Tangazo

Pages

Monday, October 1, 2012

BFT YAMTAKA PROMOTA WA NGUMI, KAIKE SIRAJU KUWALIPA MABONDIA



Na Elizabeth John
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa (BFT), Makore Mashaga amemtaka Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Kaike Siraju kuwalipa mabondia fedha zao kama walivyokubaliana kwa lengo la kuendeleza mchezo huo hapa nchini.
Kaike anadaiwa kuwafanyia kitendo ambacho si cha kiungwana mabondia chipukizi Issa Omar na Mwaite Juma kwa kuwapambanisha Julai 15 mwaka huu kwa makubaliano ya kuwalipa na baadae kutowalipa.
Juni 25 mwaka huu Kaike aliwasainisha mkataba mbele ya Katibu Mkuu wa Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Ibrahim Kamwe kuwa Omar kucheza na Ramadhan Kumbele kwa malipo ya sh. 80,000.

Pia Kaike alifanya hivyo kwa bondia, Juma aliyecheza na Anthony Mathias, ambapo vijana hao walicheza na hawakulipwa na promota huyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mashaga amesema kuwa kwa kufanya hivyo atawakatisha tamaa mabondia wakiwa bado hawajawa na uzoefu katika mchezo huo, hivyo anamshauri awalipe mapema.
Alisema kuwa mambo yaliyofanywa na promota huyo si ya kiungwana ni kuwavunja moyo mabondia chipukizi, kudumaza ngumi na kufanya mchezo wa ngumi uonekane ni mchezo wa wahuni kwa vitendo vya kihuni kama hivi.

No comments:

Post a Comment