Tangazo

Pages

Tuesday, October 9, 2012

IBF YAIDHINISHA MAPAMBANO MANNE YA UBINGWA





 Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) zimeidhinisha kufanyika kwa mapambano manne ya ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Ghuba ya Uarabu na Uajemi jijini Dar-Es-Salaam mwezi wa Novemba mwaka huu.
Mapambanohayoambayonimaraya kwanza kufanyika katika ukanda huu wa dunia yatakuwa yanashirikisha mabondia kutoka Misri, Kenya, na Tanzania na yatarushwa live na televisheni za Tanzania, Kenya naMisri.
Kufanyika kwa mapambano haya kumewezekana baada ya makapuni manne kutoka Tanzania na Misri kuungana na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na kuanzisha programu ya mwaka mmoja itakayoanza Novemba mwaka huu hadi Novemba mwakani.
Katikaprogramuhiimakampunihayapamojana IBF yataandaa mapambano kila baada ya mwezi mmoja Novemba, Januari, Machi, Mei, Julai, Septemba na Novemba mwakani.
Raiswa IBF katikabara la Afrika, Masharikiya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi Onesmo Ngowi aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Jambo Concept inayomiliki vyombo vya habari vikiwamo gazeti la Jambo Leo, Tanzanite Sports Promotion Management, Kitwe General Traders yote ya Tanzania na Louaa Boxing Promotion ya Misri.
Katikamapambanohayo, mabondia Alphonce Joseph Mchumiatumbo atapambana na bondia wa Misri anayeishi nchini Marekani, Manzur Ali katika uzito wajuu (Heavyweight) kugombania mkanda wa IBF Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi na Afrika.
Bondia wa Misri, Mohammed Metually, ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na Baraza la Ngumi la Dunia (WBC) atapambana na bondia Nofart Emilio, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Mashariki ya Kati, Ghubaya Uarabu na Uajemi na Afrika katika uzito wa Bantam.
Naye bondia bora wa TASWA mwaka 2011 Nassibu Ramadhani, atachuana vikali na bondia asiyepigika, Nick Otieno, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi na Afrika katika uzito wa Super Flyweight.
Bondia anayepanda chati kwa kasi Haji Juma, kutoka viunga vya jiji la Tanga atapambana na bondia Twalib Mubiru, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Afrika katika uzito wa bantam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na bara la Afrika kuwa na mapambano mengi ya ubingwa wa IBF kwa usiku mmoja.
Mabalozi wengi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania, wageni wengi wanaoishi Tanzania na wadau wengi wa ngumi kutoka Misri, Kenya, Uganda na chi za jirani watahudhuria mapambano haya kwa maelfu.
Imetumwana:
 Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais,
IBF Africa, Masharikiya Kati, GhubayaUarabunaUajemi

No comments:

Post a Comment