Tangazo

Pages

Saturday, October 13, 2012

MGANDA AINGIA KUMKABILI MASHALI



Bingwa wa Uganda MEDY SEBYALA MGANDA AINGIA KUMKABILI MASHALIameingia nchini  kwa ajili ya pambano lao na Bingwa wa taifa wa Tanzania THOMAS MASHALI ,katika pambano la Ubingwa wa Africa mashariki na kati litakalo fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel siku ya jumapili 14/10/2012.
Akizungumzia pambano hilo katibu mkuu msaidizi bw said chaku ambae alikuwa pamoja na rais wa TPBO bw Yasin abdallah wakati wa mapokezi ya bondia huyo aliefatana na mwalimu wake tokea Uganda,ni kuwa wamefika salama na wapo katika hali nzuri ya ushindani na muda wote mganda huyo Med sebyala alionekana mwenye kujiamini na kujitapa kuwa amekuja kumuangamiza toto tukutu au simba asiyefugika-Thomas mashali na kuondoka na mkanda wa ubingwa kwao.
Pambano hilo la ubingwa wa afrika mashariki litasimamiwa na organization ya ngumi za kulipwa nchini-TPBO chini ya yasin Abdallah'ustadh' na mabondia hao watapima uzito na afya kiujumla saa tatu asubuhi siku ya jumamosi 13/10/2012 hapohapo friends corner hotel na zoezi zima la upimaji litasimamiwa na katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim Kamwe na dr Donald Madono pia kutakuwepo na mapambano zaidi ya sita ya utangulizimapambano manne ya utangulizi ya siku hiyo ambapo Abdul Awilo atazichapa na Shedrack Juma, Selemani Shaaban atavaana na Hamisi Mohamed huku Jonas Segu akinyukana na Ibrahim Class wakati Charles Mashali atatwangana na Teacher Aaron
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali
 

No comments:

Post a Comment