Wednesday, October 24, 2012
TPBO YAMPONGEZA IMANI MAKONGORO -MWANDISHI
MWANADADA IMANI MAKONGORO KATIKA MAONI NA UCHAMBUZI ,ALIANDIKA TPBO ,PST,TPBC, ACHENI KUWADANGANYA MABONDIA.
KATIKA MAKALA HIYO BAADHI YA MAMBO ALIYOYAANDIKA YALIKOSOA UPIGANISHAJI WA MABONDIA WATANZANIA KWA WATANZANIA NA KUYAITA MAPAMBANO HAYO NI YA UBINGWA WA DUNIA ,PIA ALIHIJI KWAMBA KAMA FRANCIS CHEKA ATAITWA BINGWA WA DUNIA JE AKINA MANNY PAQUIAO WAITWEJE? BINTI HUYU PIA ALILITAKA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA [BMT] KUVIFUNGIA VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA AMBAVYO VITATHIBITIKA KUWADANGASNYA MABONDIA WA KULIPWA WA TANZANIA.
TPBO TUNAHESHIMU SANA UHURU WA MWANDISHI HUYU BINT WA KUTOWA MAONI YAKE KWA MUJIBU WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA.
ISIPOKUWA TPBO INASIKITISHWA SANA NA JINSI MWANDISHI HUYU ALIVYOITUHUMU TPBO KATIKA SUALA ZIMA ALILOLIONGELEA.
KWANI PAMOJA NA KWAMBA RAIS WA TPBO YASSIN ABDALLAH-USTAADH ,KUWA MWAKILISHI WA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA DUNIANI LENYE MAKAO MAKUU NCHINI MAREKANI HAPA TANZANIA ,TPBO HAIJAWAHI KUSIMAMIA PAMBANO LOLOTE LA UBINGWA WA DUNIA TANGU ISAJILIWE HAPO JULAI 2007.
BALI TPBO IMEJIHUSISHA ZAIDI KUSIMAMIA MAPAMBANO YA NDANI YA TANZANIA KWA WINGI SANA HUKU IKIAMINI KWAMBA INAWAANDAA MABONDIA VIJANA CHIPUKIZI AMBAO WANAWEZA WAKALIWAKILSHA TAIFA LA TANZANIA KWA UHAKIKA NA HATIMAYE KUWEZA KUIGA MFANO AMBAO ULIONESHWA NA AKINA RASHID MATUMLA.
TPBO HAINA UGOMVI NA MWANDISHI WA MAKALA YALE BINT IMANI MAKONGORO KWA KUAMINI KABISA KUWA ANAJITAHIDI SANA KUUELEWESHA UMMA WA WATANZANIA UHALISIA WA MAWAZO ALIYONAYO KAMA MUANDISHI.
TUNAMPONGEZA SANA MWANDISHI HUYU KWA KUTOKUWA MWOGA WA KUELEZEA MAONI YAKE BILA UFICHO, TPBO IKO TAYARI KUMSAIDIA MWANDISHI HUYU -IMANI MAKONGORO ILI AWEZE KUUANDIKIA VIZURI MCHEZO HUU WA NGUMI ZA KULIPWA.
TPBO DAIMA INAFANYA KAZI ZAKE KWA UFANISI KUTOKANA NA KUIRUHUSU JAMII YA WATANZANIA KUWASEMA VYOVYOTE WAPENDAVYO ,HUKU IKIAMINI KABISA NDIYO NJIA MUAFAKA YA KUIFANYA TPBO IJIREKEBISHE KAMA YAPO MAKOSA.
NAPENDA NIMSAIDIE KIDOGO TU BINTI HUYU SHUJAA MWANDISHI KWAMBA SIYO KOSA KABISA KWA MUJIBU WA KANUNI ZA NGUMI ZA KULIPWA DUNIANI KUWAPIGANISHA MABONDIA WA KUTOKA NCHI MOJA KTK PAMBANO LA UBINGWA WA DUNIA ILI MURADI CHAMA HUSIKA KIMERIDHIKA NA VIWANGO VYA MABONDIA HAO NA KIKATOWA KIBALI CHA KUWAPAMBANISHA.
OMBI KWA WAANDISHI WOTE-;
JARIBUNI KUTUULIZA MAMBO AMBAYO MNAHISI YANAWATATIZA KUHUSU MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA, KWANI IWAPO WATANZANIA WATAENDELEA KUSOMA HABARI AMBAZO HAZINA UTAFITI WA KINA IPO HATARI HATA HAWA MAPROMOTA WALIOPO WANAWEZA KUACHA KUWASAIDIA MABONDIA KWA KUWAANDALIA MAPAMBANO ,NA MATOKEO YAKE MABONDIA MATAJIINGIZA KATIKA VITENDO VYA UHALIFU ILI WAWEZE KUJIKIMU KIMAISHA ,NA PIA TUNAVITEGEMEA SANA VYOMBO VYENU KWA KUWAHAMASISHA WEMYE UWEZO KIPESA KUWASAIDIA MABONDIA KWA KUANDAA MAPAMBANO YA MARA KWA MARA.
NARUDIA TENA KUMPONGEZA MWANADADA IMANI MAKONGORO KWA UJASIRI WAKE ,
IMEANDIKWA NAMI;-
YASSIN ABDALLAH -USTAADH
RAIS -TPBO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment