Kocha Kondo nassoro akimwelekeza
bondia chipukizi Zainabu Mhamila (Ikota) huku nyuma akielekezwa jinsi ya
kutembea na kocha Habibu Kinyogoli wakati wa mazoezi yanayoendelea
katika kambi ya Ilala Dar es Salaam Picha na
MWALIMU Julius Kambarage Nyerere kipindi yuko madarakani,
alipenda michezo kuanzia mashuleni hadi kwenye makampuni na mashirika
mbalimbali hapa nchini, ingawa alikuwa akipenda mchezo wa bao.
Aliweka sera bora ya michezo na kufanikisha
kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1967 na kutoa fursa zaidi kwa wenye
vipaji kuvionyesha.
Kwa mujibu wa bondia mahiri wa Ngumi hapa
nchini, Habibu Ally Kinyogoli (64), Nyerere alifanikisha wachezaji wa Tanzania
kuitangaza zaidi nchi yetu na kufanya vizuri kutokana na mazingira bora
yaliyokuwako wakati huo.
Kinyogoli ni mwanachama wa Mabingwa wa Ligi Kuu
Tanzania bara, Simba lakini hahudhurii michezo ya timu hiyo, mapenzi yake
yanabaki kwenye ngumi.
Nyota yake ya michezo ilianzia shuleni,
Manerumango Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mwaka 1958, alicheza soka, ngumi na
riadha, aliendelea na mchezo wa ngumi kwa sababu ndio ulikuwa ndani ya damu
yake, michezo mingine ilimshinda kwa sababu ya hasira za baadhi ya wachezaji
pindi zinapotokea rafu.
Kinyongoli wakati alipokuwa akicheza, alikuwa
pia akitoa mafunzo kwa wenzake, mwaka 1966, katika klabu ya Magomeni Centre
yalipo makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni alimfunza Majuto Mahavu ambaye
baadae alikuwa tishio kwenye timu ya Taifa.
Mwaka 1970 alijitosa rasmi kwenye ngumi baada ya
kuvutiwa na Titus Simba aliyeiletea medali ya kwanza Tanzania ya Jumuiya ya
Madola iliyofanyika Scotland, ndipo na yeye akaongeza ufanisi zaidi katika
mchezo huo.
Mwaka 1971 aliajiriwa kiwanda cha Bora baada ya
kuonesha umahiri katika mchezo huo, akafanikiwa kumfudinsha ngumi, Zakaria
Yombayomba, mwaka 1973 aliasisi klabu ya ngumi ya Urafiki akawaibua akina
Charles Mhilu ‘Spinks’, Habibu Mzungu, Lazaro Makarious, Kwelu Msinjili na
wengineo.
Mwaka 1972 alishiriki mashindano ya Olimpiki,
Munich Ujerumani walikwenda na akina Titus Simba, Robert Mwakosye, Bakari
Suleimani ‘Match Maker’, Said Tambwe katika mashindano hayo, mwanariadha Clever
Kamanga aliipa Tanzania medali ya shaba kwa mbio za umbali za mita 400.
Katika mashindano hayo, Kinyogoli alifanya
vibaya baada ya kukatika kwa mshipa wa mkono wa kulia katika mazoezi nchini
humo, mchezo wa kwanza wa Olimpiki alishinda kwa pointi nyingi dhidi ya
Mcambodia, mchezo wa pili alipoteza pambano baada ya kujitonesha mkono wake na
damu zikatoka nyingi.
Maumivu hayo hakuyaona hadi, Profesa Philemon
Sarungi wakati huo alikuwa akisoma nchini humo, alijitolea kuisaidia timu hiyo.
Mwaka 1973 alishiriki All Africa Games jijini
Lagos Nigeria akarejea na medali ya fedha na kuchaguliwa kwenye timu ya Afrika
iliyoshiriki Inter-Continental
iliyofanyika Mexico , uteuzi huo pia uliwahusu pia akina Jacob Mussa,
Bakari Suleimani, Titus Simba na Mbaraka Mkanga wakati katika soka Tanzania
iliwakilishwa na akina Maulid Dilunga, Abdallah Kibadeni na Kitwana Manara.
Mwaka 1974 alisisi klabu ya Simba ambayo kipindi
hicho ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Abubakar Mwilima baada ya kuchana
mkataba wa Bora, baada ya uongozi mpya wa kiwanda hicho kutokupenda michezo,
akaondoka na wenzake wote aliokuwa nao kiwandani hapo kama Bakari Suleiman
‘Match Maker’, YombaYomba na wengineo.
1976 akiwa kwenye kambi ya maandalizi ya
Olimpiki alitangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa, mwaka 1978 akaanzisha
klabu za watoto wadogo ya Relwe na kuendelea na Simba, Simba wakachipukia akina
Rashid Matumla, Iraq Hudu Mkumwena,Rajabu Mhamila 'Super D' Shabani Mhamila 'Star Boy, Remmy Ngabo, Joseph Marwa,mohamedi Chipota na wengineo.
Hivi sasa, Kinyogoli anafundisha klabu ya
Amana ya Ilala akisaidiwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' kocha Mohamedi Chipota, Kondo Nassoro na Sako Mtulya na akiendelea na Simba pia akiwa na changamoto nyingi ambazo
ni uwezeshwaji wake kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sababu ameutengeneza mchezo
huo tangu alipokuwa akifanya kazi na alitumia gharama zake lakini sasa, kazi
hafanyi.
No comments:
Post a Comment