Tangazo

Pages

Wednesday, December 7, 2011

mabondia kupima uzito kesho


MABONDIA Ramadhani Nasibu na Antony Kairuki wa Kenya wanatarajia kupima uzito kesho kwa ajili ya pambano lao la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika litakalofanyika kesho kutwa katika ukumbi wa DDC, Keko Dar es Salaam.

Pamabno hilo lisilo la ubingwa litakuwa katika uzito kg 51 la raundi nane .

Akizungumza Dar es salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Pius Agaton alisema lengo hasa ni kusheherekea miaka 50 ya Uhuru ikiwa ni sambamba na kuwapima ubavu mabondia hao.

Alisema, maandalizi yamekamilika ambapo mabondia wote wanaendelea kujifua ambapo pia bondia huyo kutoka Kenya yupo nchini kwa ajili ya kujiweka sawa ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za kimashindano.

"Naimani mashindano yatakuwa mazuri kwani mabondia wote ni wazuri na wamejiandaa hivyo mashabiki wa subiri kupata burudani hiyo ikiwa ni pamoja na kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru

No comments:

Post a Comment