Tangazo

Pages

Monday, October 1, 2012

AMIR KHAN KUMVAA CARLOS MOLINA DESEMBA


 
 
LONDON, England
 BONDIA Mwingereza Amir Khan anatarajia kurejea ulingoni Desemba mwaka huu, kupigana na Carlos Molina – huku akiwa chini ya ukufunzi wa kocha mpya Virgil Hunter anayemnoa kwa sasa.

Khan, 25, analichukulia pambano hilo kama hatua moja mbele kuelekea mchuano anaouwania wa kupimana ubavu na bondia kama Floyd Mayweather.
 
Bondia huyo mzaliwa wa jiji la Bolton, hivi karibuni alimfukuza kazi mkufunzi wake Freddie Roach, kufuatia kichapo kutoka kwa Danny Garcia Julai mwaka huu, akidai kocha huyo hakuwa na muda wa kutosha kumnoa, kutokana na majukumu mengine.
Mkali huyu kwa sasa yuko kwenye mazoezi makali chini Hunter nje ya ‘gym’ yake huko Hayward, California, tayari kumvaa Molina.
Khan alisema: “Kusema kweli nimeridhishwa mno Virgil kuwa mkufunzi wangu mpya. Kila mmoja miongoni mwa mabondia wanatambua uzoefu, ufundi na mafanikio ya Virgil aliyopata miaka michache iliyopita.
“Naangalia mbele kuanza kambi yangu mpya kwa bidii na kufanya baadhi ya mambo muhimu nikiwa chini yake. Kuwa na Virgil katika kona yangu ulingoni, najua kwamba itanirejesha katika kilele cha ubora wangu katika uzani wa ‘Light-welterweight’.

No comments:

Post a Comment