OGANIZESHENI ya Ngumi za Kulipwa
Tanzania (TPBO) imesema kama promota wa ngumi
nchini, Siraju Kaike (Pichanihatowalipa mabondia chipukizi, watalazimika kumfungia leseni
yake kwa muda au mwaka mzima.
Kaike anadaiwa kuwafanyia
kitendo ambacho si cha kiungwana mabondia chipukizi Issa Omar na Mwaite Juma
kwa kuwapambanisha Julai 15 mwaka huu kwa makubaliano ya kuwalipa na baadae
kutowalipa.
Juni 25 mwaka huu Kaike
aliwasainisha mkataba mbele ya Katibu Mkuu wa Ngumi za Kulipwa Tanzania ,
Ibrahim Kamwe, kuwa Omar kucheza na Ramadhan Kumbele kwa malipo ya sh. 80,000.
Akizungumza Dar es Salaam leo,
Katibu Mkuu wa TPBO, Ibrahim Kamwe alisema uongozi wa oganizesheni hiyo
wamekuwa wakimsihi kila siku awalipe mabondia hao na kukubali, lakini
mabondia wakienda kwake
anawapiga kalenda.
Alisema kitendo hicho si cha
kiungwana hivyo wamewashauri mabondia hao waende mahakamani ili waweze kupata
haki yao na kuwapa
nguvu wao ya kumsimamishia eseni yake kwa muda ili awe na adabu.
“Hatuna haja ya sisi tuseme
kwamba tunamfungia, ukizingatia kiasi chenyewe ni kidogo na Kaike ana uwezo wa
kulipa, nashangaa kwa nini anasubiri mpaka aambiwe wakati ni jukumu lake kuwalipa
mabondia, anabaki kuwapiga kalenda tu, mara njoeni kesho mara kesho kutwa”
alisema Kamwe.
Alipotafutwa
Kaike kwa kupitia simu yake ya mkononi, ilikuwa inaita bila kupokelewa na
baadae ikazimwa kabisa.
No comments:
Post a Comment