Tangazo

Pages

Wednesday, March 27, 2013

Ngumi Taifa kuanza Aprili mwishoni



Katibu Mkuu, BFT, Makore Mashaga
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya Taifa kwa mchezo wa ngumi za ridhaa yanatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi ujao baada ya kufanyika kwa mashindano ya ngazi za chini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Mashaga Makore, alisema kuwa washindi watakaopatikana katika ngazi za chini ndiyo watakaoingia kwenye mashindano ya Taifa.
Amesema kuwa kwa sasa mashindano hayo yataanza katika ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa baada ya hapo washindi watashiriki mashindano ya Kanda ambapo Kanda nne zimetengwa kwa ajili ya mashindano hayo kabla ya Taifa.
“Mwaka huu tumefanya tofauti na miaka iliyopita ambapo sasa tumeanzia ngazi za chini ili kuwapata mwachezaji ambao wataliwakilisha taifa kwenye michuano mbalimbali.
“Kabla hatujaanza mashindano ya Taifa kutakuwepo na mashindano ya Kanda ambayo yatashirikisha mabondia au timu zilizofanya vizuri ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa, hao ndiyo watakuwa na sifa ya kushiriki ngazi ya Taifa,” almesema Makore.
Almesema katika Kalenda ya BFT ya mwaka huu, kuna mabadiriko mbalimbali ambayo yanamtaka kila mjumbe wa Kamati ya Utendaji kuwajibika kulingana na majukumu aliyopewa.
“Mwanzo shughuli zote zilikuwa zinafanywa na uongozi wa BFT wakati kuna kamati zake, lakini hivi kuna tofauti katika Kalenda ambapo kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa maagizo ya kamati yake inavyomtaka afanye ili kukuza na kuendeleza mchezo huu,” amesema Makore.

No comments:

Post a Comment