Tangazo

Pages

Thursday, March 28, 2013

MABONDIA ALBINUS NA HERBERT KUPIMA UZITO LEO


Herbert_Quartey 
Herbert Quartey wa Ghana
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13daf8f51fb8597e&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_heti8ztf0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1364464445455&sads=Yj0MVU1fi9izisR_b2L-O8m-_Lk&sadssc=1 
Mabondia kinda Albinus Felesianu wa Namibia na Herbert Quartey wa Ghana wanaogombea ubingwa wa dunia katika uzito wa bantam kwa vijana kesho, watapima uzito leo asubuhi katika ofisi za bodi ya mieleka na ngumi ya Namibia zilizoko katika eneo la katikati ya jiji la Windhoek, Namibia.
Mpambano huo unategemewa kuwa na kila aina na hamasa kutokana na mabondia wote kuwa wajuzi wa kuzipiga katika maisha yao mpaka sasa. Mshindi wa mkanda huu ndiye atakayekuwa bingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa bantam. 
Wananchi wengi wa Namibia na kutoka katika nchi jirani kama Afrika ya Kusini, Zambia, Botswana na Angola wameshaingia katika jiji la Windhoek na tayari hoteli na nyumba nyingi za kulala wageni tayari zimeshajaa. 
Mpambano huu utafanyika katika hoteli maarufu ya Windhoek Country Club and Casino mahali ambapo ni wiki moja tu iliyopita kuliwako na hekaheka nyingine ya kugombea mkanda wa IBF wa kimataifa kati ya mabondia Immanuel“Prince” Naidjala (Namibia) na Lesley Sekotswe (Botswana) ambao walitoka sare. 
Mpambano huu utasimamiwa na Rais wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye ni wiki iliyopita tu alikuweko tena mahali hapo kusimamia mpambano mwingine wa IBF. Rais Ngowi anaingia nchini Namibia leo akitokea nchini Ghana ambako alikuwa anasimamia mpambano wa ubingwa wa Afrika kati ya Frederick Lawson na Isaac Sowah wote wa Ghana.

No comments:

Post a Comment