Tangazo

Pages

Thursday, October 4, 2012

BONDIA BINGWA WA TAIFA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI




Bondia bingwa wa taifa wa kilo 59 toka mkoa wa Tanga Said Mundi "smart punch"amefiwa na baba yake mzazi mzee Abdulrahman mbaraka nyumbani kwake Zahrau mkoani Tanga.kifo hicho kilitokea jioni ya jana muda mchache kabla ya mpira wa simba na yanga haujaanza,sababu ya kifo chake cha ghafla inaelezwa ni shinikizo la damu lilitokea kwa muda mfupi na kujaribu kumpeleka katika hospital bombo na kufia njiani, kwa maelezo ya said mundi mwenyewe kwa  Ibrahim Kamwe"bigright" ni kuwa baba yake hapo awali hakuwa na ugonjwa huo umekuja ghafla na umemchukua baba. Wanategemea kuzika leo jioni.
Said Mundi anaetegemea kupanda ulingoni tarehe 26 octoba 2012 kuzichapa na jumanne Mohamed raundi kumi kugombania ubingwa wa PST katika uwanja wa mkwakwani-Tanga.viongozi wote wa masumbwi kwa pamoja tupo pamoja na said mundi katika wakati huu mgumu uliompata na tunashirikiana katika shughuli zima za kufanikisha msiba huu.Mungu ailaze roho ya mzee Abdi Mbaraka mundi peponi - amin

No comments:

Post a Comment