Tangazo

Pages

Tuesday, October 30, 2012

Tamasha Kuhamasisha Ngumi Mtwara


 Bakari dunda akivishwa mkanda na mbunge wa mtwara baada ya kuchukuwa ubingwa huo katika ukumbi wa makonde
 
Tamasha la kuhamasisha masumbwi mkoani mtwara lilimalizika kwa mafanikio mazuri kwa watu kuitikia na kukubali mapambano mengine mengi ya ngumi kufanyika mkoani humo.
katika tamasha hilo lililosindikizwa na pambano la ubingwa wa taifa la uzito wa unyoya kati ya Bakari mohamed'dunda wa blackmamba ya mtwara alimshinda abdala seleman wa dar es salaam,
Nae mkongwe Rashid 'snake man" matumla alimshinda kiaina yake bondia Patrick amote wa kenya katika pambano ambalo liliwasimua sana mashabiki na kuwafanya kushindwa kukaa vitini muda wote wa pambano na hasa pale mkenya alipokwenda chini kwa konde zito lililotupwa na matumla baada ya kukwepa ngumi na kutupa hilo konde kwa kushtukiza,mwanzo alianza taratibu na kuonekana kama mchovu kutokana na kitambi alichonacho na kujikwaakwaa ulingoni lakini kadiri muda ulivyosogea ndivyo alivyobadirika na kuonekana mzuri zaidi.
pambano jingine lililowaacha hoi wapenzi wa mtwara na kukaa kimyaaa na kuduwaa kwa mshangao ni la haruna mnyalukolo wa dar na ashraf wa blacmamba kwani ngumi zilipoanza tu walianza kwa nguvu sana na kutupiana makonde mfululizo yaliyomuingia kila mmoja na kupelekana chini kwa zamu na wote walivimba nyuso na kutokwa na damu baada ya kupasukapasuka mpaka mwishowe ashraf spidi na uvumilivu ulipomshinda na kukubali kuliachia pambano kwa kukataa kurudi ulingoni raundi ya nne pambano lilikuwa la raundi sita.

No comments:

Post a Comment