Tangazo

Pages

Friday, March 29, 2013

COSMAS KIBUGA KUZICHAPA NA SWEET KALUU JUMALIPILI HII




Bondia mwenye makeke mengi na asiyekubali kushindwa ulingoni na , Cosmas Kibuga, anatarajia kupanda ulingoni siku ya jumapili wiki hii katika ukumbi wa Texas Manzese, kuzipiga na bondia mkongwe, Sweet Kalulu, katika pambano la kirafiki la kusherehekea  Pasaka. 
Akilizungumzia pambano hilo muandaaji wa mchezo huo, Miraji Msusa, alisema “burudani yetu ni kuangalia ngumi na kushangilia na najua ngumi nzuri zipo katika hawa mabondia wasio na majina na wenye upinzani mkali ,nikaonelea lazima katika sikukuu hii ya pasaka tusiiache ipite hivihivi bila kupata starehe yetu,  kusubiri mpaka tarehe 7 april kwenye pambano kubwa la pale ccm mwinjuma-mwanayamala  ni mbali, Nikaafikiana na cosmas kibuga na sweet kalulu ambao ni wapinzani mitaani wamalizie kiu yao hiyo''. alisema

Thursday, March 28, 2013

BigRight YAWEKA MIKAKATI YA UBINGWA

371.JPG
Kampuni  changa ya Bigright Promotion inaanzisha mkakati wa kuwapiganisha mabondia  kwa ajili ya kugombania mikanda au kutetea mikanda yao isipotee.Ibrahim kamwe kiongozi wa kampuni hiyo alisema ” Tutaanzia kwa kuandaa ubingwa wa mapambano ya uzito mdogo kabisa yaani light fly weight,baadae tunawaandalia fly weight na super fly  ,bantam …. .. ..mpaka heavy weight ,hiyo itawasaidia mabondia kupata mapambano ya mara kwa mara na kuwapatia kipato kidogo kwa ajira walioichagua inayoambatana na utambulishaji wa kimataifa kwa nchi yetu,kwani mchezo wa ngumi ni mchezo  mmojawapo unaoutangaza na kuipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa,bila ya watanzania wengi kulifahamu hilo ,hivyo kukosa usaidizi mzuri toka serikalini na taasisi binafsi tofauti na baadhi ya nchi za wenzetu zinazopenda na kuithamini michezo, Nchi nyingi zinatangazika  kupitia  michezo hadi sisi tunazifahamu na kuzitembelea  au kuwa na shauku ya kutaka kuzitembelea, wakati uwezo huo wa kufanya vizuri  tunao lakini hatusaidiwi kujinyanyua wala kuwa na sehemu ya kueleweka kwamba hii ni kwa ajili ya ngumi (ulingo wa kisasa na ukumbi wa uhakika),na wakati wadau wa mchezo huu tunanung`unika na kuhaha kutafuta wadhamini  nasi tujikwamue tokakatika hali tuliyonayo, kuna wengine wasio wastaarabu  watataka kuchukua nafasi hii kufanya ubadhilifu dhidi ya wanaosaidia-hii sio njema  na inadumaza michezo.
Kwa mfano mashindano yaliyo andaliwa na bigright tarehe 7 april mwananyamala hayana udhamini wala ufadhili wowote hivyo yanaendeshwa katika hali ya ugumu ili vijana nao wapate kucheza kuliko kufanya mazoezi ya muda mrefu bila mashindano hivyo kuwasababisha baadhi ya mabondia kukata tama na kuacha ngumi au kijiingiza katika vitendo vya ukabaji jambo ambalo sio jema na laweza kuepukika kwa kuwaandalia mashindano kama haya na ili azma yetu ya kuyafanya yaendelee yatubidi tushirikiane kwa kushawishi wafadhili, wadhamini au wapenda mchezo wenye uwezo kidogo wawe wanatuwezesha japo kidogo walichonacho ili nasi tuwe tunaongeza nguvu ya kupigania michezo isidorole,  mipango ikienda kama tulivyopanga tunategemea kila mwezi kuwashindanisha kugombania ubingwa na kila mwezi wa 12 kunakuwa na ligi ya mabingwa na kumzawadia mshindi  kitu ambacho atakuwa anakikumbuka katika maisha yake,hivyo  kwa alie tayari na mwenye mapenzi na maendeleo ya michezo tunaomba mchango wako uwe wa vifaa kama gloves,bandages,ballguard,headguard,gumshield,chakula ,nauli,ulingo na mengineyo mengi tu sijayaorodhesha,msitutenge na uwezo wetu mdogo tusaidiane
 
IBRAHIM ABBAS KAMWE

MABONDIA ALBINUS NA HERBERT KUPIMA UZITO LEO


Herbert_Quartey 
Herbert Quartey wa Ghana
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13daf8f51fb8597e&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_heti8ztf0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1364464445455&sads=Yj0MVU1fi9izisR_b2L-O8m-_Lk&sadssc=1 
Mabondia kinda Albinus Felesianu wa Namibia na Herbert Quartey wa Ghana wanaogombea ubingwa wa dunia katika uzito wa bantam kwa vijana kesho, watapima uzito leo asubuhi katika ofisi za bodi ya mieleka na ngumi ya Namibia zilizoko katika eneo la katikati ya jiji la Windhoek, Namibia.
Mpambano huo unategemewa kuwa na kila aina na hamasa kutokana na mabondia wote kuwa wajuzi wa kuzipiga katika maisha yao mpaka sasa. Mshindi wa mkanda huu ndiye atakayekuwa bingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa bantam. 
Wananchi wengi wa Namibia na kutoka katika nchi jirani kama Afrika ya Kusini, Zambia, Botswana na Angola wameshaingia katika jiji la Windhoek na tayari hoteli na nyumba nyingi za kulala wageni tayari zimeshajaa. 
Mpambano huu utafanyika katika hoteli maarufu ya Windhoek Country Club and Casino mahali ambapo ni wiki moja tu iliyopita kuliwako na hekaheka nyingine ya kugombea mkanda wa IBF wa kimataifa kati ya mabondia Immanuel“Prince” Naidjala (Namibia) na Lesley Sekotswe (Botswana) ambao walitoka sare. 
Mpambano huu utasimamiwa na Rais wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye ni wiki iliyopita tu alikuweko tena mahali hapo kusimamia mpambano mwingine wa IBF. Rais Ngowi anaingia nchini Namibia leo akitokea nchini Ghana ambako alikuwa anasimamia mpambano wa ubingwa wa Afrika kati ya Frederick Lawson na Isaac Sowah wote wa Ghana.

Wednesday, March 27, 2013

Ngumi Taifa kuanza Aprili mwishoni



Katibu Mkuu, BFT, Makore Mashaga
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya Taifa kwa mchezo wa ngumi za ridhaa yanatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi ujao baada ya kufanyika kwa mashindano ya ngazi za chini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Mashaga Makore, alisema kuwa washindi watakaopatikana katika ngazi za chini ndiyo watakaoingia kwenye mashindano ya Taifa.
Amesema kuwa kwa sasa mashindano hayo yataanza katika ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa baada ya hapo washindi watashiriki mashindano ya Kanda ambapo Kanda nne zimetengwa kwa ajili ya mashindano hayo kabla ya Taifa.
“Mwaka huu tumefanya tofauti na miaka iliyopita ambapo sasa tumeanzia ngazi za chini ili kuwapata mwachezaji ambao wataliwakilisha taifa kwenye michuano mbalimbali.
“Kabla hatujaanza mashindano ya Taifa kutakuwepo na mashindano ya Kanda ambayo yatashirikisha mabondia au timu zilizofanya vizuri ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa, hao ndiyo watakuwa na sifa ya kushiriki ngazi ya Taifa,” almesema Makore.
Almesema katika Kalenda ya BFT ya mwaka huu, kuna mabadiriko mbalimbali ambayo yanamtaka kila mjumbe wa Kamati ya Utendaji kuwajibika kulingana na majukumu aliyopewa.
“Mwanzo shughuli zote zilikuwa zinafanywa na uongozi wa BFT wakati kuna kamati zake, lakini hivi kuna tofauti katika Kalenda ambapo kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa maagizo ya kamati yake inavyomtaka afanye ili kukuza na kuendeleza mchezo huu,” amesema Makore.

Tuesday, March 26, 2013

KING CLASS MAWE ATAMBA KUMGALAGAZA MWAMAKULA MEI MOSI

SUPER D KUSHOTO AKITOA MAELEKEZO KWA KING CLASS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu  Class 'King Class Mawe' anaendelea kujiandaa 
kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa
bondia wake anajianaa vema kwa ajili ya  kumchakaza Mwamakula bila ya huruma ili
kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D.Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD  za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Fransic Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. nyingine zitakuwa
zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

RAMADHAN KIDO AOMBA KURUDIANA NA MCHUMIATUMBO 'ARIVENJI'



BAADA ya kuchapwa katika mchezo wao wa kwanza uliokuwa na kila aina ya majigambo kwa mabondia, Ramadhan Kido na Mchumiatumbo, hatimaye sasa bondia mbavu nene Ramadhan Kido, anasema kuwa anamhitaji tena mbavunene mwenzake Alphonce mchumiatumbo, ili aweze kumuonyehs akuwa alimuotea na kumchapa kwa bahati mbaya katika mchezo wao ulipita.

Mabondia hao walichapana katika pambano lao la kwanza lililofanyika uwanja taifa na kumalizika kwa Bondia Kido, aliyekuwa amedhaminiwa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, kuchapwa kwa KO,ambapo sasa amepania kulipa kisasi.

''Mchumiatumbo amenifanya nameshindwa kulala kwa muda mrefu sana tangu aliponipiga katika pambano lililopita, jambo ambalo limenifanya kujifua kufa na kupona kujiweka fiti ili niombe marudiano niweze kurivenji.

Siku zote nimekuwa nikimfikiria yeye kanipigajepigaje jibu sipati,nimeamua kurudi tena ulingoni kwa kujipima na Mussa Mbabe, katika pambano letu litakalofanyika siku ya jumapili Aprili 7, mwaka huu katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala.

Najua Musa ni bondia mzuri lakini siwezi kupoteza mara mbili mfululizo huu ni mwiko wangu nitahakikisha nafia ulingoni na ntajituma  kwa nguvu zangu zote na kuhakikisha namchapa kwa KO mbaya, bila huruma hata nikiua sawa tu nina uchungu sana na ngumi na nataka nimuoneshe Mchumiatumbo kuwa nakuja kivingine,na nikipigwa katika pambano la mwananyamala ni bora niache ngumi kabla ya kurudiana na Mchumiatumbo''. alisema Kido

Monday, March 25, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA JITEGEMEE ULIYOKO WILAYA YA MUHEZA MKOA WA TANGA




IDDY MKWELA
BONDIA Iddy Mkwela wa Dar es salaam anatarajia kuoneshana kazi ya kurushiana makonde na Lucas Ndula wa Muheza wakati wa kusherekea sikukuu za pasaka jumapili ya march 31 katika viwanja vya wazi vya Jitegemee vilivyopo wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga

akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano huo wa raundi 6 kg,60 bondia wa siku nyingi ambae kwa sasa ni kocha wa mchezo huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi

ambapo kutakuwa na mapambano mengi ya mchezo huo yatakayoanza saa kumi jioni ikiwa kiingilio ni miguu yako tu amewataka wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kuangalia mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na vijana wengi wilayani humo ndio mana tumeamua kuweka katika viwanja vya wazi ili watu wote wajionee wenyewe mchezo wa ngumi unavyo endeshwa katika mazingira magumu

Nae Kocha wa kimataifa  wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar ili wakalete changamoto na kuleta amasa ya mchezo huo amesema atakwenda na Nassoro Mbwiga atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwela atakaepambana na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

AMOUR MZUNGU AMTISHIA NYAU MARWA


Zungu (kushoto) wakati akipima ubavu na Kiza Kinene (kulia)
BONDIA machachari mwenye makazi yake kisiwani Unguja Amour Said”Zungu”  amejitapa kumpiga vibaya na kumstaafisha ngumi bondia mkongwe aliyewahi kuchukua medali na mataji kadhaa katika ngumi za ridhaa na kuwa bingwa katika ngumi zakulipwa Joseph Marwa katika  pambano litakalofanyika katika ukumbi wa  CCM Mwinjuma-mwananyamala April  7.
Zungu alisema kuwa kwa namna alivyojiandaa atamnyuka Marwa maarufu kama Smart Man'.
"Marwa umri umekwenda, japo alikuwa mwalimu wangu, lakini lazima nimnyuke," alisema.
Mabondia hao watapigana katika pambano la raundi nane na watasindikizwa na mabondia wanaokuja vema katika mchezo huo nchini kwa sasa kama Issa Omar na Shaaban Madilu watakaocheza raundi kumi za ubingwa wa taifa wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO),Ambao upo wazi kugombaniwa na mabondia hao. 
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Saturday, March 23, 2013

CHEKA ADUNDWA KWA TKO NA Uensal Arik WA Germany

BONDIA Francis Cheka march 22 alichezea kichapo cha TKO ya raundi ya saba  katika mpambano wake wa IBF Inter-Continental super middleweight title  

lililofanyika katika ukumbi wa  Universal mjini Berlin, Germany mpambano huo uliokuwa wa raundi 12 ulikutwa unaishia katika raundi ya saba baada ya kupokea kichapo kutoka kwa bondia Uensal Arik 

  bondia huyo aliecheza won 18 (KO 18) + lost 1 (KO 1) + drawn 0 = 19 na kushinda kwa K,O yote ambapo amepigwa mpambano mmoja tu  bondia huyo ambaye ni Germany anaetamba kwa kwapiga watu mnamo raundi za awali tu Cheka amefanya kuwa mtu wa 18 wa kupigwa kwa K,O na bondia huyo

Francis Cheka anaetarajia kuzidunda na Thomas Mashali Mei Mosi mwaka huu katika ukumbi wa PTA sabasaba ameweka doa rekodi yake kwa kupigwa na anatazamiwa kupandisha upya rekodi yake kwa kumpiga bingwa wa Afrika Mashariki Thomas Mashali ili kudhilisha kwamba yeye bado mbabe kwa upande wa Tanzania Cheka mpaka sasa ana rekondi ya won 27 (KO 15) + lost 7 (KO 4) + drawn 1 = 35 

Mpambano huo wa Germany aliocheza Cheka ni mpambano ambao yeye alikwenda kuziba pengo la bondia ambaye alikuwa amepata matatizo katika mazoezi na kulazimika kuziba nafasi hiyo ili mpambano ufanyike mei mosi

Cheka atatetea mkanda wake wa IBF Continental Africa super middleweight title katika mpambano wa raundi 12

Thursday, March 21, 2013

Mnamibia, Mtswana washindwa kutambiana IBF



Mtazania Onesmo Ngowi katikati akiwa na baadhi ya maofisa

LILE Pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na watu wengi wa kumpata Mfalme wa  wa bantam wa kimataifa kati ya mabondia Immenuel Naidjala a.k.a Prince kutoka Namibia na Lesley Sekotswe kutoka Botswana haukuweza kutoa mshondi baada ya matokeo ya majaji wawili kumpa kila mmoja ushindi wana jaji wa tatu kutoa draw.
Pambano hili lilikuwa limeandaliwa na kampuni ya Sunshine Promotions ya bwana Nestor Tobias na lilikuwa na kila aina ya hamasa baada ya mabondia wote wawili kuonyesha ufundi wa kurusha makonde. 
Rais wa IBF kutoka Afrika, Ghuba ya Uajemi na mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa mpambani huu alitangaza kuwa mabondia wote wawili watakutana tena baada ya kipindi cha mapumziko ya mwezi mmoja ili kuweza kumpata mshindi wa mkanda huo ambaoni watatu kwa umaarufu katika mukanda ya ngumi. Mkanda wa kwanza kwa umaarufu ni wa ubingwa wa dunia. Mkanda wa tatu ni wa ubingwa wa mabara na mkanda wa tatu ni wa ubingwa wa kimataifa ambao ndio uliokuwa unagombewa na mabanodia hao. 
Wakazi wengi wa jiji la Widhoek na miji mingine ya jirani pamoja nan chi za jirani walijazana katika hotel ya Widhoek Country Club and Casino kuushughudia mpambani huo ambao ulikuwa na kila aina ya hamasa.

Tuesday, March 19, 2013

BONDIA STAR BOY APANIA KURUDISHA ENZI



Na MWANDISHI WETU
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' ameingia kambini kujiandaa 
SHABANI MHAMILA 'STAR BOY'
kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na  Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa
bondia wao ameingia kambini juzi kujiandaa kumchakaza Jibaba ili
kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya .won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga  Theodor Luanda
Frebruary 2,1996 na kutetea vema
10 Februar1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa 
Super D
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mjapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe

Monday, March 18, 2013

MABONDIA PRINCE NAIDJALA NA SEKOTSWE NUSU WAZIPIGE KAVU KAVU


Immanuel "Prince" Naidjala
Mabondia Immanuel “Prince” Naidjala  wa Namibia and Lesley Sekotswe wa Botswana wamekutana leo katika mkutano wa waandishi wa habari. Kukutana kwao nusura kulete balaa kubwa baada ya mabondia wenyewe kuingia midadi na kutaka kuzipiga kavu kavu mbele ya vyombo vya habari 
Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni moja ya Casino kubwa katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbakl vya habari kutoka nchi za Afrika na Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao walitambiana kupeana mkongoto wa uhakika watakapokutana siku ya jumatano tarehe 20.
Mabondia hao wanakutana tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la kupima uzito kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa nchi ya Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano huo ambao ni mkubwa kuwahi kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili na ushee!
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana kulisimamia pambano hili la ubingwa wa “IBF International Title”
Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo alishughudia mabondia Richard Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako Richard Commey aliibuka kuwa bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.
Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni maarufu ya Sunshine Boxing Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja rekodi ya kuingiza watu wengi zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika nchini Namibia.
Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia kadhaa katika mapambano ya awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia atakutana na Nelson Banda wa Zambia katika mpambano wa raundi 8

Sunday, March 17, 2013

SUPER D KUMPIKA KING CLASS MAWE KWA AJILI YA MEI MOSI


Na MWANDISHI WETU
BONDIA Ibrahimu  Class 'King Class Mawe' ameingia kambini kujiandaa 
kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa
bondia wake ameingia kambini juzi kujiandaa kumchakaza Mwamakula ili
kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D.
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mjapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe.

Wednesday, March 13, 2013

MPAMBANO WA UBINGWA WA IBF AFRICA


MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA MARCH 17 CCM TANDALE



SUPER D BOXING COACH
BONDIA Juma Fundi anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na Hassani Mandula katika mpambano wenye upinzani wa ali ya juu utakaofanyika


jumapili ya March 17 katika ukumbi wa CCM Tandale jijini Dar es salaam 

Akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mratibu wa mpambano huo Dikumbwaya Stamili amesema maandalizi yote yako sawa ikiwemo makubaliano ya mabondia kupanda ulingoni siku hiyo aliongeza kuwa mabondia wote watapimwa uzito na afya siku ya jumamosi katika ukumbi huo huo

Alitaja kuwa mapambano yatakayosindikiza siku hiyo ni Cosmas Kibuga atakaeoneshana kazi na Yohana Mathayo uku Ramahani Pido akioneshana ubabe na Faraji Sayuni pia kutakuwepo na burudani mbalimbali zilizoandalkiwa siku hiyo 


Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Monday, March 11, 2013

RICHARD COMMEY NDIYE MFALME WA UZITO MWEPESI KATIKA BARA LA AFRIKA


International BoxingFederation Africa
IMG_1038.JPGIBF/AFRICA
FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 8th, 2013-Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Richard Commey amedhihirisha uwezo wake wa upigana ngumi wakati alipomtoa kwa TKO bondia Bilal Mohammed na kutangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wills Gym City Engineers katika viunga vya Jamestwon, jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na wapenzi wengi wa ngumi wakiongozwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Ngumi cha Ghana (GBA), viongozi wa Kamati ya Olympic ya Ghana, Meya wa jiji la Accra, pamoja na wWaziri wa Michezo wa Ghana.
Mpambano huo ulianza kwa mbwebwe za aina yake baada ya mabondia wote kuwasili kwenye ulingo wakisindikizwa na mashabiki wao waliokuwa wanacheza ngoma mbalimbali za makabila ya Ghana.
Bilal alianza mpambano katika raundi ya kwanza akikurupuka kutoka kwenye kona yake kama faru na kumfuata Richard kwa nia ya kumsimamisha katika raundi ya kwanza lakini Richard aliweza kuhimili shambulio hilo na kuanza kutoa dozi kwa Bilal.
Katika raundi ya 4 Richard alimpeleka Bilal kwenye sakafu ya ulingo mara mbili kwa ngumi zilizokuwa nzito. Bilal aliweza kuendelea na pambano baada ya kuhesabiwa mara 8! Mashabiki wengi aliuzingira ulingo wakati wote wa mpambano huku wakipiga makalele na ngoma zilizoashia kuwa wawili hao kweli wametawala nyoyo za mashabiki wengi wa ngumi katika nchi ya Ghana.
Mambo yalifikia tamati katika raundi ya saba wakati Richard aliporusha ngumi tatu mfululizo za mchanganyiko na kumpeleka Bilal chini kwa mara ya tatu. Bilal aliamka kwa shida wakati mahesabu ya refarii yalipokuwa yanafikia mwisho na alianza kupepesuka huku refarii akimdaka ili asianguke tena na kuashiria mwisho wa mpambano huo.
Huu ni wakati ambapo Richard Commey alipotangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika na ukumbi mzima kuzizima kwa nderemo na shangwe. Kwa ushindi huo, IBF imempatia Richhard Commey nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito mwepesi mpambano ambao utafanyika tarehe 28 mwezi wa Aprili mwaka huu.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

BONDIA Bernard Hopkins, 48, AMEWEKA record YA KUWA BINGWA WA DUNIA AKIWA NA UMRI MKUBWA

BONDIA Bernard Hopkins

48

amemtwanga kwa pointi 117-111, 116-112, and 116-112. bondia  Tavoris Cloud wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Dunia katika mpambano uliofanyika katika jiji la New York City. na kuweka rekodi ya kuwa bingwa mwenye umri mkubwa kuchukua ubingwa wa Dunia  miaka miwili iliyopita Hopkins alimpiga kwa point bondia machachali Chad Dawson katika mpambano wao wa marudiano na kuwa bingwa wa Dunia Bondia huyo mkongwe aliyeweza kudumu katika masumbwi kwa mda mrefu bondia huyo anaefanya kuwa rekodi yake kwa sasa ni on 53 (KO 32) + lost 6 (KO 0) + drawn 2 = 63  katika michezo yake 63 amepoteza mipambano 6 tu rekoni ambayo inamfanya kuwa juu mpaka hivi sasa



Thursday, March 7, 2013

MTOTO SUZAN KASEBA ASHEREKEA SIKUKUU YAKE YA KUZALIWA

Bingwa wa ngumi za kulipwa uzito wa kati Japhert Kaseba kulia akiwa amemshika mtoto wake Suzan Kaseba wakati wa sherehe ya mtoto huyo kutimiza umri wa miaka 11 iliyofanyika shuleni kwao wengine ni mama yake mzazi Wema Kaseba pamoja na wanafunzi wanaosoma nao darasa moja katika shule ya msingi ST.Josepher .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mtoto Zuzan Kaseba akimlisha keki mama yake Wema Kaseba wakati wa kushelekea sikukuu yake ya kuzaliwa iliyofanyika shuleni kwao ST Josephe juzi katikati ni baba yake mzazi Japhert Kaseba bingwa wa taifa wa mchezo wa masumbwi nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bingwa wa Taifa mchezo wa Masumbwi nchini, Japhert Kaseba Katikati   akilishwa keki na mwanae Suzan Kaseba wakati wa sherehe ya mtoto huyo kutimiza miaaka 11 iliyofanyika katika shule ya msingi ST. Josephe Dar es alaam juzi kulia ni mama yake mzazi Wema Kaseba nae akilishwa keki hiyo.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bingwa wa ngumi za kulipwa uzito wa kati Japhert Kaseba kulia akiwa amemshika mtoto wake Suzan Kaseba wakati wa sherehe ya mtoto huyo kutimiza umri wa miaka 11 iliyofanyika shuleni kwao wengine ni mama yake mzazi Wema Kaseba pamoja na wanafunzi wanaosoma nao darasa moja katika shule ya msingi ST.Josepher .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BABA MWANA NA MTOTO KATIKA PICHA YA KUMBUKUMBU

Mtoto Zuzan Kaseba

Laila Ali 'She Bee Stingin'' BONDIA PEKEE WA KIKE ALIYECHUKUA KIWANGO CHA JUU CHA FEDHA KATIKA WANAMASUMBWI

Laila Ali Curtis Conway Curtis Jr.
Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao
Kwa sasa unakadiriwa pia utajiri wake unafikia kiasi cha dola za kimarekani milioni kumi ambazo ni zaidi ya fedha za kitanzania bilioni 16, ambazo ambazo amezitengeneza kutoka katika mchezo wa masumbwi duniani,

Matangazo ya bihashara, pamoja na kazi ya uwanamitindo 
Kutokana na umaarufu wake katika masumbwi , alijikuta akipata mikataba mbalimbali mikubwa ya matangazo ya biashara  katika makampuni na maduka makubwa Duniani, kama maduka ya kuuza vyakula,nguo na vifaa vya michezo hali iliyompatia nafasi ya kujiongezea kipato chake kwa haraka  leila alianza kujihusisha na masumbwi akiwa na umri wa miaka 15, huku msaada wake mkubwa ukitokea kwa baba yake mzazi ambapo baada ya kuonesha uwezo wake kwa mda mfupi arianza kuingia kwenye mapambano ya kimataifa 



Baada ya kupata ubingwa huo mwaka 2005 aliweza kutoa ubingwa mwingine unaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la ngumi za wanawake ' IWBF kwa kumtwanga Nikki Eplion kwa K,O ya raundi ya nne katika uzito wa female super middleweight title 

Pamoja na uwezo huo, Wapo baadhi ya mabondia wa kike kama Vonda Ward, Leatitia, Robinson na Ann Wolfe wamekuwa wakilalamika kuwa Leila anawakwepa kwa kupangiwa vibonde na kuhofia kupigwa.

Licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa masumbwi, mitindo na matangazo ya biashara kwenye runinga lakini mara kadhaa amekua akialikwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kwa ajili ya vipindi hali inayomfanya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha 

Baadhi ya vipindi hivyo maarufu ni pamoja na agaeorgr Lpez, Dancing with the Stars, American Gladiators,Celebrity Family. The Early Show

Katika historia ya  maisha yake ya ndoa ,leila amesha olewa mara mbili ambapo kwa mara ya kwanza aliolewa na Johnny Mcclain Agost 27,2000,ambaye walikutana kwenye sharehe ya kuzaliwa baba yake mzazi Mohamed Ali wakati anatimiza umri wa miaka 57.

Kabla ya kuoanaMacClain ndiye aliyekuwa promota wake katika michezo ya ngumi za kulipwa jambo ambalo lilimsaidia kufanya vizuri katika mapambano yake yote ambayo ajapigwa wala kutoa droo ata mpambano mmoja akiwa na alama won 24 (KO 21) + lost 0 (KO 0) + drawn 0 = 24  

Baada ya kuoana mwaka 2000 walikuja kuhachana mwaka 2005. mwaka 2007, leila alifunga ndoa na Curtis Conway , ikiwa ni ndoa yake ya pili . wadadisi wa mambo ya kimapenzi wanaeleza kuwa kilichomfanya kuolewa tena ni kutokana na kuwa na mvuto wa kimapenzi alionao mwana dada huyo maili awapo ulingoni,

Leila amefanikiwa kupata watoto watatu akiwa na McClain ambao ni Leilani,Cameron na Kelton. Baada ya kuolewa tena alipata watoto wawili ambao ni Curtis Muhame Conway Aliyezaliwa mwaka 2008 na Sydney  mwaka 2011

Kwa sasa leila amestafu kucheza mchezo wa masumbwi tangu acheze mchezo wake wa mwisho Tareha 3 -2-2007  na Gwendolyn O'Neil na kufanikiwa kumpiga kwa K,O raundi ya kwanza na kutangazwa kuwa bingwa wa mikata miwili ya WBC female super middleweight title
WIBA Women's International Boxing Association super middleweight title
Ingawa kazi kubwa anayofanya kwa sasa ni kutangaza vipindi mbalimbali kwenye television pamoja na mitindo 
Moja ya mambo ambayo yalishangaza ulimwengu katika fani ya mitindo mwaka 2012 akiwa na mimba ya miezi 9, aliweza kushiriki kikamilifu katika maonesho ya mavadhi aliweza kuonesha umahiri wake kwenye jukwaa kwa kupita akiwa kwenye tamasha la mavazi lililofanyika jijini London Nchini Uingereza Novemba 20, 2012

Amestaafu akiwa na rekodi ya kutopigwa ata mchezo mmoja ambapo alicheza michezo  24 alishinda kwa  KO 21 ambapo mabondia watatu pekee ndio aliwashinda kwa point 
huyo ndio leila Muhamed Ali
kwa mahitaji ya DVD ZAKE KWA AJILI YA KUONA MAPAMBANO YAKE MBALIMBALI LIVE TUWASILIANE KUPITIA


Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao