwa nini mashirikisho, mabaraza au vyama vingapi vya ngumi za kulipwa vilianzishwa duniani.
Katika makala zangu za “Mchezo wa Ngumi, Taa inayozizima” na ambazo zinaendelea (niko kwenye sehemu ya kumi na nane) nimekuwa naeleza kwanini duniani kuna mabaraza, vyama au mashirikisho mengi ya ngumi za kulipwa na faida zake ni nini!
Pengine Imani Makongoro huwa hasomi makala hizi zilizoandikwa na mimi kama mtaalam wa masumbwi nisiye mumunya maneno. Nasema mimi ni mtaalam kwa kuwa nimecheza ngumi za ridhaa, kulipwa na sasa naongoza taasisi zinazoheshimiwa duniani ambazo Imani Makongoro mwenyewe hazijui.
Kwa ufupi mimi ni Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Rais wa Chama Cha Ngumi Za KUlipwa Afrika ya mashariki na Kati (ECAPBA), Mkurugenzi wa Baraza La Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) na Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi.
Hizi sio taasisi ndogo na mimi nimekuwa "Mtu wa Kwanza kutoka bara la Afrika" kuweza kufikia katika nafasi niliyo nayo kwa sasa na inaipa nchi yangu Tanzania heshima kubwa sana duniani.
Ndiyo maana mabondia kama kika Francis Cheka, Rajabu Maoja, Magoma Shaaban (Marehemu), Rogers Mtagwa, Bakari Mambea, Thomas Mashali, Ramadhani Shauri, Manda Maugo, Mbwana matumla, Rashid Matumla, Joseph Marwa, Maneno Oswald, na wengine wengi wameweza kupata nafasi za kupigania matuzo mbalimbali ya mashirikisho haya!
Lakini kwenye kumbukumbu za Imani Makongoro yete ngumi Tanzania anamjua tu Rashid Matumla wengine kwake hawana maana yoyote!
Inanipa taabu kubwa kujaribu kufikiria ni sababu gani haswa iliyomfanya Imani Makongoro kuandika habari (piece) inayowadhalilisha viongozi wa TPBO, PST, TPBC na wadau wote wa ngumi za kulipwa Tanzania.
Kinachoweza kuelezwa ni labda ametumwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wanamtumia kuchafua TPBO, PST na TPBC. Mabwana au mabibi hawa waliomtuma Imani Makongoro wanasahau jambo moja kubwa kuwa “Ni Michezo wa Ngumi za Kulipwa pekee unaoitangaza Tanzania vizuri katika medani ya michezo duniani” kwa sasa.
Imani Makongozro alinipigia simu jana na kuniuliza ni kwanini simpatii Francis Cheka pesa za mazoezi na nikamwambiwa kuwa sheria ya mikataba ya ngumi za kulipwa haziruhusu kinachoitwa pesa za awali (Advance Payments)!!
Lakini kwa watu wa aina ya Imani Makongoro hawaelewi lolote utakalowaambia. Anachojua ni kukimbilia na kuandika habari zisizo na kichwa wala miguu!
Nilimwambia kuwa Francis Cheka hana meneja na kama anadai kuwa ana meneja basi amwonyeshe mkataba wake wa meneja!
Lakini kama nilivyokwisha sema hapo juu, Imani Makongoro hawezi kusikia au kuona hili badala yake amejaa mahasa za kukimbilia kuandika habari ambazo hazina kichwa wala miguu ili kuwadhalilisha wadau wanaohesimika katika medani ya ngumi za kulipwa!
Sisi TPBO, PST na TPBC hatuna magazeti ya kumwandika Imani Makongoro. Yeye na mhariri wake wa michezo wa gazeti la Mwananchi wala kila sababu za kuringa kwa kuwa wanalo jukwaa (forum) ya kutudhalilisha na kutuharibia heshima yetu kwa jamii.
Mahali pekee tunapoweza kukutana naye ili aweze kuthibitisha tuhuma alizozitoa kwetu ni “MAHAKAMANI PEKE YAKE!
Sisi TPBC tutakwenda mahakamani ili Imani Makongoro athibitishe tuhuma zake kuhusu "udanganyifu tunaoufanya kwa mabondia wa Kitanzania".
Imeandikwa na:
Onesmo Ngowi
Rais,
KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA (TPBC)
Chama Cha Ngumi za Kulipwa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)
Barala la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC)
IBF Africa, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi

No comments:

Post a Comment